NYOSHA MKONO MFUKONI NA UTOE PESA UIWEKE KATIKA MCHAKATO, MANA PESA HAZIJAWAHI KUZALIANA NDANI YA MFUKO.

NYOSHA MKONO MFUKONI NA UTOE PESA UIWEKE KATIKA MCHAKATO, MANA PESA HAZIJAWAHI KUZALIANA NDANI YA MFUKO.

Siku moja, nilitembelewa na rafiki yangu na kuniuliza kama nilikuwa na wazo lolote la biashara ambalo ningeweza kumpa ili aanze kwasabbu alikua na mtaji.
Nilikaa kinya kwa muda na Nikaanza kumueleza,
“Vipi ukianza biashara ya samaki kuwatoa mwanza na kuja kuwauza hapa Dar”.
Akakaa kimya kwa muda na kujibu , “Je gari likiharibika njiani na barafu la kutunza hao samaki likayayuka,samaki wakaoza si nitapoteza mtaji wangu”.

Nilichukua notebook yangu na kuangalia biashara  nilizowahi kuziandika.
Nikampa hii nyingine, Vipi Kama utaenda kununua nyanya mashambani kwa wakulima na kuja kuziuza katika masoko makubwa hapa Dar. Aliniangalia akanijibu “Wewe Zingo unataka Pesa yangu ipotee eti, mana biashara hii nyanya pia naskiaga kuna wakati zinakosaga wateja mana zinakuwa nyingi sokoni “.

Nilikaa kimya kwa muda huku nikitafakari majibu ya rafiki yangu na nikagundua huyu anapenda kuiona pesa yake iwepo tu mfukoni, ilionesha anapenda kuzishika na kuzirudisha mfukoni pesa yake. Nikagundua huyu si mfanyabiashara, mana hauwezi kuwa mfanyabiashara Kama anaogopa kupoteza pesa katika uwekezaji unaonesha uwelekeo wa muendelezo ununuzi wa bidhaa utakayokuwa unaiuza.

Yani rafiki yangu aliogopa hata kuanza kufanya biashara ya samaki kwasabbu aliogopa kupoteza pesa take…….Ukweli nakwambia mchawi wa kutofanikiwa ni wewe mwenyewe. Wewe ndo mchawi, anza kuwekeza pesa ili ilete PESA.  Anza chini kwa tabu ili baadae ule kwa furaha

Bila kuanza chini, hata kama utaanza kwa tabu ukiwa mvumilivu ndipo utatengeneza uimala wa safari yako ya mbele. Waingereza wana msemo mmoja unasema “The harder you work the luckier you become”.

Maana ya msemo huo ni kwamba kadri unavyofanya kazi kwa nguvu ndivyo bahat yako inavyozidi kuongezeka. Hivyo basi juhud ni kuni kwenye moto wa mafanikio. Hata kama kuna bahati, haipo sababu ya wewe kuketi tu bila kujiwekea malengo ya kutoka mahali ulipo ukisubiri bahati au kuwekeza kama unauwezo wa kuwekeza.

‘NYOSHA MKONO MFUKONI NA UTOE PESA UIWEKE KATIKA MCHAKATO, MANA PESA HAZIJAWAHI KUZALIANA NDANI YA MFUKO. ‘

?
Facebook: Nicholaus Zingo
Instagram:  Nicholaus Zingo
Nuru Fm Iringa~Kona ya Vijana
          Contact:  0718001890/076330516

UNAWEZA KUSIKILIZA VIDEO HII INAYOFUNDISHA JINSI YA KUTENGENEZA MOJA YA BIDHAA ZA VIWANDANI ZINAZOPATIKANA KWENYE KITABU CHA #MILIKI KIWANDA MILIKI UCHUMI.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *