Habari rafiki yangu, naamini uko vizuri na unaendelea na harakati za kuboresha maisha yako.
Leo napenda kukushirikisha umuhimu au faida iliyo katika kazi ya KUJITOLEA.
Kujitolea ni kitendo cha kuamua au kuomba kufanya kazi flani bila ya ujira au malipo yoyote yale. Nimekuwa nikizungumzia sana hili hasa pale napokuwa nawashauri vijana ambao wamehitimu mafunzo mbalimbali vyuoni.
Kujitolea ndio njia pekee inayofanya kazi kwa mtu anayehitaji ajira, kwani kwa kufanya hivo utaonekana unapenda kweli kufanya kazi hiyo japo bila malipo.
Hili si jambo la kawaida sana kwa vijana wa kitanzania walio wengi kwani huwa hata tukipewa kazi huwa tunauliza utanilipa Shilingi ngapi?
Chukua mfano huu na ukufundishe juu ya umuhimu wa kjitolea kama njia ya kupata ajira.
Huyu unayemuona kwenye picha ni kijana aliyehitimu mafunzo yake ya chuo kikuu cha dodoma katika taaluma ya ualimu.
kama mnavyofahamu, sasa hivi kuna shida sana ya ajira hasa kwa wahitimu waliokuwa wakitegemea kuajiriwa moja kwa moja, lakini mambo yamekuwa tofauti sana na wengi kuihia mtaani.
Kijana huyu aliamua kujitolea kwenye moja ya shule alizowahi kufanya mafunzo yake kwa vitendo (FIELD) na kwa bahati nzuri alikutwa na Mh. Mkuu wa mkoa wa Mwanza akifundisha bure kabisa, pale pale akapewa taarifa njema za kupatiwa kazi rasmi na sasa ataanza kulipwa rasmi.
SOMO:
“Fanya kazi kwanza, pesa zitakuja zenyewe”
Nawashauri vijana, jitolee, unaweza usipate bahati kama ya kijana huyu haraka kama unavyofikiria, lakini katika kampuni ile au taasisi ile akihitajika mtu wa kufanya kazi pale utakumbukwa kwanza kabla ya kufikiria wengine ambao hawajawahi kufanya kazi pale.
JITOLEE….Na hiyo ndio siri ya kupata kazi.
Asante kwa kuwa na mimi, Tafadhari usisahau kusubscribe hapa chini ili uwe ukipata makala mpya kila siku zinapowekwa humu.
Unaweza kuwasiliana nasi;
Pius J. Muliriye
0754745798
0657128567
piusjustus28@gmail.com