MWANAMKE MSOMI ALIYEJIKITA KATIKA USHONAJI

Joyce Ryoba  ni mwanamke mwenye shahada ya pili(Masters Degree) katika elimu ya jamii kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam ambaye hakutaka kuajiriwa na sasa akiwa amejikita katika ubunifu wa nguo .

Akiwa anasoma shahada ya kwanza mwaka wa mwisho  Joyce alianza kujitoa kusaidia watoto walio mtaani na hata alipomaliza aliendelea kufanya hivyo japo maisha yalikuwa si rafiki .

Baadaye alianzisha Asasi isiyo ya kiserikali(NGO) iliyoitwa Hope for Children lakini kwa sababu ya changamoto za hapa na pale nyingi hasa za kifedha hakuweza kuedelea na Asasi hiyo .(Joyce anasema )”Katika muda wote huo sikuwa na mtu wa kunishika mkono ,sikujuana na mtu mkubwa yeyote  hivyo sikuwa na wa kunisaidia hasa kupata fedha za kuwasaidia yatima hawa”Joyce anasema kuwa hakutaka ajira tokea mwanzo kwa kuwa kujitoa kwake kwa vijana na watoto mtaani kulichukua muda wake mwingi kwa kuwa ilibidi nifanye kazi masaa 24 na hivyo akajua hakuna kazi ya kuajiriwa inyoweza kumpa nafasi ya kusaidia watoto walio na uhitaji na  akaamua kutoomba kazi ili aishi ndoto zake.

Baadaye Joyce alifungua kiwanda cha ushonaji ambapo anasema anashona nguo za viwango sana na za aina zote (nguo za event,casual ,official n.k.Joyce ana mafundi sita wa ushonaji ambao amewaajiri  na anatumia mashine za ushonaji za viwandani (industrialized Machine).Mapumziko yake sasa ni Jumapili kwa ajili ya Ibada maana anapata kazi nyingi sana .Alivyoulizwa amewezaje kufanya vitu vikubwa bila mtaji alikuwa na haya ya kusema “nilianza kufanya kazi kama fundi nikajiunga na vikoba nikakopa pesa “.

Akieleza changamoto nyingine aliyokutana nayo Joyce alisema”Changamoto nyingine ilikuwa ni uchaguzi wa mume atakayenioa .Wanaume wengi waliniogopa kwa sababu nilikuwa sina chochote na niko busy na watoto wa mtaani lakini kwa kuwa nilikuwa na maono yangu(clear vision) sikutaka kupata kipingamizi chochote kutimiza ndoto zangu hivyo niliomba na kufunga kupata mume atakayeinua maono yangu.

Maombi yangu yalikuwa hivi Yesu nakuomba mume wangu abaki asiye wangu aondoke bila kumwambia simtaki.”Akieleza mafanikio yake mpaka leo Joyce anadokeza:” Nilikuwa sina uwezo wa kusaidia wahitaji sasa naweza Nina mtoto anasoma darasa la saba huyo   nilimtoa mtaani sasa namsomesha  mwingine yuko kidato cha nne Kuna kijana mwingine sasa amekuwa mjasiriamali ameajiri wenzie kumi kwa siku anawalipa elfu kumi kila mmoja ,amefungua viwashio kariakoo na mahala pengine penye mkusanyiko wa watu .

Mafanikio mengine ni Network .Ushonaji umenikutanisha na watu wengi ikiwemo Vijana wa kijana Jithamini,Wabunge na watu wenye mamlaka katika Nchi  kwa vile ni wateja wangu. Nimefanikiwa pia kujua tabia mbalimbali za watu na namna ya kuendana nazo.Toka nimeanza kushona nimeacha kununua nguo za kichina navaa made by Myself only”

Akiongelea swala la wasomi kubagua kazi ,Joyce alikuwa na haya ya kusema kutoka katika kilindi cha moyo wake“nawashauri wasomi wasibebe degree zao kichwani wakiwa mtaani, wanapaswa kuziweka moyoni .Wachape kazi katika mazingira yoyote bila kukata kuangalia walisomea nini .Pili washughulishe mikono na akili zao kwa kuwa ndiko utajiri ulikojificha .Tatu wamche Bwana kwa kuwa watapata maarifa na fursa maana akili na maarifa hutoka kwa Mungu “.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *