MATOKEO YA DARASANI YASITABIRI MAISHA YAKO (Sehemu ya 2)

Habari za leo rafiki yangu, natumaini uko salama kabisa na unaendelea na harakati za kubadilisha maisha yako ili yawe bora zaidi.

Leo tumekutana tena katika muendelezo wa makala yetu ya jana tar. 08/03/2017 iliyokuwa inasema MATOKEO YA DARASANI YASITABIRI MAISHA YAKO, Naamini uliisoma na kuielewa, kama hukubahatika kuisoma basi bonyeza hapa kuisoma kwanza kabla hujasoma hii ya leo.

Tulipoishia jana;

Kuna siku nilikuwa nikijaribu kupitia Yutube nikawa naangalia watoto wadogo huko U.S.A ambao wako shule wanafundishwa jinsi ya kumiliki makampuni yao na kuweza kuyaendesha wao wenyewe hapo hapo kwa chini kukawa na baadhi ya clips za watoto ambao ni matajiri duniani wengine hata hawajafika miaka 18 lakini ni millionea. Nikawa najiuliza umri kama huu kwa vijana hapa Tanzania ndio kwanza anapewa mitihani ya kutoa maana na kuelezea kuhusu Berlin Conference na kusoma kuhusu kutafuta thamani ya X mwisho wa siku unaanza kutafuta kazi au kuishia mtaani kuhangaika. Sasa hapo ufunguo wa maisha uko wapi?
Kama mwanafunzi anafundishwa kujua vya wengine kuliko kujijua mwenyewe au mwanafunzi anafundishwa kujua vya wengine lakini hata hafundishwi kuhusu maeneo makubwa Tanzania ambayo yako wazi na jinsi ya kuyatumia. Ndio maana tunalalamika hakuna ajira kwa sababu ndivyo ambavyo tumewekwa kuona kwamba sisi sio kitu na wala hatuwezi kufanikiwa bila kutumiwa na wengine.
Tunahitaji kubadilisha hali hii, ni lazima tuwe na huruma na maisha ya watu maana wengi wana mambo makubwa ambayo wanaweza kuyafanya na kubadilisha nchi hii lakini wakishaingia katika wazo la elimu, ndoto zao kubwa huwa zinakufa kwa asilimia kubwa. Hiyo inatokea kwa sababu maana anakutana na mazingira ya kujifunza ambayo kwa asilimia kubwa yanahimiza kutumiwa/kutumika (yaani kuajiriwa) sio kutumia ulichokuwa nacho. Hii ni mbaya na imepoteza mafanikio ya watu wengi. 

Elimu hii ya darasani isitupe samaki kila siku kwa kudhani wataweza kumaliza shida zetu ila elimu inatakiwa itoe ndoano na nyavu halafu watupe elimu ya jinsi ya kuzitumia na sisi hatutarudi kila siku kulalamika kwa nini hawatupi samaki.

Yoko Ono moja ya wasanii huko Amerika aliwahi kusema ” If your life changes, you can change the world too”
Akimaanisha kwamba “Maisha yako yakibadilika tunaweza badilisha Dunia pia”

Katika jamii zetu kuna matabaka mawili makubwa ambayo ni maskini na Tajiri na kwa asilimia kubwa ukiuliza watu kuhusu haya majina mawili yametoka wapi, utapata majibu mengi kutoka kwa kila mmoja. kwenye jamii zetu mtu akisoma na kupitia madaraja mengi unachukuliwa kama umefanikiwa hata kama akaunti hazisomi vizuri. Lakini mtu akifeli darasani anaonekana kama hana akili au hawezi kitu katika maisha.

Binafsi naamini kwamba mtu ambaye amefeli darasani kama kungekuwa na sector (idara) nyingine ambayo inachukua hawa watu ambao wanafeli katika masomo na kudharauliwa, naamini Mabilionea wangekuwa wengi sana lakini jamii imezungukwa na watu wengi ambao maono yao bado yako katika imani za karne ya 16 kwamba bila kwenda darasani hakuna ambacho unaweza kufanya.

Hebu jiulize kuhusu hawa wanasayansi kama Galileo Galilei, Issac Newton, Achimedes, au wanafilosofia kama Aristotle, Plato, na wengine wengi hawakuwa Madaktari au Maprofesa au wenye Masters kugundua vyote hivyo ambavyo leo unaambiwa bila darasa huwezi kuvumbua! Tunawasoma na tunaheshimu mawazo yao japo wengi wao hawakuwa na elimu kiwango cha ajabu sana. Haya ni mawazo potofu kabisa.

SOMA: Zijue fursa za waziwazi za biashara mwaka 2017


……………………………Itaendelea kesho……………………..

tafadhali endelea kutembelea ukurasa huu www.shuletanzania.info ili upate muendelezo wa mada hii.

Kama imekugusa usiache kutoa maoni yako kwa kukoment hapa chini au tuandikie whatsapp au text kwa no. 0754745798

Asante,

Karibu sana.

Pius Justus Muliriye

0754745798
0657128567
piusjustus28@gmail.com

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *