NI JUKUMU LA MZAZI KUGUNDUA NA KUENDELEZA KIPAJI CHA MTOTO.

NI JUKUMU LA MZAZI KUGUNDUA NA KUENDELEZA KIPAJI CHA MTOTO.

Habari rafiki;
Kama wewe ni mzazi au ni mzazi mtarajiwa basi ujue ni jukumu lako kugundua na kukiendeleza kipaji cha mwanano.

Nakumbuka wakati baba yangu ananitayarisha kwenda kuanza form one St. Alfred kule ngara mwaka 2001,  katika vitu alivyoninunulia ilikuwemo radio, lakini cha kushangaza alininunulia na set nzima ya vifaa vya kufungulia radio….kiukweli sikuelewa, kutokana na tabia yangu ya ukimya hasa pale napokuwa mbele ya wakubwa sikuweza hata kuuliza vitu vile vilikuwa ni vya nini na wakati mimi naenda shule kusoma.

Nilikuja kugundua nini maana yake baada ya kuingia form five mwaka 2005 kuwa alininunulia vile vitu ili hata radio ikileta tatizo basi niweze kufungua mwenyewe na nijaribu kurekebisha.

Alitamani sana kijana wake nijifunze kufanya vitu mwenyewe bila kutegemea fundi au mtu mwingine, kwa kuwa nilikuwa mwoga sana sikuweza kufanya hivo, na sasa labda ningekuwa fundi mzuri sana wa radio na hata tv.

Nimekupa story hiyo ili ufahamanu ni jinsi gani mzazi ana jukumu la kufanya kila juhudi ili kugundua kipaji cha mtoto wake.

Huyo mtoto kwenye picha ni miongoni mwa watoto wenye ndoto za kuwa kama baba zao, mtoto anapenda kumfata baba yake sehemu zake za kazi na kujifunza akiwa bado mdogo sana; na hivyo ndivyo wenzetu nchi zilizoendelea wanafanya.

Ukiona hivyo usimpige mtoto wala kumfukuza asikufwate kazini kwako, inawezekana kabisa akawa anapenda kuwa kama wewe.

Mafaniko ya mwanao yako mikononi mwako, chukua hatua kutimiza ndoto ya mwanao.

Hongera sana mzee Yustus Muliriye kuendelea kumfundisha kijana huyo kazi hizo, naamini atakuwa fundi mzuri sana siku za mbeleni.

Pius Justus Muliriye
0754745798-whatsapp
piusjustus28@gmail.com
www.shuletanzania.info

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *