HATUA YA KWANZA: NAMNA YA KUWA MBUNIFU

Habari rafiki yangu na msomaji wangu wa mtandao huu wa SHULE TANZANIA;
kabla ya kuendelea na somo au makala ya leo anza kwa kuangalia video hii naamini hutabaki kama ulivyo, utapata somo muhimu sana litakalobadilisha maisha yako kabisa.

KARIBU UTAZAME!


HATUA YA 1.

NAMNA YA KUWA MBUNIFU




Ubunifu ni uwezo wa kuvumbua bidhaa au huduma mpya ama mbinu mpya za namna ya kukamilisha jambo kama inavyotakiwa. Uwezo huu upo kwa kila mtu. Namna ya kuujua na kuutumia ndiyo inayotofautiana kati ya mtu na mtu.                                                                                                                                                       

Pamoja na kuwa sifa ya mjasiriamali halisi, ubunifu ni ujuzi unaoweza kujifunzwa, kujaribishwa na kutumiwa; hata kama hukuzaliwa nao.

Maisha ya karne hii ni tofauti na ya karne iliyopita. Katika karne hii ubunifu wa kila mtu anahitajika sana; hata kama yeye si mjasiriamali au mfanyabiashara. 

Ubunifu unatakiwa kwa wafanyakazi wa kawaida pia. Mfanyakazi hodari ni Yule anayetumia ubunifu katika kukamilisha majukumu ya kazi zake; kwa haraka na kwa ufanisi.
 Ubunifu wa meneja au mkurugenzi, unahitajika sana katika kubuni na kusimamia utekelezaji wa mipango ya biashara yake.

Mjasiriamali naye , hawezi kusonga  mbele; kama hakuzi ujuzi wa ubunifu wake. Ujuzi katika ubunifu ni uwezo wa kutumia maarifa na mbinu zinzo mhamasisha mtu atambue kile anachoacha kufanya au kinachomshinda akifanye au akishindwa. Na kwa kukifanya au kukishinda; ubunifu wake utaonekana.

Ubunifu unawawezesha watu kung’amua fursa zilizojificha na kujiandaa kuzichangamkia haraka.

Hatua za kujiandaa ni pamoja na kujitayarisha kushinda vikwazo vinavyoweza kuzuia utekelezaji wa ubunifu mzuri.

Katika sehemu hii, tutajifunza mambo mengi ikiwa ni pamoja na namna ya kuwa mbunifu, hata kama unadhani  hukuzaliwa mbunifu. Sehemu hii ya kwanza inamaarifa na mbinu za kumhamasisha msomaji  atambue uwezo wa ubunifu wake. Ajue namna  ya kushinda vikwazo vilivyopo katika ubunifu. Atumie ubunifu sahihi katika kuanzisha na kuendesha biashara au mradi wowote kwa mafanikio.


Wako katika Mafanikio
Pius J. Muliriye
0754745798
piusjustus28@gmail.com

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *