ZIJUE MBINU ZA JINSI YA KUFANYA BIASHARA MTANDAONI.

Angalia picha hii vizuri na ujifunze kitu…

Najua kuna watu wengi wanatamani kufanya biashara mtandaoni kama hapa facebook na watengeneze pesa, na nimeona watu wengi wakipost picha za bidhaa zao kwenye wall zao. Lakini je…umeshawahi kupata wateja kama ulivyotaka? Au watu wameishia kulike picha za bidhaa zako tu na kuondoka?

Umeshawahi kujiuliza kwanini bidhaa yako watu hawaichangamkii? Tatizo si kwamba bidhaa yako ni mbaya, tatizo hauko serious na biashara yako.

Mwanzoni nilifanya hivyo nilivyomaliza kuandika kitabu changu na nikapost kwenye wall yangu ya facebook lakini watu waliishia kulike na kunipongeza na hakuna aliyenunua kabisa kwa zaidi ya mwezi mzima mpaka nikaona nimepoteza nguvu zangu bure.

Niliamua kufanya utafiti wa jinsi gani ya kuwafanya watu waipende bidhaa yangu na hatimaye wawe wateja wangu.

Niligundua kitu muhimu sana katika hatua za kufanya biashara mtandaoni.
“Watu hawana shida na bidhaa yako, watu wanataka kujua bidhaa yako itawasaidiaje”

Hiyo ndiyo siri kubwa sana katika kufanya biashara mtandaoni.

Kitu kingine ambacho watu wengi hawapendi kukifanya ni kuogopa gharama!!! Watu hawapendi kulipia matangazo yao mtandaoni aidha kwa kujua au kwa kutokujua..

Ukiangalia picha hiyo utagundua kuwa nililipa gharama flani ili kuwafikia wateja niliokuwa nahitaji…..na niliuza kitabu changu kuzidi gharama niliyoitumia kulipia tangazo hilo.

Hiyo ni page yangu ya biashara ya facebook inayoitwa THINK BIG START SMALL, ina viewers 3000 lakini baada ya kulipia tangazo moja la kitabu changu nikapata watu 8,111 na kati ya hao walinunua bidhaa hiyo na hapo ndipo nilipogundua kuwa kuna wateja wengi tunashindwa kuwagikia kwa kukosa maarifa na kuogopa gharama.

Jiulize uko tayari kulipa gharama ili uuze? Au hauko tayari na uendelee kukaa na bidhaa yako?

Nakuhakishia kama unauza nguo, unaweza ukauza mpaka mikoani bila shida yoyote, kama unauza handbags, wallets, n.k unaweza ukauza mpaka ukashangaa!!! Cha msingi ni kutengeneza idadi ya watu wengi kadri uwezavyo kwenye page yako ya facebook(soko lako) …na hii ni lazima ugharamie!!

Kama unahitaji kuwa mfanyabiashara mtandaoni unatakiwa uwe na vitu vifuatavyo;

1. Facebook page(hii ni tofauti na hiyo akaunti yako unayopost picha zako ukiwa na mpenzi wako au ukiwa beach unaogelea)

2. Blog (hii utaitumia kuelezea bidhaa zako ulizonazo, na ndipo utaweka picha nyingi za bidhaa zako, huko ndiko utaelezea faida na ubora wa bidhaa zako na pia utai link na facebook page yako).

3. Lazima uwe na acount ya EQUIT BANK au benk yoyote yenye uwezo wa kulipia huduma online (hii itatumika kulipia matangazo yako).

Baada ya hapo wewe tayari ni mfanyabiashara mtandaoni.

Kama huna ujuzi huo na unahitaji kufahamu au unatamani kufanya biashara mtandaoni basi usisite kuwasiliana nami nitakusaidia kutimiza ndoto yako.

Tunatoa huduma zifuatazo katika kukusaidia:

1. Tutakutengenezea FACEBOOK PAGE na kukukabidhi ikiwa na followers zaidi ya watu 10,000 (elfu kumi).

2. Tutakutengenezea BLOG ambayo ina muonekano mzuri na tutakufundisha jinsi ya kuitumia.

3. Tutakusaidia ku link blog yako na mitandao ya kijamii.

Kama uko tayari kujitoa kwa ajili hiyo tuwasiliane Whatsapp 0754745798 na uwe mfanyabiashara mtandaoni uone tofauti!!!!

KUWA TOFAUTI NA WENGINE!!!

KARIBU SANA.

PIUS JUSTUS MULIRIYE
0754745798
piusjustus28@gmail.com
www.shuletanzania.info

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *