Hakuna mtu ambaye ni mkamilifu katika maisha yake, na haimaanishi wewe kutokuwa mkamilifu huna cha kumsaidia wengine.Kila chenye pungufu kina sehemu flani ambayo ni lulu katika maisha yake na ya wengine.
Usidhani mtu kuwa na mapungufu Mungu hawezi kukuona na kukutumia kufanya mambo makubwa. Nikupe mfano mmoja wa Zakayo mtu mfupi aliyekuwa mtoza ushuru na mtenda dhambi,unadhani Zakayo angelalamikia ufupi wake katika makutano ya watu angeweza kupanda mti na kumwona Yesu, unadhani angelalamika kuhusu dhambi zake hata angethubutu kuwa na kiu ya kumwona Yesu.
Lakini sasa tazama ilivyoajabu kwamba licha ya mapungufu yake na wingi wa watu waliokuwa wakimfuata Yesu kiu aliyokuwa nayo Zakayo licha ya kuwa mtu wa dhuluma lakini Yesu aliweza kugeuka na kumwita na kumwambia kwamba atakuwa mgeni nyumbani kwake kushiriki nae chakula (spiritual connection).
Ufupi wa Zakayo ni mapungufu yako,ufupi wa Zakayo ni matatizo ambayo unapitia,ufupi wa Zakayo ni shida ambazo unakumbana nazo bila kikomo lakini kumbuka ufupi huu usiwe kikwazo cha wewe kudhubutu kama Zakayo aliamua kuthubutu kupanda mti kumwona Yesu hata wewe sasa ni wakati wa kuchukua hatua zaidi ya changamoto zako, sasa ni wakati wa kuwa na Akili Ya Ushindi katika kila jambo ambalo unaligusa ili Mungi aweze kukutumia.
Nikwambie kitu kimoja kwamba Yesu alivyokuwa akichagua mitume wake 12 hakuangalia dhambi walizokuwa nazo naimani alikuwa ndani ya mioyo ya watu na kuamini kwamba kila mmoja anaweza kubadilika na kuwa zaidi ya matendo yake mabaya aliyokuwa akitenda. Wewe na mimi sasa ni wakati wetu wa kutumiwa na Mungu kufanya mambo makubwa yasiyo na kikomo katika maisha yetu.
Usiache kusubscribe kwa kuingiza email yako hapa, kumbuka ukishabonyeza SUBSCRIBE nenda kwenye email yako kisha bonyeza link uliyotumiwa na utakuwa tayari uko karibu na mtandao huu.
Ni mimi mpenda maendeleo yako.
PIUS JUSTUS MULIRIYE
0657128567
0754745798-Whatsapp.