Kuhusu PIUS JUSTUS MULIRIYE

Pius Muliriye Justus ni Mtanzania, Mwandishi (Author), Kocha wa Mafanikio(Success Coach), Mnenaji (Speaker) na Mjasiriamali.

Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kwa kupitia Kazi Zake Maisha ya wengi yamekuwa bora na kufanikiwa.

Kwa kupitia kazi yake ya Uandishi pekee ameweza Kuwafikia maelfu ya watu kwenye mitandao ya kijamii na kufikia kualikwa kufundisha vijana, pia kualikwa kwenye vipindi vya Redio na Tv mbalimbali hapa nchini.

Pia makala zake zimeandikwa katika magazeti mbalimbali hapa nchini. Masomo ambayo amekuwa anafundisha zaidi ni Juu ya Kutambua Kusudi Lako, Kuwa Bora na Kutimiza Ndoto.

Ni mwanzilishi wa Think Big Start Small ambayo inawasaidia watu kujitambua, kujua makusudi yao ya kuwepo hai na umuhimu wa kuwaza makubwa huku wakianza na kitu kidogo walichonacho  na kutimiza ndoto zao, na pia inaendesha semina na mafunzo mbalimbali kwenye mtandao.

Ni Mkurugenzi waPIUSJUSTUS.COM ambayo inahusika na Kutoa  elimu mbalimbali ya Ujasiriamali.

Pius Alianza Uandishi kwenye mitandao ya kijamii mwaka 2009, pia kabla ya hapo ilikuwa ni tabia yake kuandika nukuu fupi fupi na kuwatumia watu kwa njia ya sms.

Aliandika Kitabu chake cha kwanza mwaka 2013 kijulikanacho kama MILIKI KIWANDA MILIKI UCHUMI ambapo baadae mwaka 2018 kilibadilishwa na kuitwa BIASHARA ENDELEVU KATIKA MAZINGIRA YAKO.

Kuendelea Kujifunza Tembelea Website Hii Kila Siku.

Facebook

Tufatilie kupitia PAGE yetu ya FACEBOOK inayoitwa THINK BIG START SMALL kwa kubonyeza hapa.

Instagram

Tufatilie kupitia PAGE yetu ya INSTAGRAM inayoitwa @piusjustusmuliriye kwa kubonyeza hapa.

Youtube

Tufatilie kupitia CHANELL yetu ya YOUTUBE inayoitwa PIUS JUSTUS MULIRIYE kwa kubonyeza hapa.