Uongo ni katika kitu ambacho hata maandiko matakatifu yamekataza,watu weeengi huwa wanajua uongo ni kuwaongopea wengine lakini pia kumbe hata wewe mwenyewe huwa unajiongopea ACHA KUJIDANGANYA.
Maswala ya kutaka kuyabadilisha maisha yako wakati wewe mwenyewe hutaki kubadilika huo ni uongo.
Kuamini kuwa unajua kila kitu na huwezi tena kujifunza kutoka kwa wengine huo ni uongo maana kiuhalisia kila unapojua kitu ndio unagundua hujui chochote.
ACHA KUJIDANGANYA
Kukalia kila siku unataka vitu vya Bure hutaki kutoa mchango wako wowote ili kulipia gharama za mafanikio yako huo ni uongo.
ACHA KUJIDANGANYA
Kukalia kusali tuuu na kuomba halafu hutaki kujishugulisha unafikiri Mungu atashusha gunia LA pesa huo ni uongo
ACHA KUJIDANGANYA
Kuamini kuwa kuna maisha ya kulala masikini na kuamka tajiri hutaki kuwa mvumilivu huo ni uongo mkubwa sana.
ACHA KUJIDANGANYA
SALA YA LEO
Asante Mungu kwa maana leo ni siku nyingine tena,naamini kuanzia leo nitasema katika moyo wangu ukweli maana ukweli utaniweka huru.Amen
Naamini umesema AMEN!!
SOMA: Ndoto yako ni ipi?
Asante sana kwa kuwa na mimi.
Wasiliana nasi kama unahitaji ushauri wowote kuhusu maisha;
Pius Justus Muliriye
0754745798
0657128567
piusjustus28@gmail.com
Kama una ndoto ya kumiliki biashara yako ambayo itakuletea kipato siku zote za maisha yako, basi huna budi ya kuanzisha kiwanda cha kuzalisha bidhaa mbalimbali kama hizi zilizoorodheshwa kwenye kitabu hiki cha MILIKI KIWANDA MILIKI UCHUMI. Kitabu hiki kitakufundisha hatua kwa hatua jinsi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali kwa kutumia technolojia rahisi sana na kutengeneza faida kubwa sana.
Bonyeza picha hii kupata kitabu hicho;