JIPE KAZI AJIRA HAKUNA

JIPE KAZI AJIRA HAKUNA
Kabla ya kuendelea sikiliza hii;-

KAMA ULIIKOSA VIDEO HII INAYOFUNDISHA JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MCHE AMBAYO NI MOJA YA BIDHAA ILIYOPO NDANI YA KITABU CHANGU CHA MILIKI KIWANDA MILIKI UCHUMI NIMEKUSOGEZEA HAPA UISIKILIZE UNAWEZA KUJIFUNZA KITU.


Habari ndugu msomaji wa makala zangu ni matumaini yangu kuwa uko salama hadi wakati huu tazama leo ni siku nyingine tena ambayo Mungu ametupa mimi na wewe ili tuweze kufanya kitu cha tofauti kwenye maisha haya,nikupongeze kwa kuchukuwa hatua kwa kusoma makala hii naamini kuna kitu kitaongezeka kwenye maisha yako.

Leo nataka nizungumzie swala la ajira,kutokana hali halisi ya nchi yetu ilipofikia leo swala la ajira imebakia kuwa kitendawili, hebu fikiria zamani ajira za uwalimu zilikuwa ni moja kwa moja yani ukisomea ualimu yani wewe ni ajira moja kwa moja lakini leo angalia imekuwa tofauti lazima uombe,kiuhalisia mambo yamebadilika sana kwenye swala zima la ajira,lakini siku zote kuna usemi unasema kila kwenye changamoto ndani yake kuna fursa.

sasa ni wakati wa kujipa kazi mwenyewe,ni wakati wa kujiajiri wewe mwenyewe hata kwa kuanza na ulicho nacho,haijalishi leo una nini,haijalishi unakutana na mazingira magumu kiasi gani lakini hebu angalia kitu gani wewe unakipenda ambacho unaweza kukitumia au kukifanya ili iwe kazi yako,iwe ajira yako basi ukikipata hicho anza kukifanya.

kuna dada mmoja yeye alikuwa ni mwalimu lakini bado hajapata ajira alichoamua kukifanya ni kuanza kukusanya watoto mitaani na kuwafundisha bure,baada ya muda kwasababu alikuwa akitoa huduma bora wazazi walianza kwa kumchangia na baadae akaweza kufungua shule ya watoto,leo naongea na wewe anashule kubwa sana ya watoto tena sio moja zaidi ya moja.Hata wewe unaweza rafiki chamsingi kaa chini jiangalie ndani yako kuna nini? Kitu gani unakipenda zaidi,kitu gani unaona kwako ni rahisi sana kukifanya basi anza na hicho hata kwa mtaji mdogo,hata kwa kuanzia ndani mwisho wa siku utafanikiwa tu.

RAFIKI JIPE KAZI WEWE MWENYEWE UKISUBIRIA AJIRA UTACHELEWA SANA

Jipatie kitabu hiki kitakachokufundisha namna ya kutengeneza bidhaa mbalimbaki zinazohitajika katika jamii kila siku kama Sabuni ya mche, sabuni ya maji, shampoo, mafuta ya mgando, chaki, tomato na chill source n.k kwa kufanya hili utaweza kumiliki kiwanda chako nyumbani kwako na kutengeneza kipato bila kikomo.

Bonyeza picha hii kudownload kitabu hicho;

 


Pia unaweza kudownload kitabu hiki bure kabisa ili kujiongezea maarifa, ni kitabu kizuri kilichobadilisha maisha ya watu wengi ikiwemo mimi pia.
Bonyeza picha hii kudownload;

Pius Justus Muliriye
0754745798
piusjustus28@gmail.com

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *