BARUA YA WAZI KWA WAAJIRIWA WAPYA 2017

Habari rafiki, Natumai unaendelea vizuri kabisa na majukumu yako ya kila siku.


Karibu tena katika makala zetu za kila siku ambapo huwa tunakutana hapa kwenye tovuti yetu pendwa ya ShuleTanzania na kuelimishana hili na lile kuhusiana na maisha yetu vijana.

Kabla sijaendelea naomba nikushirikishe wewe kijana kama ni mwalimu au mwanafunzi.
Sasa tumekuja na mfumo mpya ambao unaitwa MWALIMU SHUSHA MZIGO WA VITABU. 
Mfumo huu unamuwezesha mwalimu au mwanafunzi kuachana na zama za kizamani kubeba vitabu kwenye begi na kukupa usunbufu, sasa unaweza ukapata vitabu vyote katika mfumo wa Electronic/Nakala tete au Softcopy kwenye simu yako ya mkononi yaani SMART PHONE kwa njia ya WHATSAPP.

Tuandikie meseji whatsapp-0754745798 na twambie unahitaji kitabu gani na kidato gani nasi tutakutumia ndani ya dakika chache.

NB: Utachangia kidogo tu Sh.1000/- kwa kila kitabu utakachotaka na kitakuwa chakwako kabisa.
Epuka malipo ya kila mwezi, hapa utalipa mara moja tu na utatumia upendavyo.

Maelezo kamili yapo kwenye picha hapa chini. KARIBU SANA.















Baada ya hapo tuendelee na mada yetu.
Leo napenda kutoa usia ambao nimeuweka kama barua ya wazi kwa waajiriwa wapya mwaka huu wa 2017.

Kila mtu sasa anajua kuwa serikali imetangaza na kuachia ajira za kada ya ualimu hasa walimu wenye mchepuo wa sayansi ma hesabu.

Ajira hizi zimetoka huku kukiwa na kelele nyingi sana za watu kukaa muda mrefu bila ajira, na sasa zimetoka lakini hazijatatua tatizo sana kwani kuna walimu wa sanaa wengi zaidi bado wako mtaani.

Hongera sana kwa wewe uliyebahatika kupata nafadi hiyo.
Sasa mnaenda kazini, najua mna mawazo makubwa sana juu ya maisha yenu lakini nataka nikwambie tu, dunia imebadilika sana, kama una mawazo ya kuwa sasa umaskini umeisha baada ya kupata ajira nataka nikwambie unajidanganya.

Kwanza kabisa nikupe hongera na pole pia kwani sasa umepata nafasi ya kuwa mmoja wa watumwa ndani ya mfumo (congratulation for becoming big slaves to the system). 

Najua umekaa sana mtaani, nafikiri maisha ya mtaani yamekufunza somo flani katika maisha, lakini kama hukupata somo lolote na ulikuwa ukikaa tu kila siku na whatsapp basi nakuhakikishia utaanza kuhangaika kuanzia siku ya kwanza unaripoti kazini mpaka siku yako ya mwisho unastaaf kazi.

Umepata nafasi kuingia kwenye system ambayo sio rafiki sana na maisha ya watanzania, nakuomba nikushauri mambo machache ili ufurahie kazi yako.
  • Hakikisha unajifunza kuweka akiba katika kila mshahara wako, atleast unabakiza hata laki 1 au mbili katika akaunti yako kwa ajili ya uwekezaji baadae.
  • Hakikisha unaacha anasa zote ulizowahi kufanya na unategemea kuziendeleza huku kazini. Kumbuka huku ndiko unaanza maisha rasmi.
  • Hakikisha unafanya kazi kwa bidii kwani system imebadilika, usishangae ukaachishwa kazi akaajiriwa mtu mwingine.
  • Hakikisha unajiendeleza kwa kusoma nambo mbalimbali nje ya yale uliyosoma darasani ili yakusaidie kuanza uwekezaji.
  • Fikiria juu ya nini uwekeze sasa ili kuongeza kipato chako na hatimaye uwe huru na maisha yako.
  • Weka nadhiri ya kutostaafu ukiwa mwalimu, wekeza, acha wengine wapate nafasi nao watumikie taifa.
Kwa kusema hayo maamini umenielewa na utafanyia kazi na naamini kazi itakuwa njema kwako.

UNAWEZA KUSIKILIZA VIDEO HII INAYOFUNDISHA JINSI YA KUTENGENEZA MOJA YA BIDHAA ZA VIWANDANI ZINAZOPATIKANA KWENYE KITABU CHA #MILIKI KIWANDA MILIKI UCHUMI.



Nikutakie maandalizi mema ya kuanza kazi.

Asante…

Pius Justus Muliriye
0754745798
piusjustus28@gmail.com

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *