MARA ZOTE UNAPOJIWEKEA LENGO UTAPINGWA, UTABISHIWA NA WATAKWAMBIA HAUWEZI KULITIMIZA.

MARA ZOTE UNAPOJIWEKEA LENGO UTAPINGWA, UTABISHIWA NA WATAKWAMBIA HAUWEZI KULITIMIZA.

Ndugu yangu Kwanza Achana na saut hizo zinazokupinga kabisa! Amini akili yako na uamini moyo wako. Hakuna kisichowezekana chin ya Jua. Hata siku moja ubongo wako hauwezi kukuruhusu uwaze juu ya jambo ambalo huwez kulifanya. Chochote unachofikiria unaweza kukifanya.

Inawezekana huwezi kwasasa lakini ukijifunza unaweza na hata kama utashindwa mara elfu moja lazima siku moja utakuja kushinda. Hivyo jiwekee malengo makubwa na ukumbuke kwamba, lengo lolote lisipokushtua wewe mwenye lengo au lisipowashangaza watu, lengo hilo ni la kawaida mno. Mtu yeyote yule anaweza kulifanya. Ni la nin sasa lengo la aina hiyo.?

Ngoja nikupe mfano wa Bwana mmoja…. Hapa nimwite Rama ambae alikuwa amefungiwa kwenye mahabusu chafu. Akiwa humo, alimwona mdudu mdogo sana ambaye husukuma mzigo wake kwa miguu. Akatulia kidogo kumwangalia akijaribu kupandisha mzigo mkubwa kuliko yeye kwenye ukuta mrefu.

Akavutiwa kidogo na tukio hïlo, akitaka kujua nin hasa la mdudu huyo. Je, ni kwel angeweza kupandisha mzio mkubwa kias hicho hadi juu?

Ukuta ulikuwa ni wa mita kama 5 hiv, basi akamshuhudia mdudu kwa mara ya kwanza akiusukuma mzigo wake kwa miguu. Sentimita km mia moja hv akaporomoka nao moja kwa moja hadi chini!

Haukupita muda mrefu, akashangaa kumwona mdudu anaukamata tena mzigo wake kwa miguu na kuanza kuusukuma taratibu. Safari hii alikwenda km sentimita mia tatu kabla ya kuporomoka tena hadi chini! Bwana Rama akishika kichwa chake akimwonea huruma.

Tofauti na alivyofikiri kwa alivyoporomoka mdudu huyo asingethubutu tena kujaribu kupandisha mzigo unaomzidi uwezo, alishangaa kumwona mdudu anaanza tena safar ya kupandisha mzigo uleule.

Safari hii alikwenda km sentimita mia mbili hivi. Lakin akaporomoka tena mpaka chini! Akamhurumia na kuamini huo ndio ungekuwa mwisho wake.

Alifanya hivyo mara  kadhaa hatimaye akamaliza mita zote tano na kupotelea darin. Bwana Rama alishindwa kuvumilïa akanyanyuka chini alipokua amekaa na kushangilia km vile gol limefungwa katka mechi, akitamka maneno “Kamwe mwanadamu hatakiwi kukata tamaa na ni lazima ujiwekee lengo kubwa maishani mwako!”

Kama mdudu anaweza kufanya sasa kwanin mwanadamu ashindwe? Mdudu alikua na lengo la kuvuka ukuta, akaanguka mara kadhaa lakini hakukata tamaa. Alijifunza kutokana na makosa na kuendelea na safari yake hatimaye akafanikiwa.

??
Facebook: Nicholaus Zingo
Instagram:  Nicholaus Zingo
Whatsapp: Adm wa Group la Mbinu Za Mafanikio
Nuru Fm Iringa~Kona ya Vijana
          Contact:  0718001890/0763305168

1 thought on “MARA ZOTE UNAPOJIWEKEA LENGO UTAPINGWA, UTABISHIWA NA WATAKWAMBIA HAUWEZI KULITIMIZA.”

  1. Ni fundisho zuri! Ni lazima tuwe tayari kukabiliana na changamoto za kila siku, ziwe ni hamasa katika kufikia mafanikio yetu. Ni ukweli usiopingika kuwa lazima kukutana na misukosuko hata wakati mwingine kutaka kukata tamaa unapoyaendea mafanikio.

    Cha msingi ni kutokata tamaa.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *