Kila Biashara Sasa Inahusisha Intaneti, Kama Bado Biashara Yako Haipo Kwenye Intaneti, Umechagua Kupoteza Wateja.

Kila wakati ambapo dunia inabadilika, huwa kuna watu hawayaamini mabadiliko hayo, na hivyo kuendelea kufanya kile ambacho walizoea kufanya. Kila teknolojia mpya inapokuja, wapo watu wanaoiangalia teknolojia hiyo kama kitu cha kupita pekee. Na wengi huona ni vitu vya vijana na siyo kwa watu wazima ambao wameshajenga misingi yao.Lakini ipo fursa ambayo siyo tu ipo na kuendelea kuwepo, bali inaendelea kuwa kubwa kadiri siku zinavyokwenda. Yaani fursa hii inakua kwa kasi na kuzidi kuwa bora zaidi.

Fursa ninayoizungumzia ni mtandao wa intaneti.Najua umekuwa unasoma makala nyingi ninazoandika kuhusu kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti, na labda unajiambia tayari nimeshajua hilo. Ninachokuambia ni kwamba bado hujajua, hakuna anayejua maana kila siku tunashangazwa na mtandao huu.Kila siku kuna uvumbuzi mkubwa unagundulika kwenye matumizi ya mtandao huu, na watu wengi, wanajua labda asilimia 10 tu ya matumizi ya mtandao huu, ambapo ni kuwasiliana na wengine.

Hivi unajua ya kwamba kila biashara sasa, ndiyo nimesema kila biashara ni biashara inayohusisha mtandao wa intaneti?Najua unaweza kusema hapana, kwa sababu labda biashara yako ni duka la mahitaji muhimu. Labda unauza vitu vidogo vidogo vya matumizi ya nyumbani. Na kuona kwa nini niwe kwenye mtandao, wakati wateja wangu ni watu waliopo kwenye mtaa wangu, ambao wakipita wanaona duka langu?
Nina swali moja kwako, je biashara hiyo ndiyo unapanga kuifanya maisha yako yote? Kweli unapanga maisha yako yote uwe na biashara ya duka la mahitaji ya nyumbani pekee? Kama jibu ni ndiyo basi unaweza kuishia hapa, kwa sababu hakuna kubwa utakalobeba hapa.

Lakini kama jibu lako ni kuwa mfanyabiashara mkubwa, zaidi ya hapo ulipo sasa, basi unahitaji kuanza kufikiria makubwa, na hapo mtandao wa intaneti ni muhimu sana kwako. Unahitaji kuanza kuitengeneza picha kubwa ya biashara yako kwa kutumia mtandao wa intaneti.Unahitaji kuijua ndoto kubwa ya biashara yako, na kuangalia namna gani unaweza kufika pale, halafu uangalie jinsi gani unaweza kuanza kwa kutumia mtandao wa intaneti.Kwa mfano kama ndoto yako ni kuuza vitu vya jumla baadaye, unaweza kuanza kwa kuwa na blog au tovuti ambayo inaelezea ile biashara ambayo unafanya au unapanga kufanya.

Unaweza kutumia blog au tovuti yako kama sehemu yako ya kuanzia, kwa kuonesha bidhaa unazouza na watu wakaweza kuziagiza moja kwa moja na ukawatumia. Kwa njia hii unaweza kuanza kidogo, bila hata kuwa na eneo kubwa la kuweka vile vitu unavyouza.

Pia unaweza kutumia mtandao wa intaneti kuwawezesha watu kufika kwenye biashara yako. Kwa kutumia blog yako kuwaelekeza ulipo. Au pia kutumia mtandao wa google kuiweka biashara yako kwenye ramani ambapo mtu akitafuta anaelekezwa.Muhimu zaidi unaweza kutumia mtandao wa intaneti kuifuatilia biashara yako hata kama upo mbali na biashara yako.

 Unaweza kutengeneza mfumo wa kupiga mahesabu wa biashara yako ambapo ukiwa popote unaweza kufuatilia kila kinachoendelea kwenye biashara yako.Kila unachofikiria kufanya biashara yako, kuna namna mtandao wa intaneti unavyoweza kukusaidia. Ni wewe kufanya utafiti na kuuliza maswali mazuri na utaweza kupata majibu sahihi ya kufanyia kazi.

Kila biashara sasa inahusisha mtandao wa intaneti, kama mpaka sasa hujaiweka biashara yako kwenye mtandao wa intaneti, au kama bado hujaweza kutumia teknolojia hizi mpya kuinufaisha biashara yako, tuwasiliane kwa wasap 0754745798 ili tuone namna gani unaweza kutumia fursa hii vizuri.

kama ulipitwa na video zangu zilizopita unaweza kuangalia hapa chini unaweza kupata cha kujifunza.


Pia unaweza kuangalia na hii, naamini utapata cha kujifunza, karibu uitazame pia.


Asante kwa kuendelea kuwa namimi.

wasiliana nasi;

0754745798
0657128567
piusjustus28@gmail.com 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *