USIPOLIPA GHARAMA KWA MAFANIKIO YAKO UTALIPA GHARAMA KWA KUFELI KWAKO.

Habari rafiki yangu mpendwa,  naamini uko salama kabisa na unaendelea vizuri na maisha,  pia nina imani umejiandaa vyema na sikukuu zijazo,  nikutakie kila lakheri katika hilo.

Somo la leo ni juu ya kulipa gharama kwa mafanikio yako.

Karibu tuendelee,
Katika maisha kuna siri kubwa sana iliyojificha,  na ili uijue siri hiyo ni lazima ulipe gharama,  si kidogo,  narudia tena lazima ulipe gharama.

Kuna kitu kinaitwa “SECRET”  au “SIRI”.  Imeitwa siri kwa sababu si wengi wanaijua,  na wanaoijua wamelipa gharama kuijua.
Kwa mfano,  unapoona tangazo katika mitandao ya kijamii kwamba kutakuwa na semina ya kitu flani unapita tu au unalike unaendelea na kufungua picha au unaendele kuchati tu bila kujua unapoteza muda kwenye mitandao ya kijamii bila faida yoyote na bando likikuishia mawazo yanabaki palepale,  yaani bando limeisha,  hujapata faida,  unawaza utapata wapi bando la kuingia tena facebook,  instagram,  twitter au mitandao mingine kutafuta umbea au kitu kinachoufurahisha moyo wako kumbe kinakuua bila wewe kujua.

Usiogope kulipa gharama kuhudhuria semina live au hata mtandaoni ili ufungue akili yako,  vinginevo utaendelea kuishi maisha yaleyale na utabaki kulalamika kila siku na hapo ndipo utalipa gharama ya kushindwa kwako kujielimisha.

Watu wengi wanashindwa kununua vitabu vitakavyowaelimisha kutoka hapo walipo lakini wako radhi kununua bando na kuchati tu na maisha yao kubaki palepale.  Nakuibia siri msomaji wangu,  siri kubwa ya mafanikio ya maisha yamefichwa kwenye vitabu,  asikudanganye mtu kwamba kuna mganga atakufanya tajiri,  soma sana utaona maisha yako yanavyobadilika.

Mfano mzuri nimeandika vitabu viwili ambavyo vina siri kubwa sana ya biashara za kawaida ambazo watu hawazijui,  ukiweza kuchukua biashara moja kati ya nyingi zilizomo kwenye kitabu hicho nakuhakikishia hutakaa ujute katika maisha yako.  Usipoamua kufanya hivo ukidhani utamfaidisha aliyeandika kitabu unajidanganya ndugu yangu,  utalipa gharama kubwa kwa kushindwa kuchukua hatua mapema.

Nimalizie kwa kusema,  usiogope kununua kitabu sh. 5000/- kitakachokufundisha jinsi ya kuboresha maisha yako,  ipo siku utalipia kwa zaidi ya hiyo sh. 5000/- na utajuta kwanini hukuchukua hatua mapema.

Mwaka unaokuja sitauza tena kitabu changu chochote kwa sh. 5000/-, hii ni kwa sababu biashara imebadilika.  Chukua hatua mapema.

Jipatie vitabu hivi kama utahitaji ili vikusaidie kupata biashara ya kufanya mwaka 2017, usikubali kuishi maisha yaleyale mwaka 2017,  amua kubadilika sasa.

Kitabu cha kwanza kinahusu jinsi ya kumiliki kiwanda nyumbani kwako na utengeneze kipato bila kikomo.  Bonyeza hapa kukipata??ZIJUE BIASHARA ZAIDI YA 10 UNAZOWEZA KUFANYA NA UKAPATA MAFANIKIO MAKUBWA.

Kitabu cha pili kinahusu jinsi ya kutengeneza chaki zinazotumika mashuleni,  kitabu hiki kitakufundisha hatua kwa hatua jinsi ya kutengeneza chaki hizo,  na pia kitakufundisha jinsi ya kupata mtaji wa kuanzisha biashara yako.  Kupata kitabu hicho bonyeza hapa ??MILIKI KIWANDA CHA CHAKI NYUMBANI KWAKO. Unaweza pia kupata sample ya kitabu hicho kwa kubonyeza hapa??sample ya kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA CHAKI NYUMBANI KWAKO.

Asante sana kwa kuwa pamoja na mimi mpaka hapa.  Nikutakie maandalizi mema kuelekea kwenye sikukuu za mwisho wa mwaka.

Tafadhari usiache kuweka maoni yako hapa chini na pia kwa chini ya makala haya kuna sehemu ya kujiunga na mtandao,  tafadhari jisajili ili uwe karibu na mimi kila mara.

KARIBU.

Wasiliana nasi 
Pius Justus Muliriye 
0754745798-whatsapp 
0657128567 
piusjustus28@gmail.com 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *