HIVI NDIVYO ELIMU YAKO INAVYOKURUDISHA NYUMA BILA WEWE KUJUA.

Habari rafiki yangu mpendwa na msomaji wangu wa ShuleTanzania,  natumai uko vizuri sana na unaendelea vizuri na harakati za maisha yako. 

Leo ningependa nizungumzie suala la elimu na jinsi inavyokudidimiza kiuchumi na kifikra. 
Sisemi elimu ni mbaya,  ni nzuri sana na ninakushauri usome sana uwezavyo. 
Elimu,  hasa elimu yetu hapa Tanzania imekuwa ni kitu ambacho kimekuwa na mchango mkubwa sana katika kuwamaliza watu na kubaki kwenye umaskini mkubwa sana. 
Mimi mwenyewe nimesoma,  na nina degree yangu,  lakini elimu yangu imenifanya niwe tajiri,  ninayetegemewa na wengi,  sina pesa za kutisha lakini akili yangu imejaa mawazo chanya ambayo nimeamua kuyatoa kwa watu. 
Watanzania wengi wamesoma sana lakini degree zao hazina msaada kwao hata kwa jamii kwa ujumla. 
Ukiingia kwenye makundi mengi ya Whatsapp ya wasomi na wenye proffession tofauti tofauti,  utajua na utaelewa hiki ninachokisema. 
Watu wamekuwa wakiongea mambo ya kijinga ambayo hayawezi kubadilisha maisha yake au hata ya watu wengine. Wamekuwa wakilalamika tu badala ya kutumia elimu yake kufanya mabadiliko na hatimaye kubadilisha kabisa tatizo la ajira hapa nchini. 
Serikali imekuwa ikipoteza pesa nyingi kusomesha watu ambao hawawezi kuwa wabunifu kwa kutumia elimu zao na hatimaye kuisaidia serikali kutatua matatizo yanayoikabili nchi yetu. 
Rafiki yangu,  natumai una elimu ya kutosha kabisa, sasa kaa chini ufikiri ufanye nini kwa kutumua elimu yako ili ufanye mabadiliko katika jamii inayokuzunguka. Ninaona kitu kikubwa sana ndani yako ambacho kinaweza kuishangaza dunia,  naona idea nyingi sana ndani yako,  fanya,  fanya ndugu Mungu atakusaidia. 
Dunia imebadilika sana,  dunia inakimbia sana,  lakini wengi wetu tunatembea tena kwa madaha kabisa.  Tunapoteza muda mwingi sana kwenye mitandao ya kijamii bila faida yoyote.  Watu wengi hawajui kama unaweza ukatumia mitandao ya kijamii kutengeneza pesa na hatimaye kubadili maisha yako kabida. 
Mimi ni miongoni mwa watu ambao wanatumia sana mitandao ya kijamii lakini ninaitumia kutengeneza wateja wa kuja kununua bidhaa zangu,  ninauza vitabu vyangu kupitia facebook,  whatsapp,  blog na hata instagram. 
Mitandao ni mizuri sana,  lakini inategemea unaitumiaje. 
Kama unahitaji kujua utawezaje kutengeneza pesa kwenye mitandao ya kijamii tuwasiliane 0754745798 –  whatsapp na nitakusaidia. 
Naomba niishie hapo kwa leo,  naamini nimeeleweka vuzuri na utafanyia kazi haya. 
Pia jipatie kitabu kitakachoweza kukusaidia kukufundisha hatua kwa hatua utengenezaji wa chaki zinazotumika mashuleni na utaweza kutengeneza hadi 60,000/- mpaka 90,000/- kwa carton moja ya chaki. 
Asante. 
Wasiliana nasi:-
Pius Justus Muliriye
0754745798 – whatsapp 
0657128567
piusjustus28@gmail.com

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *