MWAJIRI HANA MPANGO NA WEWE!!!

Habari rafiki yangu mpendwa na mfuatiliaji wa makala haya katika mtandao huu, Natumai hujambo kabisa, na unaendelea vizuri na kuboresha maisha yako.Napenda kukupongeza sana kwa kuendelea kusoma makala haya kila siku ninaposhare na wewe, wewe ni miongoni mwa watu walioko serious sana na maisha yao, endelea kujifunza, naamini utafanikiwa tu.

Leo napenda nizungumzie uhusiano uliopo kati ya MWAJIRI na MWAJIRIWA. Hawa watu huwa wanafanya kazi kwa pamoja sana na pia wanategemeana sana katika ustawi wa kila mmoja.
Kama leo hii ningeulizwa ungependa kufanya kazi gani kati ya kuajiriwa au kufanya kazi binafsi, hakika ningejibu kwa herufi kubwa kwamba ningependa kufanya kazi zangu binafsi, kwa kifupi ningetamani kufanya kitu changu ambacho kingenifanya niajiri watu wengine wafanye kazi badala yangu.

Nimesema hivo kwa nia nzuri tu, simaanishi kuajiriwa ni kubaya, la hasha! kwani hata mimi ni mwajiriwa ambaye nimeona uzuri wake na ubaya wake pia nimeuona.

Nataka kusema kwamba, siku zote mwajiri hana mpango na mtumishi wake kabisa, lengo kuu la mwajiri ni kwamba amtumie mtumishi wake ili apate faida kubwa lakini amlipe kidogo sana, na ndio maana matatizo ya waajiriwa hayaishi hata wakilalamika vipi.

Lengo la mwajiri ni kumnyonya mtumishi wake ili azalishe zaidi na anufaike kutokana na juhudi zake, na hilo ndio lengo kuu la waajiri walio wengi.

Wakati sijaanza kuwa mdadisi sana nilidhani wafanya kazi walioajiriwa wanafaidi sana kuliko mtu yeyote yule, kumbe ni kinyume chake, angalia wafanya kazi ambavyo wanalia kila siku, wana matatizo ambayo hayaishi, wana madeni kila kona, si kwamba wanapenda kuwa na madeni, ni ugumu tu wa maisha na kipato kidogo kisichokizi mahitaji yao kwani wanatumia muda mwingi sana katika siku yao kumfanyia kazi mtu mwingine lakini analipwa kidogo. 

Kama wewe umeamua kufanya kazi zako mwenyewe maana yake muda wote katika siku yako utakuwa unafanya kazi kwa ajiri yako, na mapato unayopata yote ni yakwako, na wewe ndo utaamua uajiri watu wangapi ili wafanye kazi badala yako na wewe uishi kama mfalme.

Leo napenda nikuase wewe kijana mwenzangu, bado una muda mwingi sana wa kuanzisha kampuni yako mwenyewe, biashara yako mwenyewe na hatimaye uweze kufikia ndoto zako ukiendelea kuajiriwa maana yake unatimiza ndoto za mwingine.
Mwajiri atakutumia sana, atakulipa vizuri uzeeni ambapo pesa hizo hazitakuwa na maana tena kwako kwani utakuwa umechoka taabani, na hapo ushukuru Mungu umefikia muda huo wa kustaafu kwani life expectancy ya watanzania wengi haifiki muda wa kustaafu. Chukua hatua mapema sana.

Kama unapata shida ni biashara gani ufanye usikae kimya, ongea na watu, nipigie simu 0754745798/0657128567 nikusaidie kuchagua ni biashara gani ufanye ili upate faida kubwa na hatimaye umiliki kampuni kubwa sana na uajiri watu wengine.

Pia unaweza kuchagua ni biashara gani ufanye kati ya hizi AINA YA BIASHARA KULINGANA NA SEHEMU UNAYOISHI

Nikupe mfano ambao umetokea leo hii na hapo ndio utajua mwajiri wako hana mpando na wewe;Kwa watumishi wote wa sekta zote unaweza sasa kugundua kuwa mwajiri hana mpango wa kuboresha maisha yako kama hutajiongeza na kufikiri nje ya box. Leo hii wafanya kazi wanadai malimbikizo ya mishahara yao, wanadai pesa za likizo kwa miaka mingi, wanadai kupandishwa madaraja kwa mujibu wa sheria kwa muda mrefu sasa, wanadai kuongezewa mishahara haikidhi mahitaji yao lakini mwajiri wao bila huruma hatatui matatizo yao ila inatafuta namna ya kuzidi kumpunguzia mshahara wake huyu mtumishi. Usipofikiria juu ya kuondokana na hili utakaa kulaumu tu na hutapata suluhisho ya hili.

Acha kukaa kijiweni ka kuongea sana juu ya hili, jifiche ndani ikiwezekana chini ya uvungu, jipe muda wa kufikiri sana ili upate wazo la biashara ya kufanya uondokane na utegemezi huu ambao ni hatari kwa maisha yako ya baadae.

Anza sasa, usifikiri kuhusu mitaji mikubwa sana, anza na kidogo ulichonacho, unganeni, anzisheni viwanda naamini mtatoboa tu.

Asante kwa kuwa na mimi mpaka sasa, naamini utachukua hatua juu ya hili;

Pata wazo la BIASHARA HAPA.

Kama unatafuta sehemu ya kuwekeza pesa zako ili upate faida kila mwisho wa mwezi ya 10% hadi 15% BONYEZA HAPA.

KARIBU.

Kwa mawasiliano zaidi;

Pius Justus Muliriye
0754745798
0657128567
piusjustus28@gmail.com

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *