DOGO HASSAN MWENYE MIAKA 12 AWA MJASIRIAMALI ALIYEAJIRI WENZAKE

DOGO HASSAN MWENYE MIAKA 12 AWA MJASIRIAMALI ALIYEAJIRI WENZAKE
________________________________________

Siku ya Jumamosi ya tarehe 22.7.2017 nilikuwa maeneo ya Viwege.Kwa wale wasioifahamu Viwege iko Jijini Dar es salaam Eneo la Kinyamwezi kama unaenda Chanika.

Nilikuwa huko kwa ajili ya kikao na baada ya kikao Rafiki yangu Mnepo Ezekiel alinisindikiza kuelekea kituo cha magari yaendayo Rada (Majohe) kwa kuwa nilipaswa kuonana na MTU mwingine huko.

Wakati tunaenda kituoni niliwaona vijana wadogo sana(Picha yao imeambatanishwa) ambao walikuwa wanatengeneza majiko ya kupikia.Rafiki yangu Mnepo akanieleza kuwa watoto wale ndio wanaojiongoza kutengeneza majiko hawana MTU mwingine.

*”Naomba twende pale pale nijue wamewezaje wakati tuna watu wazima wengi wanaosema hawana cha kufanya”* .Nilimuomba Rafiki yangu .Basi tulienda mpaka pale walipokuwa wakitengenezea majiko Yale .

Kijana aliyejitambulisha kwa jina la HASSAN mwenye umri wa miaka kumi na mbili akiwa anasoma shule ya msingi Viwege nilipomuuliza kwa nini wanafanya kazi ile alikuwa na haya ya kusema *”Sipendi kuzurula na kuomba omba.Wakati ninapopata nafasi na hasa weekendi,natumia muda huo kutengeneza majiko yangu”*.???

HASSAN nilipomuuliza wapi alipata mafunzo Hayo alisema *”Kuna watu waliniambia kuwa shirika la kusaidia viwanda vidogo(SIDO ) walikuwa wameandaa mafunzo ,na Mimi nikawa nimeanda pamoja na wadogo zangu hawa na baada ya mwezi mmoja kwa kuwa vichwa vitu vinashika haraka tulielewa haraka na baada ya mwezi mmoja tulikuwa tumeshafahamu vizuri”*.

Alipoulizwa swala la masoko (Wateja) HASSAN alijibu *”Huwa watu wananipa Oda na wakati mwingine tunayepeleka pale Viwege Sokoni”*.

Akielezea anavyomudu masomo na kazi HASSAN alisema *”Najitahidi sana kusoma kwa bidii lakini pia kuendeleza ujuzi huu maana baada ya shule utanisaidia na hata sasa mahitaji ya shule napata kupitia kazi hii ambayo naifanya muda wa ziada”*.

Ukweli nilifurahi kukutana na vijana wadogo wale nikaamini kama tutawajengea uwezo watoto tunaweza kuandaa kizazi kijacho kinachotatua matatizo badala ya kuwa na kizazi kama cha Leo kilichojaa lawama,mitazamo hasi na malalamiko kikao huku wakiwa wamezungukwa na kila kitu.

Si ajabu kumsikia Meneja wa kampuni  hapa Tanzania hajui nini SIDO wanafanya lakini mtoto mdogo HASSAN amejua nini SIDO Wanafanya akiwa darasa la Saba.Huwezi kushangaa msomi wa chuo kikuu aliyesoma uhandisi(engineering) naye akilalamika kuwa kakosa kazi.

*”Tuamke sasa”*

Joas 0656110906

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *