NJIA KUMI (10) UNAZOWEZA KUANZA KUTUMIA LEO KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO WA INTERNET.

Je wewe unatumia mtandao wa intaneti? Una simu ya kupangusa (smartphone) ambayo unaweza kuitumia kutembelea mitandao ya kijamii? Najua majibu yako ni ndiyo, kwa sababu mpaka umesoma hapa, lazima uwe unatumia mtandao wa intaneti.







Sasa swali muhimu zaidi ni hili;
Je umekuwa unatengeneza fedha kwenye mtandao huu wa intaneti kadiri unavyoutumia? Ulishatengeneza hata elfu moja, elfu kumi, laki na hata milioni? Kwa wengi ninaowajua, jibu lao ni hapana. Wao wamekuwa watumiaji pekee, lakini hawajawahi kutengeneza fedha kwenye mtandao huu wa intaneti.
Sasa leo nina habari njema kwako, kama na wewe ni mmoja wa wale ambao wanatumia mtandao lakini hawaingizi kipato kupitia mtandao wa intaneti. Leo nakwenda kukuambia ya kwamba, kwa hapo ulipo sasa, unaweza kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti.
Huhitaji kuwa na elimu ya ziada, huhitaji kuwa na mtaji wa kuanzia, wala huhitaji kuwa na vifaa vingi. Unachohitaji tayari unacho, ambacho ni simu yako ya kupangusa (smartphone) na kompyuta kama unaweza kupata.
Je unawezaje kutumia mtandao wa intaneti kutengeneza kipato?
Hapo ndipo pazuri na ndiyo utakachokwenda kujifunza kupitia makala hii, isome mpaka mwisho,
Kwanza kabisa kabla hujafikia kutengeneza fedha, unahitaji kutengeneza vitu vitatu.
Kitu cha kwanza; kuwa kwenye mitandao ya kijamii kibiashara.
Najua upo kwenye mitandao mingi ya kijamii, wasap, facebook, instagram na mingine ya aina hiyo. Lakini sina hakika ni mambo gani unafanya kwenye mitandao hiyo. Huenda umekuwa unafuatilia tu mambo ya watu, huenda umekuwa kwenye timu za kishabiki. Kwa njia hiyo huwezi kutengeneza fedha.

Mfano wa kuwa katika facebook kibiashara.










Ili uweze kutengeneza fedha kwenye mtandao, unahitaji kuwa kwenye mitandao ya kijamii kibiashara. Na hapa unachagua ni huduma gani ya maarifa na taarifa unaweza kuwapa wengine kupitia mitandao ya kijamii unayotumia. Maarifa na taarifa hizi unaweza kuzitoa kutokana na uzoefu ulionao, utaalamu ulionao na hata ujuzi ulionao.
Hivyo chagua mitandao ya kijamii unayoweza kuitumia kutoa maarifa na taarifa. Mizuri kwa kuanzia ni facebook, instagram na whatsapp.
Kitu cha pili; unahitaji kuwa na blog.
Blog ndiyo nyumbani kwako kwenye mtandao wa intaneti. Hapo ndipo watu wanapokutana na kazi zako zote. Kazi zako haziwezi kupotea kama umeziweka kwenye blog yako. Kwenye mitandao ya kijamii zinaweza kupitwa na kusahaulika, ila kwenye blog zitakuwepo milele.
Unahitaji kuwa na blog ambayo utaitumia kutoa taarifa na maarifa uliyodhamiria kuwapa watu ili baadaye uweze kutengeneza kipato. mfano wa blog ni kama huu www.shuletanzania.info
Kama utahitaji kufunguliwa blog na uanze kutengeneza fedha wasiliana nasi Whatsapp 0754745798.

Kitu cha tatu; unahitaji mfumo wa kutunza na kutuma barua pepe (email list).
Watu wanaokusoma na kukufuatilia kupitia mitandao ya kijamii na blog yako, watapenda kusikia zaidi kutoka kwako, hivyo wape nafasi ya kukupa wewe mawasiliano yao, moja wapo email ili uwe unawatumia vitu vizuri zaidi.
Watu hawa wanaokupa mawasiliano yao ni watu ambao wanakukubali na watakuwa tayari kupokea maarifa na taarifa zaidi kutoka kwako. Watumie maarifa na taarifa zaidi kwenye email zao na baadaye utaweza kutengeneza kipato kwenye mtandao.
Ukishakuwa na vitu hivyo vitatu muhimu, sasa unakuja kwenye kutengeneza fedha kwenye mtandao.
Zipo njia nyingi sana za kutengeneza fedha kwenye mtandao kwa kutumia blog. Hapa nitazitaja zile muhimu na nitazielezea zaidi kwenye makala zijazo.
  1. Kutangaza biashara yako na biashara za wengine kupitia mitandao ya kijamii na blog yako.
  2. Kutengeneza maarifa yako kwenye mfumo mzuri na kuwauzia wasomaji wako, kama cd, dvd, kitabu n.k
  3. Kuendesha semina kwa wasomaji wako, kwa njia ya kukutaka ana kwa ana au kwa njia ya mtandao.
  4. Kutangaza huduma zako nyingine kama ushauri.
  5. Kutoa makala za kulipia na watu kuwa wanachama wa blog yako.
  6. Kuuza bidhaa zinazoendana na maarifa unayotoa kupitia mtandao wa intaneti.
  7. Kuweka matangazo ya google na kulipwa kadiri watu wanavyobonyeza.
  8. Kushirikiana na makampuni au mashirika yanayoendana na maarifa unayotoa.
  9. Kutengeneza kundi la mafunzo kupitia mtandao wa whasap.
  10. Kuwaunganisha wasomaji wako na watu wenye huduma ambazo wanazihitaji.
Hizi ni njia za msingi kabisa unazoweza kuanza kuzitumia leo kutengeneza fedha kwenye mtandao.
Tutaendelea kuzichambua moja baada ya nyingine kwenye makala zijazo.
Tumia ujuzi, utaalamu na uzoefu wako kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti kupitia SHULE TANZANIA

Kwa msaada zaidi juu ya jinsi gani ufanye ili kutengeneza fedha kwa njia ya mtandao wa internet wasiliana nasi kwa mawasiliano haya;

0754745798-Whatsapp
piusjustus28@gmail.com

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *