HUYU MTU NDIYE ADUI WA MAENDELEO YAKO.

Habari rafiki yangu na msomaji wa mtandao huu wa SHULE TANZANIA

Nipende kukushukuru kwa kuendelea kutembelea ukurasa huu na kurasa zangu zote mitandaoni na kufatilia mafunzo yangu ambayo nimekuwa nikiwapa kila siku juu ya namna mbalimbali za utengenezaji wa Bidhaa mbalimbali za viwandani kama vile Sabuni za mche, sabuni za Unga, sabuni za maji, chaki, n.k. na pia nikushukuru kwa kuweza kununua kitabu changu cha MILIKI KIWANDA MILIKI UCHUMI ambacho kinafundisha mafunzo yote hayo niliyoyataja. Kama hujapata kitabu hicho na ungependa kujifunza pia ujuzi huo ili uweze kuongeza kipato zaidi basi wasiliana nami Whatsapp 0754745798.

Baada ya kusema hayo, naomba tuendelee na mada yetu ya siku ya leo;

Image result for bad person to your development

Katika maisha ya mwanadamu kufikia malengo yake kuna changamoto nyingi sana anapitia. Changamoto hizo huwa hazimwachi salama (kama waswahili wasemavyo). Wengi wamekuwa wakishindwa kuendelea na kuendeleza mawazo (idea) zao na kurudi nyuma kabisa.

Watu wengi wamekuwa wakianzisha mambo mbalimbali ya kibiashara lakini wanashindwa kufikia malengo yao kwa sababu ya kukosa usaidizi au kutiwa moyo na wale wanaowazunguka. Ndugu yako au mtu wako wa karibu huwa ndo watu walioko mstari wa mbele kukurudisha nyuma kabisa.

Wengi wao huwa hawapendi kabisa kuona watu wao wa karibu wanafanikiwa katika biashara zao, wanapenda kuwaona wakishindwa kufikia malengo yao na hufurahi zaidi pale wanapoanguka chini.

Wakati mimi naanza harakati za kuelimisha watu kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii (online) watu wengi wa karibu wamekuwa hawanielewi na wala hawanipi moyo kwamba ipo siku nitafaidika na swala hili. wengi wao wamekuwa wakinibeza sana, lakini nimekuwa nikijitahidi sana kusonga mbele, ilifikia mahali nikataka kukata tamaa, kuna wakati nilikuwa nikipost mafunzo flani hakuna mtu anaye like wala kukoment kwenye post yangu hata wale watu wangu wa karibu.

Hii ilinikatisha tamaa, lakini baba yangu alivyosikia kuwa kuna vitu nafanya mtandaoni baada ya kuambiwa na baadhi ya rafiki zake wanaoniona, alinipigia simu AKINIPONGEZA na akanisihi niendelee hivohivo nitafanikiwa. Maneno yale yalinifanya nisahau rejections (kukataliwa) zote zile na kukaza buti, hatimaye nikapata kuaminiwa na watu waliokuwa wakisoma post zangu na kutembelea blog yangu, na hivi sasa nina followers zaidi ya 30,000 mtandaoni nikiwa na email list ya watu 13,256. 

Leo hii nimeweza angalau kutengeneza shilingi ya ziada kupitia mtandao, watu wamekuwa wakinilipa kwa huduma mbalimbali nazotoa, na namshukuru Mungu, sikukatishwa tamaa na watu wa karibu niliwapuuza na kusonga mbele.

Nataka nikwambie kijana mwenzangu unayetaka kuanzisha kitu flani usiangalie ni watu wangapi wanakubeza, naamini wengi hawatapenda maendeleo yako, lakini sikiliza sauti sauti ya mtu mmoja ambayo itakwambia unaweza na ifanyie kazi, utafikia malengo yako haraka sana.

Naomba niishie hapa kwa leo, lakini nikusihi sana, chunga sana watu wako wa karibu, inaweza ikawa rafiki zako, ndugu zako na hata jamaa zako, wakikwambia huwezi, sema kwa yeye anitiaye nguvu NITAWEZA.

Nimefanikiwa kujifunza mbinu mbalimbali za kuweza kutumia mitandao ya kijamii na internet kwa ujumla kutengeneza kipato cha ziada na hata ukaifanya kama kazi yako, na ndo mbinu nazotumia kila mara kutengeneza pesa nikiwa nimekaa ndani kwangu, chumbani kwangu na hata sebuleni kwangu huku simu yangu ikipokea pesa kutoka pande mbalimbali za dunia hii, kama utahitaji kujifunza mbinu hizo na uko serious wasiliana nami kupitia whatsapp 0754745798 ukiandika neno ONLINE BUSINESS, nitakushauri nini ufanye bure kabisa na baada ya hapo njitakusaidia kukuza kile ambacho unataka kukifanya mtandaoni kupata pesa.

Karibu ujiunge na huu ulimwengu wa kidigitali kukufaidisha na acha kupoteza muda kupitia facebook na magroup mbalimbali ya whatsapp bila faida yoyote.Nikutakie kila lakheri;
Ni mimi mpenda maendeleo yako;

PIUS JUSTUS MULIRIYE
0754745798
0657128567
piusjustus28@gmail.com

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *