Kwa Nini Wafanyabiashara Wengi Wa Ki-Tanzania Wanahangaika Kupata Wateja Kwenye Mtandao

Kwa Nini Wafanyabiashara Wengi Wa Ki-Tanzania Wanahangaika Kupata Wateja Kwenye Mtandao

Sio siri kuwa mtandao ni HAZINA kubwa sana ya kupata wateja.

Na hazina hii inazidi kuzalisha wateja siku hadi siku kwa kasi kubwa.

Mfano mzuri ni mtandao wa Facebook wenye watumiajia zaidi ya BILIONI MOJA kwa mwezi na wenye kuingiza mapato ya zaidi ya $ 34,150,000 kwa siku (takwimu za mapato ya Facebook 2014). Mapato hayo yanatokana na matangazo yanayowekwa na wafanyabiashara kama wewe kwenye mtandao wao.

Hii inaonyesha wazi kwamba mtandao unakupa fursa kubwa sana ya kupata wateja wenye hamu ya kununua bidhaa na huduma unazozitoa kwa kubofya vitufe viwili vitatu.

Ila cha kushangaza ni kuwa wafanyabiashara wengi, hususan wakiTanzania japokuwa wanawaona wateja hao (wenye kuhitaji bidhaa au huduma wanazozitoa) mbele za macho yao, wanahangaika mno kuwapata. Na sababu kubwa ni zifuatazo:

1. Wanatangazia Bidhaa Zao Badala Ya Utatuzi Wa Matatizo Ya Wateja Wao:
Kuna mtaalamu mmoja maarufu wa Mauzo katika Mtandao (online marketer) aitwae Perry Marshal ana msemo wake unaosema,

“Every person who bought a drill NEVER wanted to buy a drill. They wanted to make holes. If you want to sell drills do not advertise information about drills, Advertise information about making holes.”

Yaani;

“Watu wote waliyonunua drili (ya kutobolea ukuta) hawakutaka kununua drili. Walitaka kutoboa ukuta. Ukitaka kuuza drili, usitangaze drili, Tangaza namna ya kutoboa ukuta.”
Kwa ufupi, unatakiwa kuwa mtaalamu mwenye kuwaonyesha wateja wako watarajiwa jinsi ya kutatua matatizo yao na sio muuzaji mwenye kung’ang’ania kuuza bidhaa zake.

Bidhaa hazitatui matatizo ya wateja wako. Ushauri na muongozo wako kwao ndio yenye kufanya hivyo.

2. Hawajengi Mahusiano Mazuri Na Wateja Wao Watarajiwa:
Japo kuwa mtandao una wanunuzi na wauzaji wengi, umejaa matapeli vile vile. Na mtu asiyekufahamu siku zote atakuona kuwa wewe ni miongoni mwa hao matapeli  hususan ukiwa unang’ang’ania sana kuuza bidhaa zako. Ukifanya hivyo wataogopa kukupa pesa zao japokuwa wanahitajia sana bidhaa au huduma unazozitoa.

Ili kujenga uaminifu kwa watu hao, ni vyema kujenga mahusiano mazuri nao kabla ya kujaribu kuwauzia chochote. Ongea nao, wajulie hali, elewa matatizo yao (yanayohusiana na taaluma yako) na kuwa tayari kuwasaidia kwa ushauri na muongozo. Maelezo zaidi ya kufanya hivyo katika nukta ya 4 na ya 5.

Ili kuhakikisha husahau umuhimu wa nukta hii, kumbuka msemo ufuatao:

“Kutangazia bidhaa yako kwa mtu asiyekufahamu ni sawa na kutangazia ndoa kwa mwanamke mzuri njiani asiyekufahamu. Japokuwa unaweza kumfaa katika maisha yake, haitomfanya yeye aache kukupiga kofi”
3. Hawana Taaluma Ya Mambo Ya Mosoko (Marketing)
Haitoshi kuwa na bidhaa au huduma nzuri. Bidhaa au huduma zako hazitojiuza wenyewe. Uwezo wako wa kufanya masoko ndio utaleta mauzo.

Achana na wahenga waliosema ‘chema chajiuza, kibaya chajitembeza’ na ufuate msemo wa Peter Drucker, mtaalamu na mshauri wa mambo ya uongozi (Management Consultant) aliposema:

“Every business has two primary functions. Marketing & Innovation”

Yaani;

“Kila biashara ina kazi kuu mbili. Masoko na uvumbuzi”
Na kweli. Kazi mbili pekee zenye kuingiza pesa kwenye biashara yako ni Masoko na uvumbuzi. Mambo mengineo yanatoa pesa nje ya biashara yako.

4. Hawana Blogu
Blogu si kwa ajili ya waandishi wa habari tu wenye mapenzi ya kuandika.

Hapana!

Utafiti unaonesha kuwa 81% ya wafanyabiashara waliokuwa katika mtandao wanaamini kuwa makala za blogu zao inaleta tija sana katika kuongeza mapato ya biashara yao [Chanzo: Hubspot]. Na sababu kubwa ni zifuatazo:

Ina wasomaji wengi kuliko tovuti ya kawaida: Kwa vile blogu inakuwa na majumuisho ya makala yenye kuelimisha wateja wako watarajiwa, watavutiwa sana kusoma na kusambaza kwa wenzao wafaidike vile vile.
Inajenga mahusiano ya karibu na wasomaji: Kwa vile makala za blogu zinaonesha jinsi ya kutatua matatizo ya wasomaji wao, usikilivu na uaminifu kwao unaongezeka, kitu chenye kurahisisha kuuza bidhaa na huduma wanazozitoa.

Ni rahisi kukusanya taarifa za mawasiliano (contact information) za wasomaji kwa ajili ya mawasiliano ya baadae.
Wenye ku blogu vizuri huonekana wataalamu na kuthaminiwa mbele ya macho ya wateja wao watarajiwa kuliko washindani wao.
Kama kweli upo SERIOUS kupata wateja wengi kupitia mtandao basi huna budi isipokuwa kumiliki blogu yenye makala mazuri yenye kuelimisha wateja wako watarajiwa. La sivyo utaachwa nyuma na kupata wateja kupitia mtandao itakuwa ni ndoto ya mchana.

6. Hawajengi Listi Ya Wateja Watarajiwa (Lead Generation)
Wataalamu wa masoko ya mtandao (online marketers) wana msemo maarufu kuhusiana na hili. Wanasema;

“Leads to your business is like blood to your body.
The less you have, the riskier it is”

Yaani

“Wateja watarajiwa kwenye biashara yako ni kama damu kwenye mwili wako.
Kila ikiwa pungufu, hatari ndio inazidi.”
Kama hupati watu kila siku wenye hamu ya kutaka maelezo ya ziada kuhusu bidhaa na huduma unazozitoa kwenye biashara yako, biashara yako itakuja kufa baada muda mfupi.

Na ndio maana kujenga listi ya watu hao kwa kukusanya taarifa zao za mawasiliano (contact information) kama jina, barua pepe na namba ya simu ni muhimu ili upate kuwasiliana nao mara kwa mara, jambo ambalo linatuleta katika nukta ya 7.

7. Hawawasiliani Na Wateja Wao Mara Kwa Mara
Kama tulivyoona katika nukta ya 6, kuwa kutokuwa na listi ya taarifa za mawasiliano ya wateja wako watarajiwa ni kosa kubwa.

Lakini kosa kubwa zaidi ni kuwa na listi hiyo lakini huna mawasiliano nao.

KITU KIBAYA SANA

Kama unataka watu hao wawe wananunua kwako mara kwa mara basi huna budi kuwasiliana nao mara kwa mara angalau mara mbili mpaka tatu kwa wiki.

Katika mawasiliano yako wajulie hali, waelimishe na uwape ofa makhsusi kwa ajili yao. Ukifanya hivyo watakupenda na kukuthamini na watakuwa hawaoni uzito kununua kutoka kwako.

Nafikiri kwa sasa ushapata picha halisia kwanini wafanyabiashara wengi wa kiTanzania na wengineo wanahangaika sana kupata wateja wa bidhaa zao kwenye mtandao.

Usiwe kama wao.

Pius Justus Muliriye
0754745798
piusjustus28@gmail.com

1 thought on “Kwa Nini Wafanyabiashara Wengi Wa Ki-Tanzania Wanahangaika Kupata Wateja Kwenye Mtandao”

  1. Yaliyo andikwa ni kweli kabisa. Wengi wetu tunashindwa kuelewa namna gani ya to create loyal customer. Kuonesha kumjali na kumthamini mteja wako inamvutia kununua bidhaa zako hata kama zinapatikana kwa mtu mwingine.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *