Njia 14 Halali za Kupata Pesa Kupitia Blog

Je unatafuta njia ya kujipatia pesa kwenye mtandao ambayo siyo ya utapeli? Blog ni njia moja wapo unayoweza kuitumia kujipatia fedha huku ukifanya kile ukipendacho. Katika makala hii nitakushirikisha njia 14 unazoweza kuzitumia kupata pesa kwa kutumia blog yako.
Kumbuka! Hizi si njia za kupata pesa za mteremko haraka haraka kwa usiku mmoja. Kamwe usidanganywe na matangazo ya kuwa utafanywa kuwa tajiri mkubwa siku moja. Mambo hayaendi hivyo.
Awali ya yote utahitaji kuwa na blog yako; pia utahitajika kuwekeza rasilimali ya muda au pesa kiasi fulani ili kuweza kuona matokeo kutokana na blog yako.
1. Kuwa wakala
Unaweza kupata pesa kwenye blog yako kwa njia ya kuwa wakala wa wauzaji wa bidhaa au huduma mbalimbali. Mara mtu anunuapo kitu kwa kukifikia kupitia blog yako basi utapata gawio.
Unaweza kujiunga na huduma hizi ili kuwa wakala:
Amazon
Commission Junction
ShareASale
Baada ya kuchagua bidhaa ya kuitangaza unaweza kutumia ThirstyAffiliates kutawala matangazo hayo.
2. Jiunge na Google Adsense
Kama una watembeleaji wengi kwenye blog yako kuanzia 1,000 au zaidi kwa siku, unaweza kujiunga na huduma hii na ukapata pesa kutokana na matangazo yatakayowekwa na Google kwenye blog yako.
Aina za utangazaji wa Google Adsense:
CPC – Cost Per Click ni matangazo ambayo utalipwa kadri watumiaji wa blog yako wanavyobofya au kuclick tangazo husika. Kiwango cha malipo kwa click hutegemea kiwango kilichowekwa na mtangazaji.
CPM – Cost Per Thousand impressions ni matangazo ambayo utalipwa kutokana na tangazo kuonwa mara 1,000.
3. Njia ya kuweka matangazo moja kwa moja
Unaweza kukubaliana na kampuni husika moja kwa moja kuweka tangazo lao kwenye nafasi fulani ya blog yako. Kwa njia hii unaweza kupata pesa zaidi kuliko kutumia huduma nyingine ambazo ndizo hukubaliana na makampuni husika au mtangazaji.
4. Andika posti iliyodhaminiwa
Hii ni post inayoandikwa kwa lengo la kufafanua au kutangaza huduma au bidhaa fulani. Kampuni husika itakulipa kwa kuandika post inayoelezea na kutangaza bidhaa au huduma yao.
5. Uza blog
Kuuza blog? Ndiyo, kuuza blog kunaweza kukupatia kipato kizuri kabisa. Kama unajua kusanifu na kutengeneza blog, basi unafahamu kitu cha ziada. Kuna watu wengi wanahitaji kununua blog zilizotengenezwa tayari. Unaweza kutafuta anwani nzuri (domain) na kuitengenezea blog kisha ukaiuza kupitia tovuti kama vile Flippa na kujipatia pesa.
6. Tengeneza maudhui ya wanachama
Unaweza ukatengeneza maudhui kwenye blog yako ambayo yanaweza kufikiwa na wanachama waliojisajili tu. Unaweza kupata pesa kwa njia ya kuwatoza ada ya usajili au uwanachama wale wote wanaohitaji kujisajili kwenye blog yako. Kwa njia hii utajipatia kipato moja kwa moja kutokana na wanachama watakaojisajili ili kusoma maudhui hayo.
7. Uza vitabu pepe
Kama una maarifa fulani unaweza kuyaweka kwenye mfumo wa vitabu pepe (e-books) na kuuza vitabu hivyo ili kujipatia pesa. Unaweza ukatengeneza kitabu chako katika mfumo wa PDF na kuwatoza watu kiasi fulani cha pesa ili kuweza kukipakua kama ninavyofanya mimi. Bonyeza hapa uone KITABU: MILIKI KIWANDA MILIKI UCHUMI
8. Uza kozi za kwenye mtandao
Kama ilivyo kwenye swala la vitabu, unaweza pia ukandaa kozi za kuwafundisha watu mambo mbalimbali unayoyafahamu. Andaa kozi vizuri na kwa ubora, zitangaze kwenye blog yako na watu wanaweza kujiunga kwa kulipa ada fulani ambayo itakupatia pesa kama ambavyo mimi ninafanya. Bonyeza hapa uone. PIUS ONLINE COLLEGE
9. Tafuta kazi kwa kuuza ujuzi wako
Kama una ujuzi wa kufanya kazi au jambo fulani unaweza kutumia blog yako kujitangaza na ukajipatia kipato cha kutosha. Watu wanapotembelea blog yako wanaweza kuvutiwa na ujuzi wako hivyo wakakuajiri ili uwafanyie kazi fulani.
10. Kuwa mshauri au kocha
Kama unauwezo wa kuwashauri watu au kuwahamasisha juu ya maswala mbalimbali ya maisha, unaweza kutumia blog yako kufikia wateja wako. Unaweza ukawahudumia kupitia mtandao au ukawaalika moja kwa moja ofisini kwako. Maswala haya yanaweza kuwa tiba, mahusiano, elimu, uchumi, malengo, maono n.k. Unaweza kuwatoza gharama fulani kutokana na huduma husika na ukajipatia pesa.
11. Anza duka la kwenye mtandao
Kama unatumia WordPress kwenye blog yako unaweza kutumia WooCommerce pluginkuanzisha duka la kwenye mtandao na ukauza bidhaa mbalimbali. Kwa njia hii unaweza kuuza bidhaa zako au za watu wengine na ukajipatia kiasi kizuri cha pesa.
12. Uza mavazi yenye chapa yako
Kama unachapa (brand) maarufu ama ya blog au kampuni yako unaweza kuitumia kuuza mavazi na ukajipatia pesa. Unaweza kuuza mavazi yenye chapa yako kama vile tisheti, kofia, mikanda, bangili, mikoba, viatu n.k kupitia blog yako.
13. Uza kazi ya usanifu mtandao
Kama unajua kutengeneza plugins za wordpress, extension za Joomla, violezo (themes/templates) n.k unaweza kuvizua kupitia blog yako na ukajipatia kiwango kizuri cha pesa.
14. Pokea msaada
Hii ni njia ambayo si maarufu sana lakini inaweza kukuwezesha kupata pesa. Umewahi kufikiri tovuti kama wikipedia inajiendeshaje? Inajiendesha kwa kutegemea michango ya misaada ya wasomaji wake. Kama unatoa maarifa au huduma fulani nzuri bila malipo kwanini usiombe msada kwa mtu anayependa kufanya hivyo? Unaweza ukapata kiwango kizuri cha fedha kupitia njia hii.
Hitimisho
Naamini umeweza kufunguka macho na kuona fursa ambazo hukuwa umeziona ua kuzielewa vyema mwanzoni. Ni vyema ukafahamu kuwa hakuna njia ya mkato kupata pesa. Ni vyema ukajitahidi kufanya bidii na kuwekeza muda au fedha kiasi fulani kwenye blog yako ili uweze kujipatia kipato kizuri.

Kama utapenda kuanza kutengeneza jina lako na hatimaye uanze kutengeneza kipato chako kupitia blog wasiliana nasi tuweze kukutengenezea blog simple na nzuri itakayoweza kukutengenezea jina na uaminifu kwa wasomaji wako na hatimaye kukuingizia kipato kikubwa.

Wasiliana nasi kwa whatsapp 0754745798. KARIBU SANA.

Kama umependa makala hii na ungependa kupata makala kama hizi basi download PIUS JUSTUS APP na uweze kupata notification kila mara. Bonyeza hapa chini kudownload moja kwa moja.

Asante kwa kusoma makala haya.
Ni mimi ninayejali mafanikio yako;
Pius J. Muliriye
075474578 | Whatsapp only.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *