TUMIA MITANDAO YA KIJAMII KWA MANUFAA.

Je! umeshawahi kuchunguza ni page gani ulizozifaata zaidi kwenye mitandao ya kijamii? Je, ni page za udaku, au habari tu, au za marafiki wengi na wengineo hata wasio na utaratibu katika vitu wanavyopost, au za mafundisho yanayokujenga na kukuinua katika kufikia ndoto yako?

Utafiti wangu husio rasmi unaonyesha, karibu 85% ya watanzania wengi wanapenda kufaata au kufatilia habari au page za udaku na umbea. Leo amua kuchunguza akaunti yako na angalia ni watu wa namna gani ulioamua kuwafuata zaidi mitandaoni.

Mwalimu wa mafanikio Jim Rohn aliwahi dhahiri kusema,“Mtu anakuwa vile alivyo kulingana na marafiki watano anaofatana nao muda mwingi.”

 Marafiki zako ni pamoja na wale ulionao mtandaoni. Hao nao wanasehemu kubwa ya kukujenga au kukuharibu kimtazamo na kifikra kulingana na vitu wanavyotuma au kupost kwenye page zao.

Leo nakusihi amua kupunguza page ulizofaata za udaku na amua kuongeza page mpya zinazotoa mafundisho ya kukusaidia na kukuinua katika maisha yako. Amua kwa dhati kubadili tabia kwa kuwa karibu na watu chanya wanaoweza kukujenga na kukuinua kiroho, kifani, kiakili na hata kiuchumi.

Kumbuka “usidanganyike mazungumzo mabaya uharibu tabia njema” Leo amua kubadilika na kugeuza maisha yako kwa kuamua kuwa karibu na watu waliobeba hatima njema ya maisha yako.

KAMA HUKUONA BAADHI YA VIDEO YUTUBE, UNAWEZA KUANGALIA HAPA

Tafadhari naomba ujiunge ili upate  makala hizi kila siku kupitia email yako.

Wako katika mafanikio

PIUS JUSTUS MULIRIYE
0754745798
0657128567
piusjustus28@gmail.com

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *