JIKUBALI,ANZA SASA,HUJACHELEWA.

”Sometimes we don’t Understand why are we in the positions we are, till  we find/meet our testominies”

Unaweza kuwa kijana msomi na mwenye ndoto nyingi na malengo makubwa.Wakati mwingine unafikiri kwamba kikwazo ni aina ya elimu uliyonayo.

Wakati mwingine unafikiri kwamba usingesoma kozi ya ualimu labda ungekuwa mhandisi wa kampuni kubwa sana na hiyo inapelekea ufikiri na kuutazama muktadha ulionao katika mtazamo hasi na kufikiri hali uliyonayo imekuwa kikwazo kwa muda mrefu kutokana na nafasi uliyonayo au aina ya elimu uliyo nayo.

Ni aghalabu kwa mwanadamu kufikiri ya kuwa kile alichonacho hakifai.Ndio maana una mwanamke mzuri ndani kwako anakila kitu unachohitaji lakini bado ”unachepuka”.Unaweza kuwa mfanyakazi mkubwa katika serikali lakini bado katika mazungumzo unatamani kuwa ni bora ungekuwa mfanyabiashara.

Wanadamu wamekuwa na kawaida ya kuponda vile walivyoanvyo,mwalimu aliyesoma kwa miaka mitatu chuoni akifurahia ”semester” zote leo anasimanga taaluma yake bila kufahamu madhara anayopata katika ubongo juu ya kutengeneza chuki inayopelekea kuutazama ualimu kama mzigo(suala hili hutengeneza aina ya uvivu na fikra mbaya juu ya kile unachokitamka vibaya). Matokeo yake unakuwa ”less productive” katika eneo taaluma yako.

Binafsi nimekuwa nikijiuliza ni kwanini nilisoma kozi ya Project Planning and Management kwa miaka mitatu lakini nimekuwa kwa muda mrefu sioni faida yake katika maisha yangu ya kawaida? Kwanini nimemaliza miaka mitatu chuoni lakini ujuzi niliopata bado haujazaa matunda ya kujivunia katika maisha ya kawaida.

Baada ya miaka takribani mitatu ya kuandika ”proposal for funds” bila mafanikio au kwa mafanikio kidogo sana,sasa nimeona maana na tafsiri ya kusoma Project Planning and Management(Development Economics).Nazikumbuka siku za Madam ZEMBA akifundisha Monitoring and Evaluation of Development Projects.

Sasa naona uzuri wa kusoma kile nilichokipenda katika fikra zangu sasa,naiona kesho ikipendeza baada ya kuwekeza katika uvumilivu wa miaka mitatu ya kujifunza katika taasisi mbalimbali na NGOs mbalimbali.

Sasa nayaona mashirika yakitangaza kazi za wakimbizi ambazo asilimia 70% za maofisa wao wanahitaji ripoti na maandiko ya watu waliosoma PROJECT MODULES,sasa naona mwanga wa andiko la page 3 kuzalisha EURO 32,000.00 bila kupepeta midomo.

Sasa naona ofisi yangu(laptop yangu) ikiandika ripoti 6 kwa mashirika ya kimataifa juu ya kazi zilizotekelezwa.Naiona kesho iliyotofauti na leo,nawaona ”donors” kupitia kalamu ya mkono wangu,naziita funds kupitia buttons za kompyuta yangu.

Kesho yako inategemea fikra na ukomavu wa uvumilivu wako,maisha yako yanategema ubunifu na namna unavyoongeza thamani ya elimuu yako.Wakati unapoteza muda katika ”groups za whatsapp” kwenye smartphone yako kuna mtu anatafuta ”scholarship” na nafasi ya kazi kupitia ”zoom Tanzania”.

JIPANGE,JIFUNZE,JIPE MUDA,Utafanikiwa.

JIKUBALI,ANZA SASA,HUJACHELEWA.

#bRAND yOURSELF..

BUNGUBULIHO Jnr.

ALL RIGHTS RESERVED 2017

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *