MATOKEO YA DARASANI YASITABIRI MAISHA YAKO. (Sehemu ya 1)

Habari rafiki yangu na msomaji wangu wa mtandao huu wa Shule Tanzania, Asante sana kwa kuendelea kuwa na mimi katika muendelezo huu wa makala za kukuhamasisha kutambua kipaji ulicho nacho ndani yako katika kutatua changamoto ya maisha yako.


Leo nimeamua kuandika kuhusu mada hii kwa sababu muhimu sana. Hii imetokana na kupigiwa simu na msomaji wangu mmoja na mfuatiliaji wangu wa facebook page yangu ya THINK BIG START SMALL baada ya kuomba mtu yeyote mwenye tatizo anipigie nimpe ushauri. Aliniambia mambo mengi na hii ndio imenipelekea kuandika mada hii ya MATOKEO YA DARASANI YASITABILI MAISHA YAKO.

Basi tuendelee;

Mara nyingi nimekuwa nikiwaza kuhusu hili naangalia chini, maana kama ningeitwa na kuulizwa nini chanzo cha watu kuwa maskini cha kwanza kabisa ningesema ni mawazo ambayo watu wanaambiwa kuhusu elimu ya darasani. Nilishasikia kwamba ukifeli darasani umefeli maisha na walimu wamesisitiza sana jambo hili wakiongeza pia kwa kusema usiposoma umeharibu maisha.

Binafsi sitasahau msemo wa elimu ni ufunguo wa maisha, lakini nashindwa kuelewa kwamba kwanini huu ufunguo ni mpaka uvae jezi kuupata au inakuaje kwamba ni lazima ufanye mitihani na ufaulu ndio uupate? kwa mawazo yangu ufunguo wa maisha ambao tunaambiwa kwamba tunaupata katika kusoma darasani na kupanda madaraja ni wa ubaguzi, usishangae kwa sababu gani nasema hivyo.

Navyojua mimi, sifa mojawapo ya ufunguo ni kufungua kufuli ambalo tunaweza kuchukulia kama giza lililotanda katika akili zetu kusonga mbele, lakini Elimu ya sasa haitoi ufunguo tofauti inachofanya inatoa funguo moja tu ambao haufungui kila mlango. 

Elimu ya darasani ni kujifunza na tunatakiwa kutambua kwamba, kujifunza kupo kwa aina tofauti sio hii ya kukariri na kwenda kupimwa kumbukumbu zako katika mtihani na baada ya hapo mtu anasahau na kukumbuka vichache. Kuna kujifunza kwa kusikia, kuna kujifunza kwa kugusa, kuna kujifunza kwa kusikiliza hadithi, kuna kujifunza kwa kuona mfano kuangalia video.
Hapa nina maana gani? Mwanafunzi anapofeli darasani ni amefeli kwa kujifunza kwa kuona na kusikiliza, lakini je, kama mwalimu unaposema mwanafunzi kwamba hana akili au kumlaumu kwamba kwa nini amefeli umefanya jitihada gani kuangalia aina nyingine za kumsaidia mwanafunzi kujifunza? Maana sio kila mmoja anaweza kuelewa kwa kujifunza kwa aina tofauti mfano kwa picha na vitendo.

Naamini kwamba mwanafunzi asilalamikiwe kwa kufeli darasani ila njia ambayo inatumika kumfundisha mwanafunzi ndizo zinazotakiwa ziangaliwe kwa umakini zaidi, kwa sababu hakuna mwanafunzi ambaye hana akili lakini njia inayotumika kumfikishia  ujumbe inawezekana ikawa tofauti na yeye anavyoweza kuelewa.

Kuna siku nilikuwa nikijaribu kupitia Yutube nikawa naangalia watoto wadogo huko U.S.A ambao wako shule wanafundishwa jinsi ya kumiliki makampuni yao na kuweza kuyaendesha wao wenyewe hapo hapo kwa chini kukawa na baadhi ya clips za watoto ambao ni matajiri duniani wengine hata hawajafika miaka 18 lakini ni millionea. Nikawa najiuliza umri kama huu kwa vijana hapa Tanzania ndio kwanza anapewa mitihani ya kutoa maana na kuelezea kuhusu Berlin Conference na kusoma kuhusu kutafuta thamani ya X mwisho wa siku unaanza kutafuta kazi au kuishia mtaani kuhangaika. Sasa hapo ufunguo wa maisha uko wapi?

SOMA: Zijue fursa za waziwazi za biashara mwaka 2017

………………………………Itaendelea kesho……………………..
tafadhali endelea kutembelea ukurasa huu www.shuletanzania.info ili upate muendelezo wa mada hii.

Kama imekugusa usiache kutoa maoni yako kwa kukoment hapa chini au tuandikie whatsapp au text kwa no. 0754745798

Asante,

Karibu sana.

Pius Justus Muliriye
0754745798
0657128567
piusjustus28@gmail.com
www.shuletanzania.info

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *