DON’T WAIT UNTILL THINGS GET READY!

Nilikutana na huyu mtu James mwang’amba back 2009, alikuwa akifundisha somo la self development kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na nilipata bahati ya kuhudhuria mafundisho yake kwa siku 2 mfululizo!

Alizungumza kitu ambacho kili stick katika kichwa changu ambapo alisema USISUBIRI MPAKA MAMBO YAWE SAWA KUPIGANIA NDOTO ZAKO!!

Kwa mara ya kwanza sikumuelewa kabisa, kwa sababu nilikuwa nikifikiria huwezi kufanikiwa ukiwa katika nchi maskini kama Tanzania, huwezi kufanya lolote bila serikali kukutengenezea mazingira, na nilikuwa miongoni mwa watu wanaolalamika sana nikiona mambo hayaendi sawa!
.
.
Baada ya miaka mitatu wakati napitia makablasha yangu nikakutana na notebook niliyoandika masomo aliyokuwa akifundisha, nikakutana na sentensi hiyo tena iliyokuwa ikisema ” Don’t wait untill this get ready”…

Hapo ndipo nilipoanza kujitafuta mimi ni nani!

Siku hiyo nilipata wazo la kuandika kitabu ili niweze kushea na watanzania ujuzi nilionao na niliamini kabisa kitabu changu kingewasaidia wengi!

Nilimshirikisha rafiki yangu nikamwambia nataka niandike kitabu hiki ninaamini kitauzika sana na watu watanufaika na mimi nitanufaika pia, alicheka sana akaniambia hivi wewe unawajua watanzania???? Tangu lini watanzania wakawa wasomaji wa vitabu?? Nakuhakikishia hutauza kitabu hata kimoja unapoteza muda na nguvu zako achana na wazo hilo, kwanza gharama za kuzalisha kitabu hicho ziko juu sana hutaweza kabisa.?

Kusema ukweli alinikatisha tamaa, nikaanza kuwaza upya juu ya maoni yake, lakini nikakumbuka kabisa mwalimu wangu James Mwang’amba aliniambia kijana “Usisubiri kabisa mambo yawe sawa ndio uchukue hatua” ndipo nilipojiambia sitasubiri mpaka watanzania wapende kusoma vitabu ndipo niandike…..!! Nikaanza mara moja kuandika na nikakamilisha kitabu changu ndani ya mwezi mmoja!

Shida nyingine ikaja, Sina pesa ya kupublish kitabu changu pamoja na kuzalisha copy nyingi na kusambaza, nikakwama na nikaacha na kuendelea na mambo mengine!!
.
.
Lakini mwaka 2017 mwezi wa kwanza nikapata wazo ambalo lilinifanya nishindwe kulala kabisa, nikakumbuka kuwa nina simu ya smartphone, nima laptop ambayo nilinunua wakati nipo chuo kikuu lakini vikawa havinisaidii chochote, ndipo nilipoanza kuvitumia na kuanza kusoma wenzetu nchi za nje wanafanya nini!..

Nikapata mwanga na nikaanza sasa kufanyia kazi elimu ile niliyoipata na mwaka huo huo mwezi wa nne nikafanikiwa kufungua channel yangu ya Youtube na nikarekodi video yangu ya kwanza kwa kutumia simu yangu ya mkononi nikizungumzia kitabu changu na faida zake na kukitangaza kwa atakayehitaji kupata ujuzi huo nitamtumia kwenye whatsapp au email yake…..Sikuamini macho yangu???

Nilipata oda nyingi sana, na sasa video ile ina views zaidi ya 20,000 na nimeshauza copy takribani 3650 mpaka sasa bila gharama ya kutoa copy wala usambazaji, copy zote nimetuma nikiwa ndani kwangu, kwenye gari nikiwa nasafiri, nikiwa kijiweni napiga story na marafiki zagu n.k. hii ndio nguvu ya TEKNLOJIA, wewe unatumiaje mapinduzi haya ya teknolojia??

Siku hizi watu hawahangaiki kufanya malipo MPESA, TIGOPESA n.k ziko kila mahali mtu akipenda kitu hasumbuki kulipia, tumia nafasi hiyo utafanikiwa.

Nakushauri wewe kijana mwenzangu, mazingira yasikifanye ushindwe kupigania ndoto yako, usisubiri serikali itengeneze mazingira ya biashara ndipo ufanye, wakati huo fursa itakuwa si yako tena, isome jamii yako ina matatizo gani kisha tafuta jawabu la matatizo yao na maisha yako yatabadilika.

Asanteni sana na niwatakie siku njema!
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Pius J. Muliriye
www.piusjustus.com

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *