Unaweza pata ujuzi kwa kuhudhuria semina mbalimbali,workshop mbalimbali,au kufundishwa na mtu wenye ujuzi husika na baada ya kupata ujuzi kuanza fanyia kazi katika maisha yako ya kawaida kila siku na kuwa bora kwa upande huo.
Nimejaribu kuorodhesha aina zaidi ya 14 unaweza anzisha pasipo kuwa na mtaji kabisa au mtaji kidogo sana.Hizi ni aina ya biashara ambazo nimezifanya kwa muda sasa na kuona matunda yake na nyingine nimeshuhudia watu wakifanya na kufanikiwa.
Kama kweli una shauku la kweli kuanza leo biashara soma kwa umakini sana na kuona je ni wapi pa kuanzia ili uweze timiza lengo lako la maisha
Zifuatazo ni baadhi ya biashara unazoweza anzisha kwa mtaji mdogo sana au pasipo mtaji kabisa:
i. Huduma za kuandika miradi biashara(business plan),kama ilivyo kwa tafiti za uchanganuzi yakinifu(hali halisi ya biashara)wajasiriamali wengi huwa huepuka kufanya kazi hii ngumu ya kuandika mradi biashara(business plan) yao.Ukweli ni kuwa wajasiriamali wengi hawajui hata kuandika business plan katika uwezo wa kuwashawishi wawekezaji kuja kuwekeza na huwa hawawekezi muda wa kutosha kujifunza kwa hilo.Kama unaweza timiza hitaji hili biashara ipo mikononi kwako.
ii. Mshauri wa mambo ya biashara:Wewe ni unauzoefu wa ujasiriamali au mmliki wa biashara?Unajua nini kinahitajika ili uanzishe biashara,kujenga biashara,kuingoza biashara na kukua?Sasa unaweza kuanza kazi ya ushauri wa biashara.Unaweza saidia kampuni au biashara mbalimbali kutoka chini ya uvungu na kwa kutoa ushauri na maelekezo muhimu.Unaweza kuwasaidi watu walioajiriwa kuanza kutoka kwenye ajira na kuingia kwa ujasiriamali kwa malipo.
iii. Huduma za kuandaa vitabu vya mahesabu.Wewe ni mzuri katika kuandaa vitabu vya uhasibu vya kampuni au biashara mbalimbali?unaweza weka ulingano kwa vitabu kwa vya uhasibu(hili ni jambo huwa na shauku kulipata)? Sasa hamna kitu kinaweza kukuzuia wewe kuanza huduma za kuandaa vitabu vya mahesabu anza sasa.
iv. Kutoa huduma ya kuandaa nakuendesha matukio(Event management),kampuni nyingi kila mara huwa na matukio mbalimbali mfano semina,siku ya familia,sherehe mbalimbali mara nyingi kampuni kama kampuni haiwezi kufanikisha kwa ufanisi uandaaji wa matukio haya,na hivi ndivyo ilivyo kutokana na wafanyakazi wao kuwa na majukumu husika tofauti na kuandaa matukio ya kampuni na kuyasimamia,hivyo ili kuwa na ufanisi hapa inabidi kampuni zikodi watu wan je wenye ujuzi wa kuandaa shughuli husika kwa uhakika,wewe kama una ujuzi na uzoefu wa kuandaa shughuli kama hizo mwanzo mpaka mwisho uwanja ni wako.Mfano kuna matukio kama siku ya familia,semina kwa wafanyakazi,maonyesho ya biashara ndani nan je ya nchi kwa kampuni husika nk
v. Kuanzisha tovuti kwa huduma mbalimbali,Kwa afrika watu kunufaika na tovuti ndio kwanza ipo steji za mwanzoni,Unaweza anzisha tovuti na kutoa huduma ya taarifa watu wanatafuta ,baada kuwa mmiminiko wa watu wengi wanaotembelea tovuti yako,unaweza sasa ongea na kampuni kadhaa kuja kutangaza na wewe na kutengeneza fedha za kutosha.Kama hujui jinsi ya kutengeneza tovuti usijali kuna tovuti za bure kabisa ambazo zimetengenezwa tayari kinachohitajika ni wewe kujaza fomu zao na ndani ya dakika moja unakuwa na wewe tovuti yako,na kama unahitaji nunua domain unaweza ikawa moja kwa moja tovuti yako.Tovuti unazoweza ingia na kutengeneza tovuti yako bure ni www.weebly.com,www.webs.com nk au pia unaweza tengeneza blog ikawa ni unaweka taarifa watu wanatafuta na kisha kutafut wadhamini wa hiyo blog.
vi. Mshauri wa masoko,Je wewe unaweza nionyesha mimi njia ya gharama ndogo ya kuongeza wateja wangu kuanzia aslimia 30% -70% au zaidi?kama ndio biashara ipo mikononi mwako.Unaweza jiweka wewe mwenyewe katika ushauri wa masoko kwa wamiliki biashara ndogo na kati hata kubwa jinsi ya kuteka na kuwavuta wateja na kuongeza mauzo ya bidhaa kwa ada Fulani ,kutokana huduma husika.
vii. Mtafasiri wa maandiko mbalimbali kwenda lugha ya wazawa;Kampuni nyingi za nje zinazokuja hapa nchini,huwa wanahitaji kutafsiri taarifa zao kwenda lugha ya wazawa,mfano mradi Fulani,tovuti zao,mfano kama ni kampuni ya vitabu mwandishi mmiliki angependa ili auze kwa wazawa inabidi atafasiri kwenda lugha ya wazawa,Pia mfano kuna hata miradi mbalimbali ambayo inatakiwaiangaliwe na wazawa nk.
viii. Kutafiti fursa mpya za biashara,Nina marafiki wangu ambao walianza kutoa huduma ya kutafi fursa mpya na wanafanya vema kwenye hii biashara.Wanachofanya kutupia jicho kwa mambo yajayo,mwelekeo,mahitaji aua fursa za biashara;na kuandaa mradi/mpango kuhusiana hilo na kuuza hilo wazo kwa makampuni makubwa.Wakati mwingine wanakuja na mawazo ya bidhaa na mawazo ya biashara yenye soko moja kwa moja kubwa la kutosha;na kuuza hayo mawazo kwa makampuni kwa ajili ya kuayaendeleza.Kama kazi hii unaipenda unaweza anza kutoa hudumu kutafiti fursa mpya za biashara
ix. Kutoa huduma za ku-print,Biashara hii inafahamika sana na wengilakini bado inalipa sana.Unaweza kuanza kutoa huduma ya ku-print business,banner sposters card,viperushi,flyers,catalogues kwa biashara ndogo na za kati.
x. Kutoa huduma za kuajiri,Siku hizi kazi za managementi za rasilimali watu kwa kampuni nyingi hutolewa na tenda kwa kampuni za nje ya kampuni husika kufanya hiyo kazi ili kuongeza ufanisi kwa kampuni husika na hivyo kupelekea kampuni husika kuweka umakini wake wa kutimiza lengo lake mahususi.Kama una uelewa na ujuzi wa kutosha wa kushughulika na maswala ya rasiliamali watu uwanja ni wako,kwa sasa hapa Tanzania kujisajili kuwa wakala wa kuajiri ni bure unatakiwa uende pale wizara ya ajira na vijana kujisajili.
xi. Mshauri wa mitandao ya kijamii (social media consultancy),Kwa hii dunia mitandao ya kijamii imechukua asilimia kubwa sana.Je wewe unajua jinsi ya kutengeneza foleni kwa mitandao ya kijamii?Unajua jinsi ya kuboresha na kuelimisha umma juu ya chapa(brand) za makampuni ndani ya mitandao ya kijamii kama facebook,twitter na linkedin?Basi unaweza kuwa mashauri wa mitandao ya kijamii na kutengeneza fedha zako.
xii. Kutoa huduma za kuandikisha majina ya kampuni,Je wewe ni mzuri katika kuandika katiba za kampuni?unajua jinsi ya kuchagua jina sahihi la kampuni?unajua stepu zinazohitajika ili ukamilishe uandikishe jina la biashara?Anza sasa fungua biashara yako ya kutoa huduma za kuandikisha majina ya kampuni .
Huduma nyingine unaweza fanya ili kutengeneza fedha:
xiii. Kutoa huduma za kuandikisha hakimili za bidhaa au huduma yako
xiv. Huduma za ushauri kwa biashara ndogo
xv. Kuandika kitabu kizuri na kukiuza kwa umma.
Imeandikwa na :Deogratius kilawe