ZIJUE NJIA ZA KUTAMBUA KIPAJI CHAKO.

Habari rafiki,  naamini unaendelea vizuri sana na harakati za kuboresha maisha yako.
Pia nikupe hongera kwa kumaliza sikukuu ya chrismass salama kabisa na pia kwa uwezo wa mwenyezi Mungu utamaliza na kuuanza mwaka mpya salama kabisa.  (HAPPY NEW YEAR) 

Leo napenda kuzungumzia kuhusu kipaji cha mtu katika kutimiza ndoto zake.

Kila mtu amezaliwa angalau na kipaji kimoja au zaidi,  lakini imekuwa ngumu sana kwa watu kutambua vipaji vyao na kuviishi.

Chukulia mfano wa Masanja Mkandamizaji,  amekuwa ni mtu mwenye mafanikio makubwa sana katika maisha yake kwa sababu ya kipaji chake cha uchekeshaji,  laiti asingegundua kipaji chake hicho basi leo usingekuwa unamfahamu kabisa,  sio huyo tu, waangalie watu kama Joti,  Brother K,  Mbwana Samatta na wengine wengi wanaopeperusha bendela ya nchi hii ni kwa sababu ya vipaji vyao.

Angalia picha hiyo hapo juu,  huyo ni mdogo wangu,  kanitumia picha hiyo kwa whatsapp akisema siku hizi yeye ni mpiga picha za video.  Imenichekesha sana lakini nimejifunza kitu na ndio maana nikapata wazo la kuandika makala hii.

Charles(jina lake halisi) amekuwa akifanya vitu vingi sana katika umri huo mdogo alio nao,  amekuwa akijaribu mambo mengi sana,  mpaka amediriki kuwa akimfata baba sehemu zote ambazo huwa anaenda kufanya kazi za ufundi,  na baadae anaanza kuigiza kufanya kama baba,  ninaamini hii itamfanya awe na ujuzi mwingi na hatimaye atagundua kipaji chake na mwisho atafanikiwa katika maisha yake kupitia vipaji alivyovigindua kipindi cha utoto wake.

Picha hiyo unayoiona hapo juu,  ni mdogo wangu pia anaenifata kuzaliwa,  anaitwa Frances Muliriye. Amekuwa mtu anayependa kujaribu kila kitu ambavyo imemfanya ajue mambo mengi ambayo siwezi kuyaorodhesha hapa,  ni mengi sana.  Alichonifurahisha zaidi ni kuweza kutengeneza bidhaa yake mwenyewe baada ya kuwaz sana kwanini watu wananunua vitu kutoka china na wakati anaweza kutengeneza? Hivi sasa navyokwambia yuko njiani anapeleka order ya dazani 1000 ya pochi za kike alizotengeneza tukishirikiana.

SOMO LA KUJIFUNZA. 

  • Si lazima wewe kwenda shule na kusoma sana ndio ufanikiwe,  unaweza kufanikiwa hata kama huna elimu,  jaribu kufanya vitu vingi ili ugundue nini kipaji chako.  Hiyo itakusaidia kufanikiwa katika maisha yako. 
  • Usimchape mtoto kama wewe ni mzazi anapoharibu kitu akijaribu kutengeneza,  muelekeze kwa upendo inawezekana hicho ndicho kipaji chake kitakachompa mafanikio siku za mbeleni.  Wazazi wamekuwa wakichangia kwa aslimia 100% kuharibu ndoto za watoto wao wakidhani wanawatakia mema watoto wao.  Wazazi wanadiriki kuwachagulia watoto wao cha kufanya kulingana na matakwa yao,  utakuta mzazi anamsiaitiza mtoto asome awe daktari ili apate heshima mtaani ana mtoto daktari,  kumbe mtoto anapenda kuwa DJ,  au fundi kompyuta. Mzazi anataka mtoto wake awe mwalimu ili apate sifa kuwa ana mtoto mwalimu kumbe mtoto anataka kuwa mtangazaji wa TV.  Mwache mtoto afanye kile moyo wake unahitaji na unamsukuma kufanya ilimradi kiwe halali utaona matunda yake baadae. 
Kama wewe ni miongoni mwa watu ambao wanasema hawana kipaji hata kimoja unajiongopea.  Inawezekana hujui ni njia gani uzitimie kutambua kipaji chako.  Nataka nikwambie tu kuwa wewe ni mtu tofauti sana nanjisni ulivyo. Wewe ni mtu ambaye unamiliki biashara kubwa ndani yako.  Nataka nikudokeze tu njia kadhaa za kuweza kutambua kipaji chako. 
  1. Kuwa mtu wa kujaribu vitu vingi kila mara,  hii itakufanya kujua ni kitu gani unakipenda na kukifanya kwa ufanisi mkubwa kuliko kingine. 
  2. Usikilize moyo wake.  Hapa ni pale ambapo unapata muhemuko wa kufanya jambo filani na ukilifanya unasikia ahueni,  hili litakufanya ufanye kitu kile kwa ufanisi kwa sababu unapenda sana kulifanya,  nakuhakikishia itakutoa kimaisha.  Kama wewe kwa bahati mbaya umesoma ukalazimika kuwa mwalimu,  jiulize nini hasa lilikuwa lengo lako? Ukishajua basi lifanyie kazi ili ufanye kile kitu moyo wako unapenda.  Kama ulitamani kuwa mwandishi wachache habari,  nenda kasome uonyeshe uwezo wako,  au ulitamani kuwa mcheza mpira,  nenda kacheze mpira muda wako wa ziada na fanya kwa moyo wako utafanikiwa na hatimaye kuushangaza ulimwengu. 
  3. Penda kuwaangalia watu wanaofanya kitu unachokipenda.  Hii itakufanya kujua wanafanyeje kitu kile,  igiza kufanya kama wao utajikuta unaweza na hatimaye kukiishi kitu hicho. Mfano mzuri ni mimi,  nilikuwa napenda sana kuwa mhamasishaji,  na kuzungumza na watu kuhusu ujasiri wa kuthubutu na kuwa mjasiliamali mwenye mafanikio,  nilitamani kumiliki blog na website ili niwe naandik makala kama wanavyofanya watu wengine, hii ilinivuta na nikaanza kuwafatilia watu wanafanya vitu hivyo na kujifinza kutoka kwao,  nimelipa gharama kuyajua yote hayo kwa sababu moyo wangu ulihitaji kufanya hilo,  na hatimaye niko hapa nikikuandikia makala mbalimbali za kukuhamasisha na umekuwa ukinufaika juu ya hili.  Nimeweza kuandika vitabu vitatu vya ujasiliamali na kuviuza online na watu wamekuwa wakifaidi katika hili. 
ACHA KUSUBIRI,  FANYIA KAZI KILE MOYO UNAHITAJI.  Omba ushauri ufanyeje ili utimize ndoto zako,  nipigie nikufundishe jinsi ya kugundua kipaji chako na hatimaye uishi ndotp zako.  Kuna watu wanadhani kunipigia simu nitawapotosha kwa sababu tu wananifahamu au kwa sababu nimesoma nao,  wanajua uwezo wangu,  unajidanganya.  Watu wanabadilika,  nimesoma sana,  ninajua vitu vingi ambavyo inawezekana wewe huvijui,  usiogope,  nipigie simu tuongee. 
Kwa sasa natoa ushauri na consultation bure kabisa,  itakuja siku ushauri kama huu itabidi unalilipe pesa nyingi.  Chukua hatua leo,  mwaka usiishe hujapata elimu hii.  Karibu. 
NIKUTAKIE HERI YA MWAKA MPYA WENYE MAFANIKIO TELE.  UWE MWAKA WA MABADILIKO KWAKO KATIKA KUBORESHA MAISHA YAKO. 
Kwa mawasiliano zaidi:-
Pius Justus Muliriye 
0754745798-whatsapp 
0657128567 
piusjustus28@gmail.com 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *