MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA ILI UWEZE KUFIKA MAHALI UNATAKA KUFIKA 2017

Baada ya kuona namna ambavyo maamuzi na kujisikiliza vinavyoweza kutupeleka hatua nyingine ya maisha, leo nitakueleza mambo ya kufanya baada ya kufanya maamuzi sahihi na kujisikiliza mwenyewe ili utoke sehemu ulipo .Mambo yafuatayo ni muhimu sana kuyazingatia ili uweze kufika mahali unataka kufika 2017.


1. Achana kabisa na hofu ya kitu usichokijua ( Abandon with fears of unkwnown)

Wanadamu wengi wamejawa na hofu lakini hofu yao ni ya vitu wasivyovifahamu .Nakumbuka jinsi ambavyo kabla ya kuingia kwenye mtihani kipindi nasoma  watu walikuwa wanaanza kutetemeka hata kabla hawajaona mitihani .Siwezi kumsahau rafiki yangu mmoja aliwahi hata kujikojelea kwa kuogapa mtihani ambao hata maswali yake alikuwa hajayaona  pamoja na kuwa alikuwa na uwezo mkubwa darasani .

Watu wengi wanapenda kufanya mambo (kudhubutu ) lakini ukweli ni kwamba bado wana hofu ya kushindwa,wana hofu ya kuchekwa lakini mimi  huwa nasema kuwa  kitu pekee tunachopaswa kuogopa 2017 wakati tunapoutangaza kuwa ni mwaka wa KUINUKA ni hofu peke yake na si kingine .Anza leo kuogopa hofu .

Jana nilikupa mfano wa mwana mpotevu aliyekuwa ameomba sehemu ya urithi kutoka kwa babaye na akaenda mbali na huko alikokwenda akawa ameishiwa pesa na baadae akaamua arudi kwa baba yake bila hata kuogopa kama baba yake angemchukuliaje .Kwangu namuona ndugu huyu kama mtu asiyeogopa hata kidogo na anachokiamua huwa anakisimamia.

2. Jiamini mwenyewe ( Believe in yourself)

 Ni lazima ili ufike kule unakofikiri ufika 2017 ujiamini mwenyewe kabla hujaaminiwa maana watu hawamwamini mtu asiyejiamini .Amini uwezo wa kipekee wa kufanya vitu ambao Mungu alikupa na usiofanana na mwingine .Amini ubunifu ulionao ambao hata haufanani na mwingine .Amini kile ulichonacho ambacho kiko tofauti na mwingine haijalishi watu wanakionaje.

Acha kuamini kama wengine wamependelewa na kuwa huwezi kufanya mambo makubwa kama wao huko ni kujidharau kunakotakana na kutojiamini .Kama hujiamini utaanza kunakili maisha ya watu na kufanya vitu usivyovipenda ili kuwafurahisha wengine wasiojua unakokwenda

3.Jenga uwezo wako wa ndani ( Build your inner ability )

 Ni lazima uanze kujijenga kwa ndani ili ufike kule unakotaka kufika vinginevyo hautafika .Uwezo wa ndani unajengwa kwa kutafuta maarifa na taarifa abazo ndizo zitakuza sana uwezo wako binafsi wa kufanya  mambo .Maarifa haya na taarifa hupatikana kwa njia ya kusoma vitabu mara kwa mara .Kusikiliza vitu vyenye tija vinavyokupeleka kule unakotaka kwenda  na kuhudhuria semina na mafundisho mbalimbali

Bila kujenga uwezo wako wa ndani hautafika kokote maana utakosa nguvu ya kukupeleka kule unapotaka kufika. 

“imeandaliwa na JYB”
wasiliana nasi kwa ushauri au maoni kupitia;
Pius Muliriye Justus
0754745798
0657128567
piusjustus28@gmail.com

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *