Habari rafiki yangu mpendwa sana na mfuatiliaji wangu wa makala zangu hizi za kila siku kupitia blog hii ya ShuleTanzania.
Natumai uko na afya njema kabisa na unaendelea na majukumu yako ya kila siku.
Kama ambavyo nimekuwa nikikuandikia makala mbalimbali za kukuhamasisha ili uchukue hatua katika maisha yako basi leo napenda nikushirikishe kitu kimoja muhimu sana ambacho kama kijana unatakiwa ukifate na uchukue hatua mara moja kwani kitakusababishia kusogea mbele kimaisha.
Hizi ni aina chache kati ya nyingi ambazo zinaweza kukunufaisha kwa haraka sana hasa pale utakapoamua kuchukua hatua mara moja na kufanyia kazi. Najua watu wengi huwa wanasingizia mitaji, nataka nikwambie wewe kijana mwenzangu, tatizo huwa sio mtaji, tatizo ni wewe na woga wako. Kuna usemi unasema “Woga wako ndio umaskini wako” ukiendelea kuogopa utakuja kushtuka umri umeenda na utashindwa kuchukua maamuzi na kubaki kulaumu tu. Anza hata kama una kidogo, Mungu atakubariki.
Aina hizi za biashara ambazo nitakwenda kukushirikisha hapa nimeshawahi kuwashirikisha katika semina niliyoitoa mtandaoni mwishoni mwa mwaka jana, waliofatilia mpaka sasa wako mbali na wanafanya vizuri sana katika biashara hizo.
Baada ya hapo wengi walivutiwa sana na mafunzo hayo wakatamani nirudie lakini ratiba yangu ikawa hainiruhusu kufanya hivyo kwani kuna mambo mengi ya kufanya, lakini kwa kuona umuhimu huo nikaamua kuwawekea mafunzo yote katika kitabu kimoja, na kila anayehitaji alikipata. Kama utakihitaji basi usisite kuwasiliana nami kwa whatsapp 075474579 au bonyeza maandishi haya.
Basi nikupeleke moja kwa moja katika mada yetu ya leo; Hizi ni aina ya biashara zinazoweza kukuletea faida kubwa kama utazingatia na kuweka juhudi binafsi;
- UTENGENEZAJI NA UUZAJI WA SABUNI ZA MCHE.
Hii ni aina moja ya biashara ambazo unaweza ukafanya na zikakuletea faida kubwa sana.
Utengenezaji wa sabuni ni rahisi sana kama una nia ya kufanya biashara hii.
Sabuni ni bidhaa ambayo inatumika kila siku na watu wote, hata wewe hapo ulipo unatumia sabuni na utaendelea kutumia kila siku. Bidhaa hii ina wateja wengi sana na una uhakika wa kufanya biashara kila siku bila kikomo.
Sabuni ya magadi ya mche ni sabuni inayopendwa sana na watu, inatengenezwa kwa njia rahisi sana, ukiifanya biashara hii naamini itakutoa sana.
- UTENGENEZAJI NA UUZAJI WA SABUNI ZA MAJI
Hii ni moja ya bidhaa pia inayopendwa na watu wengi hasa kwa kazi ya kufulia au hata kuoshea magari na hata vyombo.
Kuna aina nyingi sana za sabuni za maji mojawapo ni ile ya kuoshea magari, kuoshea vioo vya nyumba na magari, kufulia na zile za kuoshea vyombo.
Ukijifunza kutengeneza bidhaa hii hutakosa soko la kuuza kwani hata mtaani kwako unaweza kuuza na kutengneza faida kubwa kuliko hata yule aliyeajiriwa.
Utengenezaji wa sabuni hii ni rahisi sana pia, malighafi kubwa sana hapa ni maji na materials mengine kidogo yatakayogeuza maji hayo kuwa sabuni.
- UTENGENEZAJI NA UUZAJI WA DISFECTANT (DAWA ZA KUSAFISHIA VYOONI NA SINK)
Kulingana na hali ya sasa ilivyobadilika na mtindo mzima wa maisha ya binadamu kustaarabika zaidi, watu wameanza kuwa na vyoo vya ndani ya vyumba maarufu kama MASTER ROOMS ambapo kuna masink ambayo yanasafishwa na sabuni hii special. Sabuni hii haitoki mbinguni, inatengenezwa kwa technolojia kidogo sana na ya kawaida ambayo kila mtu anaweza kutengeneza nyumbani kwake na ukateweza kuuza na kutengeneza faida. Nakushauri changamkia fursa hii na utengeneze kipato kikubwa.
- UTENGENEZAJI NA UUZAJI WA SABUNI YA UNGA.
Rafiki, nfahamu kabisa umeshawahi kutumia sabuni za unga kufulia nguo zako. Sabuni hii si inatengenezwa na viwanda vikubwa sana, la hasha! hata wewe unaweza kutengeneza nyumbani kwako. Najua utakataa, lakini huo ndio ukweli…
Utengenezaji wa aina hii ya sabuni hauhitaji utaalamu mkubwa sana, bali tu unahitaji utayari wako, kisha utahitaji materials ambayo yanapatikana pia. Changamkia fursa hii ambayo ina wateja kila siku, una uhakika wa kuuza kila siku kwa rejareja au hata kwa jumla katika maduka mbalimbali na ukatengeneza kipato kikubwa zaidi.
- UTENGENEZAJI NA UUZAJI WA CHAKI.
Hii pia ni biashara nyingine ambayo inaweza ikakutajirisha sana kuliko kawaida kwani ni bidhaa ambayo inatumika kila siku mashuleni na hata vyuoni.
Chaki ni bidhaa ambayo inatengenezwa kwa technolojia rahisi sana, na malighafi zake ni za kawaida ambazo zinapatikana kwa wingi madukani, naamini hapo ulipo kuna maduka ya hardware, na materials haya yanapatikana.
Unaweza kutengeneza hadi milioni 9 kwa mwezi kama utakuwa serious na kazi hii. Changamkia fursa hii, unachelewesha maendeleo yako.
Hizi ni baadhi tu ya bidhaa ambazo unaweza kutengeneza na kuuza na kutengeneza faida kubwa kwani mzalishaji ni wewe na muuzaji ni wewe pia. Tengeneza kiwanda kidogo nyumbani kwako na anza biashara kwa mtaji kidogo sana.
bidhaa zingine ni kama
- MISHUMAA
- MAFUTA YA MGANDO
- JAM (FRUIT)
- TAMBI (ZA DENGU)
- UNGA WA LISHE
- CLIPS
- TOMATO SOURCE
- N.K
Hakika nakuhakikishia huwezi kukosa hata biashara mojawapo hapo ya kufanya mwaka huu wa 2017. Jitume zaidi na utafanikiwa.
Najua utakuwa unajiuliza utawezaje kutengeneza bidhaa moja wapo kati ya hizo?
Usijali! Nimekuandalia kitabu kizuri sana chenye maelekezo mazuri sana, kitakufundisha HATUA KWA HATUA utengenezaji wa bidhaa zote hizo.
Kitabu hiki kitakuelekeza materials zinazofaa kutengeneza bidhaa hizo unazoziona hapo na zinapopatikana kiurahisi kabisa.
Kitabu hiki kina kichwa cha habari kinaitwa “MILIKI KIWANDA MILIKI UCHUMI”
Kitabu hiki kilichoandaliwa kwa ustadi mkubwa sana kinapatikana kwa bei ndogo sana ya Tsh. 5000/- lakini natoa ofa kwa wewe unayesoma makala hii, watu 20 wa kwanza watapata nakala zao kwenye simu zao kupitia whatsapp au email zao kwa Sh. 3500/- tu badala ya Tsh. 5000/-. na baada ya hapa kitaendelea kuuzwa kwa Sh. 5000/-
NB: Kitabu hiki kipo kwenye mfumo wa PDF ambao utaweza kuusoma kwenye simu yako ya mkononi kwa njia ya Whatsapp au Email yako. Jifunze kupitia simu yako uone faida ya simu yako.
Lipia nakala yako kwa namba; MPESA- 0754745798 – PIUS MULIRIYE
TIGO PESA – 0657128567 – PIUS MULIRIYE Kisha wasiliana nami kwa Whatsapp 0754745798 nami ntakutumia.
Asante kwa kuendele kusoma makala zangu. Endelea kutembelea ukurasa huu kila siku upate maarifa mbalimbali.
Pius Justus Muliriye
Mwalimu, Mwandishi na mjasiriamali
0754745798
0657128567
piusjustus28@gmail.com