SIRAHA HAZITENGENEZWI WAKATI WA VITA

SIRAHA HAZITENGENEZWI WAKATI WA VITA

NIMEKUSOGEZEA VIDEO INAYOFUNDISHA JINSI YA KUTENGENEZA BIDHAA MOJA INAYOTUMIKA SANA KWENYE JAMII ZETU KILA SIKU NA YENYE SOKO KUBWA SANA NA NI MOJA YA PRODUCT KATI YA PRODUCT 12 ZILIZOPO KWENYE KITABU CHANGU CHA MILIKI KIWANDA MILIKI UCHUMI.

UNAWEZA KUIANGALIA HAPA KABLA HUJASOMA MAKALA YA LEO.
Habari ndugu msomaji wa makala zangu nimatumaini yangu makubwa sana kuwa unaendela vyema kila iitwapo leo,nikupongeze tena kwa maamuzi uliochukuwa siku ya leo kwa kuweza kusoma tovuti hii ili uweze kujifunza zaidi na ninaimani haswaa utajifunza mengi kupitia safu hii.

Leo nataka nikukumbushe wewe ambae unasubiria siku ifike kwenye maisha yako ndio uanze kuchakalika,nataka nikupe usemi mwepesi tu siku zote kwenye maisha siraha huwa hazitengenezwi wakati wa vita bali siraha huwa zinatengenezwa wakati wa furaha.

Lakini siraha hizo hizo ndio zinatumika wakati wa vita.Huenda ukawa hujanielewa nini namaanisha nikwamba maisha hayaanzi kutafutwa ukishazeeka au ukishastafu kazini.Kuna tabia ambayo imezoeleka kwa mfano kwa wafanyakazi unakuta wafanyakazi wengi anafanyakazi malengo yake anasubiri akistafu achukue mafao eti ndio aanze kufanya biashara,hajajiandaa mapema anasubiri ameshazeeka ndio anaanza kukimbizana kwa kiasi kikubwa atafeli tu,kwanini hakujiandaa kipindi akiwa kazini?

Kuna watabia ya wanafunzi wanasoma kipindi cha mitihani kwanini hujiandai mapema,rafiki maisha ni vita na siraha zake haziandaliwi wakati vita ikishaanza bali wakati vita hakuna,anza leo kujipanga kama unataka kuwa mjasiriamali anza leo kutafuta maarifa ya ujasiriamali hata kama hauna mtaji,kama unataka kufaulu masomo yako anza leo kujipanga kusoma sio usubiri mitihani,chochote ambacho unakitaka kwenye maisha yako anza kukiandaa mapema sana maana maandalizi yatakusaidia wewe kuhakikisha kuwa unafanikiwa sana kwenye vita yako ya maisha,ninachoamini mimi kila mtu ameumbwa kushinda na wewe ni mshindi pia.

Endelea kupambana hadi kieleweke.

Asante kwa kuendelea kuwa na mimi mpaka sasa.

PIUS JUSTUS MULIRIYE
0754745798
piusjustus28@gmail.com

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *