HII NDIO MAANA HALISI YA ELIMU ULIYOIPATA DARASANI.

Habari rafiki yangu,  naamini utakuwa poa sana na sikukuu ilienda vizuri kabisa.

Karibu tena katika muendelezo wa makala zetu za kila siku,  zinazotukumbusha na kutufundisha kuwa na mtizamo chanya katika maisha yetu.

Watu wengi wamekuwa wakijidanganya kuwa ni wasomi sana na hata kufikia hatua ya kuwadharau watu ambao kwa bahati mbaya hawakuweza kusoma.
Elimu uliyonayo ndugu yangu ni kitu ambacho wengi wanakitamani kuwa nacho,  lakini katika uhalisia elimu yako haina uhusiano na maisha yako.

Sisemi elimu ni mbaya, la hasha. Elimu ni nzuri,  tena sana,  na ninakushauri ukasome sana kama ukipata nafasi.
Nimeamua kulizungumzia hili kwa sababu watu wengi hawajui nini maana ya elimu waliyonayo.  Elimu haiwezi kukupa maisha ya ndoto yako kama hujui nini maana ya elimu.

Elimu maana yake ni falsafa ambayo unapewa wewe ili ikusaidie kuona kile kisichoonekana kirahisi.

Elimu ni jicho la tatu ambalo linatakiwa kuona zaidi ya yale macho yako mawili uliyopewa na mwenyezi Mungu.

Elimu ili iwe na manufaa kwako ni lazima ikupe maono ya kuona fursa zinazokuzunguka,  na hapo ndipo utaishi ndoto zako kuliko kujisifu mbele za watu kuwa umesoma sana.

Kuna mifano mingi sana ya watu waliosoma,  lakini ndio wa kwanza kulalamika kila siku,  hawana njia ya kutatua matatizo yanayowazunguka.
Utakuta mtu ana masters lakini hawezi hata kuitumia masters yake kuona fursa,  yupo tu kijiweni akijisifu tu na maisha yake kuwa palepale.  Nakwambia wewe kama uko hivo umepoteza pesa zako na mbaya zaidi umepoteza muda.

Suluhisho la hili ni wewe kujifungia ndani kwa muda na ufikirishe ubongo wako ni nini ufanye ili uonyeshe jamii kweli ulisoma na unaweza ukafanya makubwa.

Fursa zipo nyingi sana,  acha kukaa kijiweni kuzungumzia watu,  fanya kitu kulingana na elimu yako na uisaidie jamii yako hatimaye uache kumbukumbu duniani.

Mwisho nikutakie kila lakheri katika kubadilisha mtizamo wa elimu katika maisha yako.

Kwa ushauri kama umeshindwa kabisa ufanye nini na elimu yako,  nipigie,  nitakusaidia kukupa mawazo. Au kama unahitaji ushauri wowote ule ili ukunufaisha katika maisha yako nipigie pia.

Jipatie kitabu kitakachokufundisha hatua kwa hatua jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali kama sabuni za mche,  za unga,  za maji,  n.k,  Bonyeza hapa kukipata kitabu hicho

Mawasiliano yangu ni haya:

Pius Justus Muliriye
0754745798 – whatsapp
0657128567
piusjustus28@gmail.com 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *