JINSI TULIVYONUSURIKA KIFO MIMI NA MPENZI WANGU.

Habari rafiki yangu mpendwa na msomaji wangu wa mtandao huu;








Leo napenda nikushirikishe katika stori mbaya sana ambayo imetaka kugharimu maisha yangu mimi na mpenzi wangu nayempenda sana.

Ilikuwa jioni ya saa 1 kama na nusu hivi ambapo mimi na mpenzi wangu, mwanamke ambaye nampenda sana kuliko kawaida. Tulikuwa tumetoka out kwa ajili ya kupata chakula cha jioni  na vinywaji jijini Mwanza.

Tulipomaliza ilibidi nimrudishe mpenzi wangu nyumbani kwao kwani bado alikuwa ni mwanafunzi na alitakiwa kuwa nyumbani kabla ya saa 12 jioni.

Mpenzi wangu huyo alikuwa akiishi maeneo ya Nyamanolo jijini mwanza njia ya kuelekea uwanja wa ndege wa Mwanza. 
Kwa kuwa nyamanolo haiko mbali sana na mjini basi tulishawishika kutembea mimi na yeye ili tuwe tunaongea ongea njiani na ndipo tulipoanza safari kuelekea nyamanoro.

Baada ya hatua chache kutoka katika round about ya nyerere karibu kabisa na jengo la CCM ilipo radio ya Passion ndipo tulipopatwa na tatizo ambalo isingekuwa ujasiri niliokuwa nao tungeweza kuumia sana na hata kupoteza maisha kabisa.

Tulipolivuka daraja mbele kidogo nikasikia mpenzi wangu ghafla akiniambia kwa sauti kubwa Pius unaibiwaaaa!!! ndipo hapo nikagundua kuna mtu yuko nyuma yangu na kuniwahi na kuingiza mkono wake kwenye mfuko wangu ili achukue simu yangu huku akinichoma choma na kitu chenye incha kali kama bisbis vile.

Wakati tukio hilo likiendelea kumbe mpenzi wangu naye kakabwa shingo na kibaka mwingine, kumbe walikuwa wawili wakijaribu kutuibia. Cha kushangaza watu walikuwa wakipita na magari pia yalikuwa yakipita na wala hakuna aliyejaribu hata kutaka kutusaidia, ndio ujue kuwa binadamu si mtu wa kumtegemea sana katika maisha yako hasa pale unapokuwa na shida.

Basi kama unavyojua, ukitaka kujua hasira za mwanaume, mchokoze pale anapokuwa na mpenzi au mke wake, hapo huwa hataki masihara kabisa na hataki kuaibika mbele ya mke wake. Hapo ndipo nilipojiambia moyoni “Pius, you are a Man, FIGHT” ndipo nilipata nguvu za ajabu sana zilizonifanya nipigane mpaka point  yangu ya mwisho. Nakumbuka aliyekuwa akinichoma bisbis kwenye bega nilimpiga kiwiko cha mkono akadondoka barabarani nusura akanywagwe na gari, kwa bahati nzuri hakufanikiwa kuchomoa simu yangu iliyokuwa mfukoni.

Baada ya kumshinda huyo ndipo nikageuka nyuma na kukuta mpenzi wangu amekabwa shingo yake na hakuweza hata kuzungumza tena na tayari alikuwa ameshapoteza kiatu chake, ndipo nikajawa na hasira ambazo zilinifanya niruke mithiri ya chui akiwa mawindoni, nilirusha ngumi moja yenye uzito mkubwa sana zaidi ya tofali la zege na likampata yule kibaka kwenye paji lake la uso na kudondoka chini wote yeye na mpenzi wangu huku akivuja damu kutokana na uzito wa ngumi ile.

Nilimuwahi mpenzi wangu na kumyanyua pale chini na hapo yule kibaka alipata upenyo na kukimbia kusikojulikana. 

Mpenzi wangu alikuwa akihema sana, na alipata mshituko wa tukio lile, lakini kwa bahati nzuri hawakuweza kumuibia chochote pia. 
Ndipo nilipotafuta viatu vyake na kumvalisha na kusimamisha gari (daladala) na kupanda huku mpenzi wangu akinilalia kifuani huku akihema sana kwa sababu ya tukio lile. Na ndipo nilipomfikisha kwao na kwa macho ya huzuni na mahaba akanikiss na kuniambia asante sana umeokoa maisha yangu, nami nikamjibu, wewe ndio kila kitu kwangu na nitahakikisha nakulinda na chochote kibaya. Na akaniacha akaenda nyumbani huku nikibaki na furaha moyoni kwani uanaume wangu ulionekana mbele ya mpenzi wangu na kuniongezea umaridadi kwake.

Kwanini nimeamua kukupa stori hii?

Ni kwamba, watu wengi sana tunashindwa kuchukua hatua ya kufanya kitu ambacho kitakufanya uishi maisha bora kipindi uko hai kwani hujui ni siku gani utapatwa na mauti, ni jambo lisilopendeza kama wewe umeishi duniani halafu hujatimiza kusudi la wewe kuwepo hapa duniani.

Kwa mfano mimi ningeweza kupoteza maisha yangu kipindi kile maana yake ningekuwa nimepoteza ndoto yangu ya kueleimisha watanzania kama navyofanya hivi sasa.

SOMO:

Chukua hatua haraka iwezekanavyo, usisubiri kesho, kwani kesho haitafika hata siku moja, acha visingizio kwamba huna pesa za kuanzisha biashara yako, anza kidogo kidogo, anza na uliichonacho utafanikiwa tu. 

Kumbuka, kifo kinakuja bila hodi, chukua hatua katika maisha yako uache alama katika dunia hii.

Kama unahitaji kufanya biashara yenye faida na bila kikomo huna budi kujiingiza katika uzalishaji wa bidhaa za viwandani na hapo utapata faida kubwa sana. Tengeneza bidhaa kama Sabuni za mche, sabuni za maji, sabuni za kusafishia vyoo, kuoshea magari, unga wa lishe, batiki, n.k na nakuhakikishia hii ni biashara yenye soko kubwa sana hapa Tanzania, hakuna mtu asiyetumia sabuni, kila mtu anatumia, kumbe una soko kubwa sana karibu yako.

Kama unataka mwongozo na hatua za kufanya katika uzalishaji wa bidhaa kama hizo BONYEZA HAPA

Tafadhari usiache kunipigia kama utahitaji ushauri wowote katika biashara, nina uwezo wa kukushauri ni jinsi gani ufanye ili uweze kumiliki biashara yako na hatimaye kufanikiwa katika maisha yako.Pia nina mbinu nyingi sana ambazo zitaweza kukusaidia wewe kupata mtaji wa kuanzisha au kuendeleza biashara yako.

Chati  na mimi whatsapp 0754745798 tuzungumze.


Wasiliana nami;

Pius Justus Muliriye 
0754745798
0657128567

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *