unaweza kuangalia na hii pia;
Baada ya hapo basi tuendelee na mada yetu ya leo;
Ukifuatilia kwa kina sana utagundua watu wengi wanapoteza muda na fursa nyeti ya kutangaza shughuli au biashara wanazofanya.
unajua ni kwa njia gani ilivyo rahisi kwa sasa kukutana na watu wengi unaowafahamu na usiowafahamu pia kupitia mitandao ya kijamii?
Hivyo basi, tumia fursa hii kutangaza biashara yako au kazi unazofanya kwa huo umati wa wanajamii. Zingatia maadili na sheria za nchi unapotangaza biashara yako.
kizuri zaidi hapa, hakuna gharama kubwa ya kujitangaza, ni bure kabisa! ikiwa unahitaji kutengeneza ukurasa ili uwekwe kwenye upande wa matangazo ndio unalipia kidogo kwa mtandao husika.
Naomba nikuhakikishie kuwa kwa kipindi hiki cha maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia ni rahisi mno kuwasiliana na watu wengi sana kuliko kawaida kwa muda mfupi sana.
Imekuwa ni mazoea mtu kuweka picha mbalimbali mfano akiwa anakula, na nyinginezo za kujionyesha ili watu wabonyeze kitufe “LIKE” Je! Unaingiza shilingi ngapi kwa watu kubonyeza kitufe cha “LIKE”? au unalipwa shilingi ngapi kwa kubonyeza kitufe cha like?
Kuna wengine kazi yao kubwa ni kubonyeza kitufe cha LIKE hata kama kuna picha ya msiba au majonzi au kuna picha ya tukio la maovu.
Nisieleweke vibaya, namaanisha ni vizuri pia kuangalia faida ya mitandao hii ya kijamii kwa upande mwingine tofauti, hatimaye kujiongezea kipato.
Haya tuiachane na hilo, tufanye nini ili kutengeneza pesa kupitia facebook, instagram na mengineyo?
- wajulishe marafiki kuhusu biashara yako, weka picha ya bidhaa uanazouza na mawasiliano
- tumia muda vizuri kwa kuhakikisha “unachart” na mtu bila kusahau kumueleza biashara yako.
- tengeneza ukurasa unaoeleza bidhaa yako au biashara yako, ukiweza ilipie ili ikae upande wa matangazo kutegemeana na mtandao wa jamii husika
- kwa wale ewanaotafuta kazi, weka sifa ulizo nazo watu wajue uwezo wako, kwa hakika utajikuta unaunganishwa kupata kazi. usione aibu kujielezea kuwa huna kazi.
- tumia mitandao ya kijamii kupata fursa za kubuni aina ya biashara au huduma kwa jamii.
Kama umevutiwa na kuanza kufanya biashara mtandaoni hasa kutumia facebook basi huna budi kuwa na copy ya kitabu hiki kikupe mwongozo wa jinsi ya kuanza kutangaza biashara yako mtandaoni.