SONGA MBELE

‘’Maishani unaweza kushindwa mara nyingi, kamwe usisalimu amri. Kweli, lazima ushindwe mara nyingi ili uweze kujitambua, ili uweze kujua unaweza kubadilika kuwa nani na kujua jinsi ya kujitoa katika kushindwa huko.’’
      Umeweza kuwa umelifanya jambo la kukupeleka kwenye mafanikio kwa muda mrefu lakini huoni mwisho, huoni utafanikiwa lini. Naomba uwe mvumilivu, vuta subira, muda si mrefu utafika unakotaka kwenda vizuri, maisha ya kukumbukwa hata miaka mia moja ijayo.

  • ·  Safari ya kutafuta mafanikio si lelemama! Ni safari ngumu inayohitaji watu waliodhamiria kufika kileleni. Wengi wetu hatuko tayari hata kidogo kufuata barabara ya kawaida, tunataka njia za mkato. Hatuna uvumilivu ila tunataka njia za mkato. Hatuna uvumilivu ila tunataka mambo yatokee haraka kama tunavyotarajia.
  • ·        Yakichelewa kidogo tu tunaacha na kusema hili haliwezekani, kasha tunaanza kitu kingine. Hicho nacho kikichelewa tunaacha! Tumekuwa kina Bwa/Bi kuanza na kuacha.
  • ·  Ndugu zangu, kama tunataka kufanikiwa ni lazima tuwe wavumilivu. Humchukua mwanamke muda wa miezi tisa kupata mtoto. Katika muda huo atakuwa na kichefuchefu, uchovu, kutema mate ovyo, hasira na mambo mengine mengi ya kufanana na hayo ambayo ni lazima ayavumilie kama kweli anataka mtoto.
      unaweza kupata kitabu hiki na ujifunze utengenezaji wa bidhaa mbalimbali na uwe mfanya biashara mkubwa, bonyeza picha hii KUDOWNLOAD

Asante kwa kuwa nami;

Nakutakia mafanikio mema na utekelezaji mwema;
Wasiliana nasi;
Pius J. Muliriye
0754745798/0657128567

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *