Habari rafiki mpenda maendeleo,  ni matumaini yangu uko poa kabisa na unaendelea kupambana na maisha. 
Leo ningependa nikuletee hii kuhusu mambo mawili muhimu unayotakiwa kuyapata kwenye mitandao ya kijamii. Kuna mitandao mingi sana ya kijamii kwa sasa ambayo hutumika kwa namna mbalimbali,  mitandao hiyo ni kamafacebook,  twitter,  whatsapp,  yutube,  blogs,  websites n.k.  lakini yote hii ilibuniwa ili kuleta watu karibu na hapo ndipo tunaona dunia ni kama kijiji. 
Kama wewe ni mtumiaji wa mitandao hii,  basi haya mambo ndiyo unatakiwa kuyapata… 
  • KUELIMIKA (ELIMU) 
Mitandao ya kijamii inabidi ikufanye wewe uelimike kutokana na yale yanayowekwa ndani yake,  kama wewe utaingia kwenye mitandao hii halafu usijifunze kitu maana yake umepoteza muda na maisha yako yataendelea kuwa palepale na maana halisi ya mitandao hii inakuwa imepotea. Unapoingia kwenye mtandao wowote kama facebook au whatsapp katika magroup mbalimbali,  hakikisha umejifunza kitu positive,  vinginevyo utakuwa unapiteza muda. 
 Jiwekee ratiba kwamba nikiingia facebook naangalia ni kitu gani mwandishi fulani kapost kitu cha maana,  kwa mfano mimi kila siku lazima niandike makala kwenye blog yangu ya www.shuletanzania.info  na hapo unaweza ukapata mambo mengi ya kukuelimisha. 
  • KUFANYA BIASHARA. 
Mitandao ya kijamii pia inabidi uitumie ili ikutengenezee biashara,  unapokuwa na marafiki wengi kwenye mitandao hii basi unaweza ukafanya biashara kwa kuuza bidhas zako.  Kwa mfano wateja wangu wakubwa wa vitabu navyoandika huwa ni watu ninaokutana nao kwenye mitandao hii ya kijamii,  kwa hiyo mitandao hii inanifaidisha kuliko kunipotezea muda.  Kama wewe unaingia kuangalia udaku tu,  nani leo kagombana na nani basi ujue unapoteza muda.  Badilika na ujifunze jinsi ya kufanya biashara na mitandao ya kijamii. Kama utahitaji kufundishwa jinsi ya kufanya biashara kwenye mitandao ya kijamii basi nipigie 0754745798 Au 0657128567 nitakuelekeza njia za kufuata.Usikubali kutumia bando lako bila faida. 
 Kwa leo naomba niishie hapo,  nikutakie kila lakheri katika kupambana na maisha. 
Kwa ushauri,  wasiliana nasi kwa
Pius Muliruye Justus
0754745798 
0657128567 
piusjustus28@gmail.com 
Jipatie kitabu kitakachobadili maisha yako??BONYEZA HAPA KUKIPATA