DAKIKA 2 (2 minutes principle)

“Dakika 2 Zinatosha Kuanza”

Kuna kitu kinaitwa Procrastination.  Hii inatamkwa _prokrastineishen











Kwa ambao hamfahamu neno hili, hii ni hali ya kuahirisha mambo. Kila siku unatamani kuanza kufanya kitu fulani lakini unajikuta tu umeahirisha.

Unatamani kuanza biashara, unaahirisha
Unatamani kuomba kazi, unaahirisha
Unatamani kuandika kitabu, unaahirisha
Unatamani kumuambia unataka awe mkeo, unaahirisha
Unatamani tuuu unatamaniii, unaahirisha

Kuna wakati unaweza kuahirisha kufanya jambo moja leo ili ulifanye wakati mwingine, kwa nia njema tu ya kuja kulifanya vizuri zaidi ambapo unaweza kuwa na ujuzi zaidi au ukawa na rasilimali za kutosha. Hata hivyo, lile linaloleta shida ni kuahirisha wakati unajua kabisaa ukilifanya wakati huo litakupa matokeo chanya kabisa.

Tabia hii ya kuahirisha mambo ni tabia mbaya na isiyovumilika. Wakati unajua kabisa ukifanya na kutenda wakati huu basi matokeo yatakuongezea faida, yatakupa hadhi zaidi, yatakuboresha wewe na kukuongeza lakini bado unayaahirisha. Hii sio njema.

Mattin Luther King Jr aliwahi kusema _”if you can not run, walk, if you can not walk crawl, just make sure you do something to move..”_ yaani, kama huwezi kukimbia basi tembea, kama huwezi kutembea basi tambaa, hakikisha unafanya kitu ili kusonga mbele. Usiahirishe.

Siku moja nilikua namsikiliza  Joel Nanauka katika kipindi nikipendacho cha Temino cha Harris Kapiga na Lilian Mwasha hapo Clouds FM. Joel alikua akimalizia somo lake juu ya _procrastination_. Kwa bahati nzuri kabisa akatoa mbinu ya kukabiliana na janga hili. Mbinu hii anaiita *2 minutes principle* . Hii ni pale ambapo una angalau dakika mbili tu za kufanya jambo fulani, anzaaa.

Ushawahi kujiambia _”ngoja niingie katika instagrama kwa dakika mbili tu..”_ halafu ukajikuta umekaa uko masaa mawili.

Ushawahi kujiambia _”ngoja nijinyooshe hapa kwenye kochi kwa dakika mbili tu..”_ ukajikuta umelala hapo masaa mawili. Naamini una mifano mingi zaidi. Kumbe, tatizo huwa ni muda wa kuanza tu.

Sasa basi, Joel Nanauka, anatupa mbinu rahisi tu ya *kuanza*, anasema *Dakika 2 zinakutosha kabisa kuanza*. Yaani unapojikuta una dakika 2 tu basi anzaa. Huko utajikuta unamaliza masaa mawili na bado utataka kuendelea.

Usiseme hauna muda wa kuandika kitabu, chukua dakika mbili na uanze kuandika. Usiseme hauna muda wa kufanya mazoezi, chukua dakika 2 na uanze.

Usiseme hauna muda wa kusoma kitabu au notes zako ili ufaulu, chukua dakika 2 na uanze.
Usiseme hauna muda wa kandika juu ya biashara yako, chukua dakika mbili na anza.

Yaani Dakika 2 ulizo nazo zinatosha kuanza kufanya jambo lolote lile. Ukiisha anza, yaliobaki, yatakuja _automatically_ rafiki yangu.

Ngoja niishie hapa, nimeanza na dakika zangu mbili na nimejikuta nimemaliza hii _kurasa ya Dakika mbili. Sasa nahamia kwenye kitabu. Dakika mbili nyingine naamini nitaandika page 10 leo.

Unaweza pia nikutakie dakika mbili bora kabisa rafiki yangu !!

Chukua dakika mbili tu kubonyeza link hii ZIJUE BIASHARA ZINAZOWEZA KUKULETEA TIJA KATIKA MAISHA YAKO MWAKA HUU 2017.

Asante kwa kuendelea kuwa na mimi.

Pius Justus Muliriye
Mwalimu, Mwandishi na mjasiriamali
0754745798
0657128567
piusjustus28@gmail.com

1 thought on “DAKIKA 2 (2 minutes principle)”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *