CHA MIND IS THE MASTER KEY TO THE WORLD

CHA MIND IS THE MASTER KEY TO THE WORLD

Mind is the master key to the world ni kitabu kilichoandikwa na James Allen,kiukweli ni kitabu ambacho kimezungumzia sana kuhusu akili na mawazo kuna mengi ambayo nimejifunza kutoka kwenye kitabu hicho lakini nikupe nafasi wewe msomaji wa makala hizi kujua miongoni mwa machache ambayo nilijifunza kutoka kwenye kitabu hicho

1.Mawazo yako ndio uhalisia wa maisha yako

   Kila mtu anamawazo lakini utofauti wa mtu mmoja na mtu mwingine ni jinsi ambavyo kila mtu anawaza na maisha ya mtu mmoja na mtu mwingine hutofautiana tu kwa jinsi ambavyo watu wanawaza unaweza kuamua kuwaza vizuri au kuwaza vibaya,vyovyote utakavyoamua kuwaza ndivyo maisha yako yatakuwa hivyo,nakushauri uchague kuwaza mambo mazuri ili maisha yako yawe mazuri sio kwamba mabaya hayatakuja la hasha bali chagua mawazo mazuri.

2.Jinsi tulivyo ni matokeo ya fikra zetu

   nikweli kabisa jinsi ulivyo ndivyo unavyowaza,kwaiyo kama unataka kubadilisha jinsi ulivyo badilisha jinsi ambavyo unawaza na hii iko mikononi mwako hata kama ni ngumu kiasi gani lakini unaweza kuanza kujifunza kuwa na fikra nzuri

3.Kila mawazo unayowaza ni nguvu ambayo hutolewa nje kama maisha halisi

4.Fikiria mawazo mazuri yatajitokeza nje kama hali nzuri

   haijalishi leo uko kwenye hali gani lakini unachotakiwa kufanya ni kufikiria fikra nzuri,kama unaumwa weka fikra za kupona,kama unamaumivu weka fikra za maumivu kupotea,kama unashida weka fikra za kufanikiwa na hayo ndio yatatokea kwako.

5.Ukibadilisha mtazamo kuhusu watu wengine na wao watabadilisha mtazamo kuhusu wewe

6.Magonjwa yote duniani chanzo chake ni kwenye akili

7.Fikra sahihi ukiongeza na matendo sahihi unachopata kwenye maisha yako ni matokeo sahihi

8.Wajinga wanapenda kupiga domo na kulalamika,wenye akili wanafanya kazi na kusubiri matokeo ya kazi zao yatokee

9.Wewe ni mtengenezaji wa hatma ya maisha yako,maana kwamba hatma ya maisha yako iko mikononi mwako ni wewe tu kuamua kuchukuwa hatua kuyaendea yale ambayo yatatimiza ndoto zako.

10.Ubinafsi ni chanzo cha kutokuwa na furaha kwenye dunia,lakini pia ubinafsi ni chanzo cha umasikini kwenye dunia,hakuna sababu ya wewe kuwa mbinafsi maana utakufa masikini bure,msaidie kila mtu kukuwa,msaidie kila mtu kunyanyuka maana kiala ambae ananyanyuka kupitia mikono yako wewe unabarikiwa zaidi.

11.Kila anachokifikia mwanadam na kile ambacho anashindwa kukifikia kwenye maisha yake ni matokeo ya fikra zake.jitahidi sana kufikiria fikra ambazo zitakuletea mafanikio mbayo wewe unayataka haijalishi leo uko kwenye hali gani mbaya lakini wewe waza fikra zenye kukuletea nafuu utaona nafuu inaanza kujengeka ndani yako na kupata kile unachohitaji.

12.Kisiwa cha baraka ni tabasam,hakikisha maisha yako yanabebwa na tabasamu maana utabarikiwa kama utakuwa na tabasam

13.Nikweli tunapitia shida na matatizo lakini mwisho wa siku ni kwenda kwenye pumziko,shida unazopitia leo sio za milele zinapita tu kwaiyo usikate tamaa katika maisha yako kabisa.

UNAWEZA KUSIKILIZA VIDEO HII INAYOFUNDISHA JINSI YA KUTENGENEZA BIDHAA MOJAWAPO KATI YA NYINGI ZILIZOPO KWENYE KITABU CHA #MILIKI KIWANDA MILIKI UCHUMI.


1 thought on “CHA MIND IS THE MASTER KEY TO THE WORLD”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *