Habari rafiki;
Natumai uko vizuri na unaendelea na majukumu yako ya kila siku. Asante sana kwa kuendelea kuwa na mimi kila siku, umekuwa ukisoma makala zangu hapa na hata kusikiliza na kuangalia video zangu Yutube, asante sana kwa hilo.
Leo napenda kukushirikisha msomaji wangu aina ya mtaji ambao kila mtu anao lakini hatuna uwezo wa kuudhibiti kabisa.
Mtaji huu wa kipekee unaogusa watu wote, lakini usioweza kuudhibiti bali kujidhibiti wewe mwenyewe uutumie vizuri, mtaji huo ni MUDA.
Kwa mjasiriamali halisi Muda una thamani kubwa kuliko mtaji wa kifedha au vifaa ulivyonavyo.
Mmiliki wa muda na anayeweza kuudhibiti ni Mungu muumbaji pekee.
Tunaweza kuutumia vizuri lakini si kuudhibiti, yaani, kuurefusha zaidi au kuupunguza. Adui wa mafanikio yetu Shetani anapenda tuutumie vibaya. Hapo ndipo unakuta wengi wamapoteza mitaji ya kifedha kwa kuwa hawakutumia muda vizuri.
Wamechelewa kutuletea bidhaa na huduma zao; huku wakiendelea kudokoa pesa za mtaji. Mwisho wake wenzao wakatuletea bidhaa zao, wao wakabaki wanashangaa.
Kumekuwa na misemo mingi sana kuhalalisha matumizi mabaya ya muda, kwa mfano utawasikia watu wakisema NO HURRY IN AFRICA. Hii ni misemo ambayo inawafanya watu washindwe kutumia muda wao vizuri na hatimaye kuharibikiwa kwenye maisha.
TAFAKARI
Je, ni kweli kwamba muda hauna thamani Africa?
Na kwako je? Ni kwa nmna gani unaweza kuboresha matumizi ya muda? Endapo ungeulizwa swali hili, “kati ya muda na pesa ni kipi kitumike kwa uangalifu?” Ungelijibuje? Na kama ukilazimishwa kutumia vibaya muda wako na kufuja rasilimali nyinhine ungefanyaje?
Asante kwa kuwa nami mpaka sasa.
Kama wewe ni mjasiriamali au mfanyakazi na ungependa kuongeza kipato kwa kujifunza jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali basi nakushauri upate KITABU HIKI ambacho kitakufundisha hatua kwa hatua utengenezaji wa bidhaa kama sabuni za mche, sabuni za unga, sabuni za maji, chaki, shampoo na bidhaa nyingine zaidi ya 15 ukiwa nyumbani kwako kwa teknolojia rahisi sana.
Kitabu hiki kipo kwenye mfumo wa softcopy ambao utaweza kusoma kwenye simu yako hiyo au kompyuta yako. Kitabu hiki kinauzwa sh. 5000/- kama utataka nikutumie kwa WHATSAPP au EMAIL yako, lakini utakipata kwa sh. 1000/- tu ukikinunua kwa njia ya mtandao, yaani kulipia mtandaoni na KUDOWNLOAD mwenyewe ambayo ni njia rahisi sana. Unachotakiwa ni kubonyeza Picha hii hapa chini kisha utalipia Sh.1000/- kwa MPESA au TIGO PESA na utapewa link ya kudownload.
Bonyeza picha hii sasa kupata ofa hii.