Kubali kupoteza kwa ajili ya kile ukipendacho.
Habari rafiki yangu na msomaji wangu, natumaini hujambo kabisa na unaendelea na harakati za kuboresha maisha yako.
Karibu tena leo katika makala ya siku ya leo.
Katika maisha kuna vitu unatokea kuvipenda sana na unatamani kuwa navyo ili uwe na furaha katika maisha yako. Je uko tayari kupoteza nini ili upate kile unachokipenda?
Unaweza ukampenda msichana flani na ukahitaji kuwa naye kama mke wako, je uko tayari kupoteza kile ulichonacho ili umpate yule msichana unayemhitaji?
Je, uko tayari kuacha pombe ili uwe na yule mwanamke unayemtaka ambaye hapendi mwanaume mlevi?
Je wewe ni mwanamke ambaye huwezi kuacha ofa za wanaume na kuzurula kila bar? Je uko tayari kuacha ili umpate yule mwanaume ambaye unamhitaji na hapendi tabia zako?
Vivyo hivyo katika biashara, upo tayari kuacha usingizi ili usimamie biashara yako usiku na mchana?
Uko tayari kuwaacha rafiki zako unaowapenda ili utimize malengo yako?
Hiyo ndiyo siri kubwa katika maisha. Inabidi uwe tayari kupoteza kile ulichonacho ili upate unachokipenda!
Asante kuwa nami mpaka hapa. Tukutane katika makala ijayo.
Wasiliana nami kwa ushauri katika biashara au kitu chochote katika maisha;
Pius J. Muliriye
0754745798
0657128567
piusjustus28@gmail.com
0754745798
0657128567
piusjustus28@gmail.com