MAMBO NANE YA KUFANYA ILI KUJENGA NA KUKUZA BIASHARA YAKO.

Kujenga biashara itakayofanikiwa unahitaji ujuzi na uelewa mkubwa wa hiyo biashara na soko lake. Uelewa mkubwa hupatikana baada ya kuanza.
Kwa mfano tayari una wazo bora la biashara na nia ya kujenga bishara yenye mafanikio. Mambo muhimu unayotakiwa kujua unapotaka kuanza au unapoanza biashara kwa mara ya kwanza:

1. Epuka malengo yasiyokuwa na uhalisia. Biashara nyingi mpya zilizoanzishwa na watu wasiokuwa na uzoefu MARA NYINGI HUANGUKA NA KUSIMAMA hivyo hutakiwi kuogopa.

2. Hakikisha bidhaa yako au huduma ina ubora wa kutosha ili umudu ushindani.

3. Usitazamie faida ya haraka kwenye biashara mpya huchukua muda hata mpaka miaka mitano au zaidi kupata faida kwa sababu kuna makosa mengi utayafanya kwa kutokuwa na uzofu wa kutosha, wateja wa kutosha, mtaji wa kutosha na wafanyakazi wa kutosha NA MWANZO HUENDA UTAKUWA UNAFANYA KAZI MWENYEWE BILA MSAIDIZI.

4. Jitahidi kutengeneza team uwe na watu wengine ofisini angalau wawili watatu baada ya muda kwa sababu wateja huwa na mashaka na biashara ya mtu mmoja ikitokea ukipata tatizo wanahisi kukosa uhakika na huduma yako.

5. Usiogope kubadili mwelekeo wa bishara kwa sababu bishara mpya inayoanzishwa na mtu mpya ukizingatia muda mwingi wa mwanzo ni wa kujifunza, yaweza tokea ukapata wazo jipya la biashara ambalo ni halisi kulinganisha na wazo ulilokuwa nalo mwanzo.

6. Faida za kwenye karatasi juu ya meza hazina uhalisia. Pambana kufanya kazi kwa bidii na usifikirie faida kwanza. Ili biashara itengeneze faida inahitaji muda.

7. Epuka watu ambao watakufuata ili waisaidie biashara yako ikue. Kuna watu wengi watakufuata kutaka wakusaidie kuitangaza, kukutafutia fedha, n.k. Usipoteze muda na hao watu watakupotezea fedha, muda na mwisho kukuacha na maumivu makubwa.

8. Biashara haitakiwi kukata tamaa na inahitaji ujasiri. Hata kama wazo uliloanza nalo halionyeshi mafanikio inawezekana hujapata uzoefu wa kutosha kwenye hiyo biashara au baada ya muda utapata wazo linalofaa.

Kama hujaangalia video hii itakayokufungua kahisa na hatimaye kufikia mafanikio yako basi nimekusogezea hapa, isikilize na tuwasiliane kama utakuwa na maswali juu ya hayo mambo niliyozungumza.

Asante sana kwa kuendelea kuwa na mimi mpaka sasa.
Ni mwalimu wako, mjasriamali na mwandishi wa kitabu cha MILIKI KIWANDA MILIKI UCHUMI.
PIUS JUSTUS MULIRIYE
0754745798
piusjustus28@gmail.com

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *