UVIVU WAKO WA KUFIKIRI NDIO UMASKINI WAKO

Habari rafiki yangu na msomaji wangu wa makala zangu za kila siku, Natumai uko salama kabisa na unaendelea na juhudi za kuboresha maisha yako. Nikupongeze kwa kuwa uko katika mstari wa mafanikio, kwani mafanikio ni juhudi unazoziweka kila siku katika kazi zako, iwe kazi binafsi au hata ajira.

Nikukaribishe tena kwenye mfululizo wetu wa makala zetu za kila siku kama ambavyo huwa nafanya kila siku;

Leo napenda kuzungumzia nguvu iliyoko katika kufikiri.

Nimeshawahi kusema kwamba, kufikiri ni bure, chukua muda na kaa peke yako ufikiri unataka nini katika maisha yako, na hapo ndipo utaona fikra ikifunguka na kufanya maajabu ambayo hata hukutegemea.

Watu wengi wamekuwa wakilalamika sana kuhusu hali ngumu ya maisha kwa sasa, hii ni kweli kabisa, hali ni ngumu sana, tena sana, lakini katika muda huu huu mgumu ndio muda mzuri wa kutengeneza faida katika biashara yako.

Katika wakati huu mgumu ndipo unatakiwa kufikirisha akili yako ili uone nini jamii inahitaji na fanyia kazi, nakuhakikishia utatengeneza pesa nyingi sana. 

Huu ndio muda watu wengi wanafunga maduka na kuzikimbia biashara zao, na huu ndio wakati wa wewe kuchukua changamoto kama hii kama fursa kwako, wakati wanafunga, wewe fungua, badili mfumo wa biashara yako na hatimaye utatengeneza faida kuliko mtu yeyote anayekuzunguka.

Mimi ni muajiriwa, lakini sikubweteka na kuridhika na mshahara wangu ambao hata nifanyeje hakidhi mahitaji yangu. Nilikaa chini na kufikiri sana nifanye nini ili niongeze kipato changu, ndipo nikapata wazo la kuanzisha kiwanda ambacho kinazalisha bidhaa mbalimbali. Kama unataka kujua nazalisha nini bonyeza maandishi haya. 

Nimekuwa nikiwaza sana vijana wa kitanzania wanaeleka wapi nakosa jibu kabisa, kwani walio wengi wamesoma lakini elimu zao haziwasaidii kuwaza nje ya box, nimekuwa nikiona wahitimu wengi wakilalamika kila siku ukosefu wa ajira na huku wamekaa tu nyumbani bila kufanya chochote kuinua maisha yao, kwa kuliona hilo nikaamua kwasaidia kwa kuandika kitabu ambacho kitawafungua fikra ambazo zinawafanya wadumae na washindwe kutumia mazingira yao kujiongezea kipato.

Niliamua kuandika kuhusu UZALISHAJI WA BIDHAA MBALIMBALI, nimejaribu kuelezea kwa vitendo kuanzia hatua ya kwanza mpaka ya mwisho ya uzalishaji wa bidhaa hizo, ukiwa na kitabu hiki kitakufundisha kutengeneza unga wa lishe hatua kwa hatua, utengenezaji wa tambi za dengu, sabuni aina zote (na hii ndio ina faida nyingi kuliko  zote), kutengeneza chaki na bidhaa nyingine nyingi sana zaidi ya kumi ambazo zina soko hapa Tanzania.

Kama unahitaji kopi ya kitabu hicho Bonyeza maandishi haya.

Narudia tena kusema, hali ni ngumu sana kiuchumi, lakini ndio muda wa kutengeneza faida zaidi, ndio muda wa kuchukua fursa na kufanyia kazi, acha kulalamika, nguvu hiyo ihamishie kwenye kuzalisha bidhaa, naamini utatoboa tu. 
Remember….“Thinking is Free”

Kama utahitaji ushauri juu ya nini ufanye kulingana na mazingira yako, basi usisite kuwasiliana na mimi kwa mawasiliano haya;

Pius J. Muliriye
0754745798-Whatsapp/text
0657128567
piusjustus28@gmail.com

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *