Natumaini unaendelea vizuri na harakati za kuboresha maisha yako, naamini uko katika njia sahihi kabisa ya kufikia ndoto zako.
Leo napenda kukushirikisha kitu hiki muhimu sana katika maisha yako. Kitu hicho ni FURSA.
FURSA maana yake nini?
Ni kitu ambacho kimejificha na hakiwezi kuonekana kwa urahisi sana kama utatumia macho yako ya kawaida na ukaacha kutumia akili yako.
Fursa nzuri ni zile ambazo zinamfanya mtu kuwa na mikakati ya muda mrefu. Fursa ni kitu ambacho kinaleta mwanga katika ndoto za mtu alizokuwa nnazo na ambazo angetamani kuona zinatimia.
watu wengi wamekuwa wakikimbilia fursa ambazo ni rahisi na sio sahihi bila kuangalia muunganiko kati ya fursa na ndoto zao.
Kuna fursa ambazo zinaweza kukupotezea muda kwa kukupa matumaini ya muda mfupi. hii ni kwa sababu wengi wanakurupuka kwa matatizo ambayo wanayo na kutumia fursa ambazo sio sahihi.
Usifanye kitu ambacho ni rahisi ila fanya kitu ambacho ni sahihi, kitu rahisi kila mtu anaweza kufanya, lakini kitu sahihi kinatofautiana kutokana na utofauti wa ndoto walizonazo watu.
Thomas Edison; aliwahi kusema; “Opportunity is missed by most people because it is dressed in overall and looks like work”
akiwa na maana kwamba; “Watu wengi wanakosa kuziona fursa, kwa sababu fursa huja kwa ujumla na huonekana kama kazi”
Kila fursa inakuwa na muunganiko fulani na mtu ambaye anaifanya. ndio maana ni vizuri mtu kujua fursa ambayo unataka kuifanya kwa usahihi kabla ya kuanza kuifanya maana unaweza kufuata upepo na upepo ukakuangusha. tafuta maarifa ya hiyo fursa ili uielewe kiundani na hata utakapoamua kuifanya, fanya kiusahihi sio kulegalega. Ni bora kufanya kitu ambacho ni sahihi hata kama ni kigumu kuliko kufanya jambo rahisi ambalo kila mtu anafanya, kwa namna hiyo huwezi kufanikiwa.
SOMA – JIPATIE KITABU KITAKACHOKUFUNDISHA JINSI YA KUMILIKI KIWANDA KIDOGO NYUMBANI KWAKO NA KUTENGENEZA KIPATO BILA KIKOMO
Asante kwa kuendelea kuwa na mimi. tafadhari shea na wenzako kwa kubonyeza kitufe cha facebook au whatsapp kuwashirikisha wengine wapate somo hili.
Kwa ushauri wowote ule usisite kuwasiliana na mimi;
Pius Justus Muliriye
0754745798 – Whatsapp
065712856
piusjustus28@gmail.com