HAYA NDIYO MAFANIKIO YAKO

HAYA NDIYO MAFANIKO YAKO

Habari rafiki yangu.
Natumai unaendelea na harakati za kuboresha maisha yako.

Karibu leo katika ukurusa wetu pendwa wa THINK BIG START SMALL ambapo huwa tunakutana kuhamasishana na kupeana fursa za mafanikio.

Leo nataka nikushirikishe fursa ya wewe kijana mwenzangu katika kuwekeza katika viwanda, Yes, viwanda.

Naamini kuna watu hawaamini katika hili, lakini nisikilize nikueleze utaanzia wapi katika hili.

Naomba nianze kukueleza jinsi watu wa CHINA walivyoendelea kwa kasi sana na mpaka kufikia kutishia nchi ya MAREKANI kiuchumi.
Si kwamba wana bahati sana, hapana….walichukua hatua mapema na hawakusubiri wala kukaa na kulaumu serikali yao.

Watu wa china wana maendeleo kwa sababu kila nyumba iliamua kuanzisha viwanda vidogo vidogo ambavyo viko katika sehemu ndogo sana kuliko hata sehemu unayoishi wewe.

Kwa mfano leo hii unaletewa nguo kutoka china, usifikiri imetoka kwenye kiwanda kikubwa sana kama cha Bakhresa…hapana, zimetoka kwenye kiwanda kidogo sana chenye cherehani tu na mafundi ambapo hata hapa Tanzania tuna watu wanashona lakini hawaendelei sana kwa sababu ya kujidharau wao wenyewe.

Nataka nikusihi, una nafasi ya kuanzisha kiwanda nyumbani kwako;
Ebu jiulize, kwanini leo hii tutumie Sabuni, chaki, tomato source, chill source, tooth pic, shampoo, nguo n.k kutoka china au nchi zingine?

Yote haya unaweza kuyafanya wewe mwenyewe nyumbani kwako sebuleni au hata kwenye chumba cha stoo nyumbani kwako.

Najua kuna watu hawaelewi na wananishangaa, lakini nakwambia kwa kufanya hivi utayafikia mafanikio yako kwa haraka sana.

Kwa kuliona hili kama changamoto kwa vijana wengi nikaamua kuanzisha page hii ya THINK BIG START SMALL ili kuhamasisha vijana kuanza na kidogo huku wakiwaza makubwa.

Think big start small Imefanikiwa kuandika vitabu vitatu ambapo viwili viko tayari ambavyo vitawasaidia watu kuanzisha viwanda vidogo nyumbani kwao na kutengeneza pesa kila siku.

Cha kwanza kinaitwa UTENGENEZAJI WA BIDHAA ZA VIWANDANI

Na kingine kinaeleza juu ya MRADI WA KUTENGENEZA CHAKI.

Vitabu vyote hivyo vinaeleza kwa kina kabisa hatua kwa hatua jinsi ya utengenezaji wa bidhaa nyingi za kawaida zinazotumika majumbani kwetu.

Ebu jiulize; watu wanalia maisha magumu lakini je wameacha kutumia SABUNI? MAJI, CHUMVI, CHAKULA, CHIPS zenye TOMATO na MAYAI? Kula KUKU? N.k

Hii ni fursa kijana mwenzangu.

Kujifunza yote hayo jipatie nakala ya vitabu hivyo na uanze leo, usisubiri kesho, muda huu wa watu kulalamika ndio fursa ya kupata maendeleo.

Wakati watu wanalamika huwa hawafanyi chochote, sasa wewe fanya uone matokeo yake.

Bonyeza picha hii kupata kitabu hicho uanze uzalishaji mara moja na uwe wa tofauti.

Karibu sana kwa maoni au ushauri nasi tutakushauri.

Pius Muliriye Justus
0754745798
piusjustus28@gmail.com
www.shuletanzania.info

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *