HII NDIO MIFANO YA UBUNIFU KATIKA KUJIINGIZIA KIPATO

HII NDIO MIFANO YA UBUNIFU KATIKA KUJIINGIZIA KIPATO

‘’Maelezo yakikosa picha, ni rahisi kuyasahau. Si lazima picha iwe katika umbo Fulani, hata maandishi yanaweza kubeba picha halisi ya kitu yunachojifunza’’


Ubunifu unalenga kuleta suluhisho la matatizo ya pande mbili muhimu. Upande wa kwanza ni ule wa kwako na upande wa pili ni watumiaji wa kile unachobuni. Unapokuwa na nia ya kuishi kwa kujipatia mahitaji yako vizuri; siri ya kutatua shida zako inabaki moyoni.

Baada ya hapo wafikirie wengine uondoe baadhi ya shida zao. Tutaona mifano ya ubunifu unaoweza kuondoa shida za wengine. Matatizo ya wengine yanatoa ajira kwako.

Bosi wa biashara yako ni Yule anayeiona biashara yako kama mkombozi wa shida zake. Vitu vinavoondoa kero au matatizo kwa watu ni vingi mno na kwa kuwa matatizo nayo ni mengi pia.  Usipoweza kutoa huduma au bidhaa kwa watu wengine unadhani ni nani atakayekuwa tayari kukupatia fedha zake ukazitumie kuondoa matatizo yako?

Hii ni mifano ya watu waliotumia ubunifu kutengeneza kipato;

JOHN; MKAZI WA DAR ES SALAAM
Alipokuwa na umri wa miaka 7, John alijitambua kuwa hana baba wala mama. John alitambua wazazi wake si hao aliokuwa naishi nao. Kumbe wazazi wake walifariki kwa ugonjwa wa ukimwi angali mtoto mdogo. Alikuwa akinyanyasika kwa wazazi wa kambo. Akaamua kutoroka nyumbani, awe mtoto wa jamii au mtoto wa mitaani.

Alipochoka kuombaomba huko mtaani, akagundua kuwa, endapo atakuwa na kopo lenye maji, sabuni ya unga, kipande cha godoro na ‘wiper’ anaweza kusafisha vioo vya mbele vya magari, yanapokuwa kwenye foleni yakisubiri kuruhusiwa na taa za usalama barabarani.

Basi, alianza kusafisha vioo vya magari madogo kama matatu hivi na kujipatia sh. 200/- kwa kila gari yaani sh. 600/- kwa kila zamu ya kusimamishwa kwa magari katika barabara aliyopo. Alipata Tsh. 210000/- hadi Tsh. 240,000/-

Ebu jiulize, huu ubunifu si umeleta tija kwa John? Kiasi hicho cha pesa kinaweza kikawa sawa au kikazidi mshahara wa baadhi ya wafanya kazi wa umma.
Hii ndio nguvu ya ubunifu. Ebu jiulize, ni kitu gani unaweza kukifanya na kutatua tatizo la watu na utengeneze pesa zaidi?

kama ulipitwa na video hii, basi nimekuwekea hapa, iangalie unaweza kujifunza kitu;

Asante kwa kuwa nami;
Nakutakia mafanikio mema na utekelezaji mwema;
Wasiliana nasi;
Pius J. Muliriye
0754745798/0657128567

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *