MALIZA MWAKA KWA USHINDI WA KISHINDO.

Habari mdau wa ShuleTanzania,  napenda kukupongeza kwa kuendelea kuwa na mimi mpaka muda huu tukielekea ukingoni mwa mwaka huu wa 2016.

Natumai umefaidika na makala ambazo nimekuwa nikiandika mara kwa mara tangu mwaka 2014,  pia nikushukuru kwa wewe ambaye umekuwa ukinunua vitabu vyangu ambavyo vimekuwa vikikufundisha mambo mbalimbali ya maisha.

Kwa kuwa tunaelekea ukingoni mwa mwaka basi ningependa nikupe changamoto ya kujiuliza ni kwa kiasi gani umeweza kufikia ndoto zako?
Umekuwa ukipanga kila mwaka utafanya mambo flani lakini ni kwa kiasi gani umekamilisha yale uliyoyapanga?

Asilimia kubwa sana ya wengi wanaopanga kufanya mambo flani hawafikii yale waliyoyapanga. Hii imekuwa ikiwafanya watu wengi kutofikia mafanikio waliyoyapanga katika maisha yao na kuishia kulalamika tu bila kuchukua hatua.

Baadhi ya mambo ambayo huwa yanafanya watu wengi kushindwa kufikia malengo yao ni:-

  1. KUPANGA MALENGO YASIYOFIKIKA.  

Watu wengi wanakuwa na malengo makubwa sana mpaka yanawashinda kutekeleza ndio maana unaona wengi wanashindwa kubadilika kwa sababu hiyo, sio vibaya kuwa na malengo makubwa, lakini hakikisha malengo hayo makubwa unayavunja vunja na kuyaweka madogo madogo ambayo yanatekelezeka kwa muda muafaka na hatimaye utafikia yale  makubwa.
kuhusu hili nimeandika kitabu ambacho kitakufundisha jinsi utakavyoweza kupanga mipango inayofikika, kitabu hiki kinaitwa “HOW TO SET ACHIEVABLE GOAL”kitabu hiki kitakufanya uweze kupanga mipango yako unayotaka kufikia mwaka mpya wa 2017 utakapoanza, kitabu hiki kitakufundisha hatua kwa hatua jinsi ya kutekeleza yote yale uliyopanga, yawe madogo au makubwa.

      2. KUTOHESHIMU MUDA (DEADLINE) 

Hili pia huwa linawaruudisha nyuma sana watu wengi mpaka kufikia wakati wanakata tamaa. kila mtu anapanga na anaweka mikakati yake ili kufikia malengo yake, lakini wamekuwa hawaheshimu muda au hawaweki muda wa kikomo kufanyia kazi jambo fulani. Kwa mfano, unataka kuwa na kiasi cha Sh. 2,000,000/- kwenye akaunti yako, lakini husemi lini utaweza kumiliki hizo pesa ndani ya mwaka huo, kwa kufanya hivyo huwezi kufikia malengo yako.
unachotakiwa kufanya ni kuweka muda muafaka wa kutimiza kile ulichokipanga, kwa mfano, kabla ya mwezi wa sita ninatakiwa kuwa na 2,000,000/- kwenye akaunti yangu. Hii itajufanya ufanye kazi kwa bidii bila kuchoka ili ufikie kile ulichojiahidi.

     3. KUAHILISHA MAMBO. 

Ndugu msomaji, nafikiri utakubaliana na mimi juu ya hili, kuna watu wengine hata ufanye nini, wao kuahilisha ahilisha ni jambo la kawaida kwao, unakuta mtu anatoka kazini amepanga aende moja kwa moja nyumbani, lakini akipita sehemu fulani labda kijiweni anaamua kukaa na kusahau kwamba anatakiwa kwenda nyumbani kama alivyojiahidi, hii itamfanya mambo yake yasinde vizuri.
Mtu mwingine amepanga kabla ya june mwa 2017 nitakuwa nimesoma angalau kitabu kimoja, lakini anaacha na kufanya mambo mengine ambayo si yale aliyojipangia, hii haiwezi kukufikisha pale unapopataka katika maisha yako.
Acha tabia ya kuahilisha ahilisha mambo yako, itakusaidia kufikia malengo yako.

Hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo yanamfanya mtu ashindwe kufikia malengo yake katika muda aliojipangia.
Huu ni muda wa kujipanga kumaliza mwaka kwa kishindo kikubwa kwa sababu kama umeshindwa kufikia yale uliyoyapanga mwaka unaoisha sasa ni muda muafaka wa kujisahihisha ni wapi umekosea ili urekebishe  uweze kufikia malengio yako unayoyatarajia.
Sasa unaweza ukamaliza mwaka na mpango wa kusoma vitabu ambavyo vinaweza kukusaidia kubadili fikra na kukutoa hapo ulipo mpaka pale unapopatarajia. Ninakuletea viatabu viatatu ambavyo nimeandika ndani ya miaka mitatu ambavyo vimekuwa vikisaidia watu wengi sana kuwakwamua katika dimbwi la fikra mbovu juu yao wenyewe na nchi yao, sasa unaweza ukavipata hapa hapahapa.

 Vitabu hivo ni pamoja na;

  • UTENGENEZAJI WA BIDHAA ZA VIWANDANI.  (Katika kitabu hiki utajifunza hatua kwa hatua jinsi ya utengenezaji wa bidhaa mbalimbali ambazo zinapendwa na kutumika na watu wengi sehemu yoyote ulipo, bidhaa hizi ni kama Sabuni  ya mche, sabuni ya maji, sabuni ya kusafishia vyooni, batiki, cahki n.k. Hii itakufanya umiliki kiwanda kidogo nyumbani kwako kwa kuweza kuzalisha moja ya bidhaa tajwa hapo juu). 
  • UTENGENEZAJI WA CHAKI. (Katika kitabu hiki utajifunza jinsi unavoweza kumiliki kampuni yako au kiwanda kidogo ambacho unaweza kuzalisha na kuuza chaki mashuleni na ukapata faida kubwa sana, kitabu hiki kitakufundisha hatua kwa hatua jinsi ya kutengeneza chaki hizi na utaelekezwa ni wapi zinapatikana malighafi za kutengenezea na masoko yake pia. )
  • HOW TO SET ACHIEVABLE GOAL. (Katika kitabu hiki utajifunza mambo mengi sana juu ya jinsi ya kuweka malengo ambayo yanafikika, kitakufundisha ni njia zipi ufate ili ufikie yale unayotarajia mwaka 2017. ) 

Kwenye picha hiyo kuna maelezo yote kuhusu vitabu hivyo ambavyo vinaweza vikakusaidia kumaliza mwaka 2016 au kuuanza mwaka 2017 kwa mafanikio makubwa sana.
Ukihitaji vitabu hivyo tuwasiliane kupitia Whatsapp 0754745798 

Ndugu msomaji,  nakuomba uendelee kuwa pamoja na mimi hata kwa mwaka mwingine tena tuendelee kuelimishana.

Usisite kuwasiliana nasi kwa jambo lolote la ushauri katika maisha,  nina ujuzi nitakusaidia.

SOMA: MAMBO 15 YA KUJIFUNZA KUTOKA KWA WATU WALIOFANIKIWA.

Wasiliana nasi kwa:-

Pius Justus Muliriye 
0754745798-WhatsApp 
0657128567 
piusjustus28@gmail.com 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *