MAMBO MAKUU MAWILI YANAYOWANGUSHA WAJASIRIAMALI/WAFANYA BIASHARA WA KITANZANIA.

Habari rafiki yangu mpendwa sana;

Natumaini leo uko salama kabisa na unaendelea vizuri na harakati za kubadili maisha yako kuwwa bora zaidi.
Leo ningependa tuzungumze kidogo kuhusu wajasiriamali au wafanya biashara hapa Tanzania na changamoto zao ambazo kwa namna moja au nyingine wanashindwa kufikia mafanikio waliyoyatarajia.
Kama wewe ni mfanya biashara wa kitu chochote kile basi unaweza ukawa umeshakumbana na tatizo hili na hatimaye kukurudisha nyuma kabisa katika maisha yako.
Yafuatayo ni mambo mawili nyeti sana ambayo kwa namna moja au nyingine yanawarudisha nyuma wajasiriamali au wafanya biashara hapa Tanzania.

  • KUKOSA ELIMU YA BIASHARA.
Hii ni moja ya changamoto mbayo ni kubwa sana  ambayo kwa namna moja ama nyingine inawaumiza wafanyabiashara walio wengi bila hata ya wao kujua.
Wengi wao wamekosa elimu ya biashara na ndio maana kila siku wanaanguka, wanaoanza biashara wanashindwa ndani ya mda mfupi sana.
Wengi wao wanatumia uzoefu tu walionao katika biashara, na hata miaongoni mwao wanatumia bahati tu katika kufanya biashara zao, na watu wengine wanaenda mbali zaidi na kuamini katika vitu vya ajabu ajabu kama ushirikina na uchawi wakidhani utawasaidia kufanikiwa katika biashara zao.
Wengine wamekuwa wakiwatoa sadaka ndugu zao wa karibu wakidhani watafanikiwa. Nikwambie tu, hakuna mafanikio ya kibiashara katika kumwaga damu ya mtu, watu wengi hufanya hivi kwa kukosa tu elimu ile ya msingi ya biashara.
  • KUKOSA MASOKO NA UJUZI WA KUTAFUTA MASOKO.
Hili pia limekuwa sugu sana kwa wajasiliamali walio wengi na imefikia wakati wanakata tamaa na kuona biashara ni mbaya sana na wengine hata kuacha biashara zao.
Hii ni kwa sababu watu wengi hawataki kuwekeza katika elimu ya msingi kabisa kuhusu masoko.
Kuna ujuzi mmwingi sana ambao ukiujua basi itakuwa rahisi sana kupata masoko na bidhaa yako kuuzika sana kuliko ya mwingine. Lakini ukitaka hili ukubari kulipa gharama za kujifunza hili.
Katika kitabu changu kipya kitakachotoka hivi karibuni kitakachozungumzia NJIA 10 ZA UHAKIKA ZA KUPATA MTAJI WA KUANZISHA BIASHARA YAKO, kitaelezea kwa kina sana jinsi ya kuweza kupata masoko, kitakupa njia nyingi sana za kuweza kuteka soko na hatimaye uwe mfanyabiashara bora kabisa kuliko wote wanaokuzunguka.
Kwa leo niishie hapo; kama una lolote la kuweza kuniambia au kuniuliza basi usisite kuweka comment yako hapa chini au niandikie au kunipigia 0754745798/0657128567 na tutazungumza kwa kina.
Pia usisahau kujaza fomu hapa chini kabisa ili uwe karibu na masomo yatakayokuwa yanarushwa kila siku katika mtandao huu. KARIBU SANA.
Asante sana, nikutakie siku njema.
Pius J. Muliriye
0754745798
0657128567
piusjustus28@gmail.com

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *