HUU NDIO MTIHANI, KILA MTU LAZIMA APITIE

Habari ndugu msomaji wa makala zangu,tazama leo ni siku nyingine nzuri kabisa ambayo Mungu ametupatia ili tuweze kufanya kitu ambacho hatujawai kufanya ili tupate matokeo ambayo hatujawahi kupata na maisha yetu yaweze kubadilika.


Leo nataka kuongea na wewe kuwa kwenye maisha hakuna ushuhuda pasipo kuwa na mitihani.
Kuna mwanamziki mmoja wa mziki wa injili amewahi kuimba kuwa jinsi Mungu anavyokupatia mitihani kwenye maisha ndivyo anakuandalia ushuhuda.Hii ni kweli kabisa siku zote kwenye maisha watu ambao wameweza kutoa ushuhuda ni wale tu ambao wameweza kupitia mitihani kwenye maisha yao,na jinsi mtihani wako unavyokuwa mkubwa ndivyo na ushuhuda wako utakuja kuwa mkubwa sana.

Kwenye kitabu kitukufu qur’an Mungu ametuambia kuwa “hivi mnafikiri nitawaacha tu hivi hivi? Hapana nitawajaribu kwa magonjwa,njaa na umasikini” hiyo ni ahadi ya Mungu katika mitihani lakini ukiangalia kwa undani sana watu wengi ambao walijaribiwa kwa umasikini leo ni mashuhuda wa maisha yao kuwa maisha yao yamebadilika.Nataka niongee na wewe ambae muda huu unapitia mtihani wako,unaweza kuwa ni magonjwa,unaweza ni umasikini,uko kwenye madeni makubwa,unaweza kuwa ni ndoa matatizo yamekuzidi,unaweza kuwa ni njaa haijalishi ni mkubwa kiasi gani lakini kitu kimoja unapaswa kujua ni kuwa Mungu anakuandalia ushuhuda.

Hakika usikate tamaa wala kulalamika maana kwenye maisha hakuna ushuhuda pasipo mitihani na Mungu hawezi kukupa mtihani ambao hauna mlango wa kutokea amini kutoka moyoni kuwa siku moja utatoka hapo ulipo na utakuwa na maisha mengine kabisa.

Asante kwa kuendelea kuwa na mimi rafiki.


wasiliana nasi;

Pius J. Muliriye
0754745798
0657128567
piusjustus28@ggmail.com

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *