HIKI NDICHO KITAKACHOKUFIKISHA KATIKA KILELE CHA MAFANIKIO.

KILE UNACHOKIPENDA.
Ili kuwa mtaalamu Fulani, tambua kile unachopendelea. Kitu hicho kimo katika kuhudumia wengine, hakiko katika kuhudumiwa wewe mwenyewe. Hakiko katika yale unayoyachukia. Kwa mfano, wengine hawatakuwa wauguzi endapo wanakuza hisia za kinyaa kusafisha vidonda. Wengine hawawezi kuwa waalimu endapo hawakuzi uvumilivu na utiaji moyo katika kushughulika na wanafunzi. 











Mama lishe anaweza kukuza ujuzi wake endapo anafurahia kuona walaji wanashiba na kufurahia chakula chake, na namna anavyo wahudumia.
Kipaji au talanta ya mama lishe ingekuwa haraka kama walaji wa chakula chake wangekuwa wazi. Hula na kuondoka kimyakimya. Hawako wazi. Endapo wangelikuwa wanashukuru na kuelezea kile kinachowaridhisha na kile kinachowakera katika ujuzi wake wa kuandaa chakula; angelikiboresha zaidi.

Pale mtu anapopongezwa, napopongezwa, anapotiwa moyo na siyo kusifiwa; akili yake huhamasika kuboresha utendaji wake.
Ingawa wapongezaji na watia moyo wanazidi kupungua kutokana na kuongezeka kwa ubinafsi. Jipime mwenyewe ikiwa ungeliridhishwa na ubora wa huduma au bidhaa yako. Wahimize wateja waeleze kile wanachodhani kingeboreshwa zaidi.

Kile kizuri unachopenda, wapo watu wanakipenda pia. Ukifanikiwa kukitoa kwa wingi, utafanikiwa katika maisha. Ukifanikiwa kukiboresha, utakuwa mtaalamu.  Wataalamu wengi wana maisha mazuri; kwa kwa wanahudumia watu wengi vizuri. Maisha mazuri hutokana na kuhudumia watu wengi vizuri. Ili uhudumie watu wengi vizuri, kuwa mtaalamu mahiri.


Asante kwa kuwa nami;


Nakutakia mafanikio mema na utekelezaji mwema;
Wasiliana nasi;
Pius J. Muliriye
0754745798/0657128567

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *