HUWEZI KUPATA MAFANIKIO BILA KULIPA GHARAMA.

Habari rafiki mpenda maendeleo, naamini upo salama kabisa na unaendelea vizuri na harakati za kuboresha maisha yako. nami pia niko salama na ninaendelea vizuri na harakati za kuendelea kukuelimisha ili kwa pamoja tuweze kufikia kile tulichokitarajia katika maisha yetu.

Leo nataka nikukumbushe tu, huwezi kupata mafanikio bila kulipa gharama, iwe ya pesa au kitu chochote kile kama Muda n.k, kila penye mafanikio pana gharama zake, kwa mfano watu wengi wanapoona mtu ana maisha mazuri sana wanahisi mtu yule kayapata kirahisi sana mpaka wengine wanadiriki kusema wamerithi mali kutoka kwa wazazi wao. 

Unapoona mtu anaendesha gari zuri, anaishi kwenye nyumba nzuri, ana kazi nzuri, ana mke na watoto wazuri ujue amelipa gharama kubwa sana kuvipata hivyo vitu. Ametumia muda wake mwingi sana kuhangaikia yote hayo, lakini mtu mwingine hawezi kulipia gharama kidogo za kujifunza katika semina mbalimbali, yupo radhi aharibu pesa yake kwa vitu ambavyo si vya msingi. Katika semina au mafunzo yoyote yale unapata kujua ambayo huyajui na utashangaa unapata mwanga na kubadili mtizamo wa maisha yako kabisa.

mfano mzuri ni mimi mwenyewe, mwanzo nilikuwa sielewi wala sichukulii maanani mambo haya, lakini nilipopelekwa na rafiki zangu kwenye semina moja hivi, ilinifungua mpaka sasa nimenufaika na mafunzo, sasa ninagharamia mafunzo mbalimbali na yananinufaisha sana.

Siku moja nilikuwa nikiangalia documentary ya CHRISTIAN RONALDO, nafikiri kila mtu anamjua, alikuwa akionyesha utajiri wake, kwa kweli ni mtu mwenye mafanikio makubwa sana, alisema statement moja tu “people think that we got these things easily,No! we paid the price by working hard” kwa hiyo nikushauri tu rafiki yangu, endelea kupambana, utafanikiwa tu, usichoke kujifunza ujuzi mbalimbali utakusaidia.


Kwa kusema hayo nikutakie kila lakheri katika siku hizi zilizobaki kuumaliza mwaka huu wa 2016 na kuukaribisha mwaka 2017, pia endelea kutembelea ukurasa huu ili upate kueleimika na kuweza kuanza mwaka kwa kishindo kikubwa.
Pia kwa kuumaliza mwaka na kuuanza mwaka vizuri, nimekuandalia vitabu vitakavyoweza kubadili kabisa fikra zako  na vitakujenga na utaweza kufikia kile unachokitaka katika maisha yako. vitabu hivyo ni kama
  • UTENGENEZAJI WA BIDHAA ZA VIWANDANI.  (Katika kitabu hiki utajifunza hatua kwa hatua jinsi ya utengenezaji wa bidhaa mbalimbali ambazo zinapendwa na kutumika na watu wengi sehemu yoyote ulipo, bidhaa hizi ni kama Sabuni  ya mche, sabuni ya maji, sabuni ya kusafishia vyooni, batiki, cahki n.k. Hii itakufanya umiliki kiwanda kidogo nyumbani kwako kwa kuweza kuzalisha moja ya bidhaa tajwa hapo juu). 
  • UTENGENEZAJI WA CHAKI. (Katika kitabu hiki utajifunza jinsi unavoweza kumiliki kampuni yako au kiwanda kidogo ambacho unaweza kuzalisha na kuuza chaki mashuleni na ukapata faida kubwa sana, kitabu hiki kitakufundisha hatua kwa hatua jinsi ya kutengeneza chaki hizi na utaelekezwa ni wapi zinapatikana malighafi za kutengenezea na masoko yake pia. )
  •  HOW TO SET ACHIEVABLE GOAL. (Katika kitabu hiki utajifunza mambo mengi sana juu ya jinsi ya kuweka malengo ambayo yanafikika, kitakufundisha ni njia zipi ufate ili ufikie yale unayotarajia mwaka 2017. ) 
Katika picha hiyo kuna maelezo kamili ya jinsi ya kupata vitabu hivyo, vitabu hivyo utavipata kwa njia ya whatsapp au email yako, tutakutumia na utavisoma kwenye simu yako. Usiogope kugharamia elimu hii kwani ndio msingi wa maisha yako, usichoke kujifunza.

Faida ya vitabu hivi ni moja kuu, vitaweza kukufanya uwe wa tofauti na wengine na utaendelea sana wengine wakikuangalia. Na mimi pia nilikuwa ivo, sasa ivi wenzangu wananishangaa sana hawaamini kama ni mimi, kumbe ni elimu niliyofanya juhudi kuipata. Elimu hii ni ya wachache, si wengi wanayo, una bahati sana kuipata, usiache iondoke.

Karibu sana tukuhudumie, usisite kuwasiliana nasi kwa Whatsapp 0754745798 au tupigie kwa ushauri.

ASANTE SANA.

Pius Justus Muliriye
0754745798 – Whatsapp
0657128567

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *